MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
SPIKA mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania, Anne Makinda amesema kuchaguliwa kwa Dk John Magufuli kuwa Rais wa Awamu ya Tano, kumenusuru Watanzania na machafuko yaliyokuwa yakielekea kutokea.
Huku akipongeza mtindo wa Magufuli kuweka nchi sawa maarufu utumbuaji majipu, ambao umekuwa ukikosolewa na viongozi wa Chadema, Makinda amesema machafuko hayo, yalikuwa yasababishwe na tofauti kubwa ya vipato vya wananchi baina ya masikini na matajiri.
Alisema hayo jana alipozungumza na wanahabari kwenye mkutano wa kupitia utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania (Sagcot), katika Kongani ya Ihemi inayohusisha mikoa ya Iringa na Njombe.
“Tungeendelea tulivyokuwa tunaendelea, hakika tungekuja kuuana kwa sababu wenye nacho waliendelea kupata zaidi na wasio nacho waliongezeka kwa kuwa watumwa wa wenye nacho,” alisema Makinda.
Mamilionea bila kazi
Makinda katika mazungumzo yake ya jana, alisema bahati mbaya iliyokuwa ikilikumba Taifa ambayo mwenye suluhisho lake ni Rais Magufuli, ni baadhi ya matajiri kutoeleweka wanafanya kazi gani, lakini wakifikia mafanikio waliyonayo kutokana na kunufaika kijanjajanja na fedha za Serikali.
“Kuna watu walikuwa hawaeleweki wanafanya kazi gani, lakini ni mamilionea, baadhi yao ndio wale walikuwa wananufaika na mamilioni ya Serikali,” alisema.
Makinda alisema katika kuiweka nchi sawa katika nyanja mbalimbali, kila Mtanzania ataonja machungu yatakayokuja kuliponyesha Taifa mbele ya safari.
“Kutakuwa na magumu, wengi watasema aah huyo bwana mbona kabana hivi, lakini ni muhimu Watanzania wajue hii ni oparesheni kubwa itakayotuumiza wote, lakini mwisho wa yote Taifa na Watanzania tutapona,” alisema.
Aliwataka Watanzania waendelee kumuombea kwa Mungu Dk Magufuli ili aendelee kuwa na afya njema, busara na afanye kazi kwa kasi aliyoanza nayo hadi atakapomaliza awamu yake.
SOURCE: Habarileo