Makinda: nikiukandamiza upinzani nchi haitotawalika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makinda: nikiukandamiza upinzani nchi haitotawalika!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mujumba, Mar 13, 2011.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  [​IMG]
  Spika wa Bunge, Anne Makinda  Spika wa Bunge, Anne Makinda, ametabiri kuwa mkutano ujao wa Bunge utakuwa moto kuliko uliopita na ameapa kwamba hatakipendelea Chama cha Mapinduzi (CCM) kwani akifanya hivyo anaweza kusababisha machafuko nchini na kusababisha nchi isitawalike.
  Aliyasema hayo jana mjini Bagamoyo wakati akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari baada ya kufungua semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na ofisi ya Bunge.
  Kuhusu swali kwamba anaonekana kupendelea CCM, Makinda alisema hawezi kufanya hivyo kwa kuwa jambo hilo ni la hatari na wananchi hawatakubaliana nalo kwa kuwa hali hiyo inaweza kusababisha ghasia na nchi kutotawalika.
  “Kwa dini yangu mimi naapa kabisa sitapendelea chama chochote cha siasa, ukipendelea chama fulani wananchi wanaona, vyombo vya habari vinaona na unaweza kusababisha nchi isitawalike kabisa,” alisema Makinda.
  “Siwezi kukandamiza upinzani hata kidogo, hii nafasi ya Spika ni nafasi nyeti sana huwezi ukafanya mchezo huo maana amani itatoweka na kitakachofuata ni machafuko, na nimeapa sitapendelea kwa kuwa naogopa kuokota makopo barabarani,” alisema Makinda.
  “Mimi natambua mamlaka na majukumu niliyopewa kikatiba, katika kuliongoza Bunge hivyo siwezi kujiingiza katika ushabiki na maamuzi ya aina yoyote ya upendeleo kwa sababu najua kwa kufanya hivyo naweza kuiingiza nchi katika machafuko makubwa,” alisema.
  Akizungumzia malumbano ya wabunge, alisema hayo ni mambo ya kawaida katika mabunge yote duniani na wengine katika nchi mbalimbali wamekuwa wakifikia hatua ya hata kupigana.
  Alisema wananchi hawana sababu ya kushangaa mijadala mikali iliyotokea kwenye Mkutano wa Pili uliopita kwa kuwa siku zijazo inaweza ikatokea mijadala mikali zaidi ya mkutano uliopita.
  Alisema wabunge kuzomeana ama kutoka nje ya mkutano wa Bunge kwa kutoridhishwa na jambo fulani ni hali ya kawaida kwa kuwa wabunge hao hao wanaotoka nje baadaye hurudi bungeni na kuendelea na shughuli nyingine.
  Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walitoka nje ya ukumbi wa Bunge katika Mkutano wa Kwanza kususia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete ya kufungua Bunge la Kumi Novemba 18, 2010.
  Wange hao walitoka tena nje ya ukumbi wa Bunge Februari 8, mwaka huu kupinga kupitishwa kwa marekebisho ya kanuni za Bunge ambazo tafsiri ya neno “Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni” ilitolewa.
  “Mbunge au wabunge kutoka nje ya ukumbi sio issue (suala) hata kidogo, jambo muhimu ni uamuzi wa Spika kuhusu jambo linlobishaniwa, mabunge mengine mambo yanayotokea mle yanatisha, tuliwahi kwenda Bunge la India tukashangaa kila mbunge anasimama anataka kuzungumza,” alisema Makinda na kuongeza:
  “Kwa hiyo Bunge letu bado ni la kistaarabu kabisa, watu wasione ajabu yanayotokea mle.”
  Kuhusu ushauri uliotolewa na mmoja wa waandishi wa habari kuwa afute kauli yake aliyoitoa bungeni kuwa wabunge wasome magazeti kama barua zingine za wasomaji, Makinda alisema hawezi kufuta kauli yake kwa kuwa alikuwa sahihi.
  Alisema mwandishi aloiyeandika makala ya kumkosoa yeye na Bunge zima kuhusu utaratibu wa kutafsiri kambi rasmi ya upinzani alimkasirisha sana kwa kuwa hakujua ambacho alikuwa akikiandika.
  “Sitaomba radhi na ambaye hataki kukubaliana na maoni yangu shauri yake, niliwaambia wabunge wasome magazeti kujifurahisha tu kwani baadhi ya mambo yanayoandikwa hayana ukweli wowote, mfano sisi tulichofanya ni kutafsiri kanuni kuhusu kambi rasmi ya upinzani bungeni, lakini yaliyoandikwa ni tofauti kwa kweli yale yalinikera sana mimi,” alisema.
  Kuhusu kumnyima Mbunge wa Arusha Mjini, Chadema, Godbless Lema, kutoa ushahidi bungeni wa kauli yake kuwa Waziri Mkuu alilidanganya Bunge, Makinda alisema muda ulikuwa hautoshi.
  Alisema baada ya Lema kumpelekea ushahidi wake kwa maandishi, alipeleka vielelezo hivyo kwa wataalamu na wanasheria wake ili wavifanyie kazi, lakini mpaka mkutano wa Bunge unamalizika hakukuwa na muda wa kujadili suala hilo.
  source: NIPASHE
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,318
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  Historia itakuandama milele na hata dini yako haiku support madudu unayoyafanya heri ungebakia back bencher kuliko kuwa agent wa mafisadi.....naumia sana moyo nchi haina mwenyewe!!!hata wewe!!!!!
   
 3. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mafisadi wanamtesa huyo bibi, hana lolote! She will never balance bunge even one day. Aende kwa babu loliondo ma hasira na jazba zipungue kwanza teh teh

  [​IMG]
  Spika wa Bunge, Anne Makinda  Spika wa Bunge, Anne Makinda, ametabiri kuwa mkutano ujao wa Bunge utakuwa moto kuliko uliopita na ameapa kwamba hatakipendelea Chama cha Mapinduzi (CCM) kwani akifanya hivyo anaweza kusababisha machafuko nchini na kusababisha nchi isitawalike.
  Aliyasema hayo jana mjini Bagamoyo wakati akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari baada ya kufungua semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na ofisi ya Bunge.
  Kuhusu swali kwamba anaonekana kupendelea CCM, Makinda alisema hawezi kufanya hivyo kwa kuwa jambo hilo ni la hatari na wananchi hawatakubaliana nalo kwa kuwa hali hiyo inaweza kusababisha ghasia na nchi kutotawalika.
  “Kwa dini yangu mimi naapa kabisa sitapendelea chama chochote cha siasa, ukipendelea chama fulani wananchi wanaona, vyombo vya habari vinaona na unaweza kusababisha nchi isitawalike kabisa,” alisema Makinda.
  “Siwezi kukandamiza upinzani hata kidogo, hii nafasi ya Spika ni nafasi nyeti sana huwezi ukafanya mchezo huo maana amani itatoweka na kitakachofuata ni machafuko, na nimeapa sitapendelea kwa kuwa naogopa kuokota makopo barabarani,” alisema Makinda.
  “Mimi natambua mamlaka na majukumu niliyopewa kikatiba, katika kuliongoza Bunge hivyo siwezi kujiingiza katika ushabiki na maamuzi ya aina yoyote ya upendeleo kwa sababu najua kwa kufanya hivyo naweza kuiingiza nchi katika machafuko makubwa,” alisema.
  Akizungumzia malumbano ya wabunge, alisema hayo ni mambo ya kawaida katika mabunge yote duniani na wengine katika nchi mbalimbali wamekuwa wakifikia hatua ya hata kupigana.
  Alisema wananchi hawana sababu ya kushangaa mijadala mikali iliyotokea kwenye Mkutano wa Pili uliopita kwa kuwa siku zijazo inaweza ikatokea mijadala mikali zaidi ya mkutano uliopita.
  Alisema wabunge kuzomeana ama kutoka nje ya mkutano wa Bunge kwa kutoridhishwa na jambo fulani ni hali ya kawaida kwa kuwa wabunge hao hao wanaotoka nje baadaye hurudi bungeni na kuendelea na shughuli nyingine.
  Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walitoka nje ya ukumbi wa Bunge katika Mkutano wa Kwanza kususia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete ya kufungua Bunge la Kumi Novemba 18, 2010.
  Wange hao walitoka tena nje ya ukumbi wa Bunge Februari 8, mwaka huu kupinga kupitishwa kwa marekebisho ya kanuni za Bunge ambazo tafsiri ya neno “Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni” ilitolewa.
  “Mbunge au wabunge kutoka nje ya ukumbi sio issue (suala) hata kidogo, jambo muhimu ni uamuzi wa Spika kuhusu jambo linlobishaniwa, mabunge mengine mambo yanayotokea mle yanatisha, tuliwahi kwenda Bunge la India tukashangaa kila mbunge anasimama anataka kuzungumza,” alisema Makinda na kuongeza:
  “Kwa hiyo Bunge letu bado ni la kistaarabu kabisa, watu wasione ajabu yanayotokea mle.”
  Kuhusu ushauri uliotolewa na mmoja wa waandishi wa habari kuwa afute kauli yake aliyoitoa bungeni kuwa wabunge wasome magazeti kama barua zingine za wasomaji, Makinda alisema hawezi kufuta kauli yake kwa kuwa alikuwa sahihi.
  Alisema mwandishi aloiyeandika makala ya kumkosoa yeye na Bunge zima kuhusu utaratibu wa kutafsiri kambi rasmi ya upinzani alimkasirisha sana kwa kuwa hakujua ambacho alikuwa akikiandika.
  “Sitaomba radhi na ambaye hataki kukubaliana na maoni yangu shauri yake, niliwaambia wabunge wasome magazeti kujifurahisha tu kwani baadhi ya mambo yanayoandikwa hayana ukweli wowote, mfano sisi tulichofanya ni kutafsiri kanuni kuhusu kambi rasmi ya upinzani bungeni, lakini yaliyoandikwa ni tofauti kwa kweli yale yalinikera sana mimi,” alisema.
  Kuhusu kumnyima Mbunge wa Arusha Mjini, Chadema, Godbless Lema, kutoa ushahidi bungeni wa kauli yake kuwa Waziri Mkuu alilidanganya Bunge, Makinda alisema muda ulikuwa hautoshi.
  Alisema baada ya Lema kumpelekea ushahidi wake kwa maandishi, alipeleka vielelezo hivyo kwa wataalamu na wanasheria wake ili wavifanyie kazi, lakini mpaka mkutano wa Bunge unamalizika hakukuwa na muda wa kujadili suala hilo.
  source: NIPASHE[/QUOTE]
   
 4. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  wapo watu wakizungumza unawaamini wao na unaamini wanachokisema, bahati mbaya sana mama Makinda si mmoja wa hao watu.
   
 5. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  hivi ni nani yule Msajili wa vyama,alisema ana mpango wa kuifuta CHADEMA???na ameshawaandikia barua kali kuwaonya???nikumbusheni hapa!!!!
   
 6. A

  August JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  naona maandamano ya cdm na mahakma za kimataifa zinamtia uoga,
   
 7. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kashaga ni wewe ndio ulioleta posti hii?
  Siamini, umeanza kuja kuja karibu sana
   
 8. n

  niweze JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  This is good topic here. Kweli wanaohataraisha amani Tanzania ndio hao walio kweye rosta ya Rostam Aziz. Huyu mama sijui kama ni elimu au ni jinsi alivyo lelewa kwa kupendelewa pendelewa miaka mingi katika nafasi nyingi za serikali, she feels like she needs to give back kwa mafisadi na ccm. Wananchi tunachokifahamu leo hii ni kwamba mbinu za kulifanya Bunge kama tawi jingine la ccm litaishia hapa. Makinda ukae ukijua misaada unayotoa kwa ccm na Kikwete kipindi hiki vitakutokea puani na damu itakutoka, sijui kama ulishapigwa kipepsi ukaona uchungu wa maamuvi ya senses za pua. Elimu yako ni ndogo sana na upeo wako wa maswala ya sheria na taratibu za kujenga demokrasia kupitia "Bunge la Wananchi" unaonekana wazi. Kama unajiona huna upeo na kujua kazi yako vizuri, uende ukaingie mabunge ya Marekani au Uk, ukaangalie jinsi gani viongozi wa Bunge wanavyoongoza Mabunge kwa manufaa ya Mataifa yao. Let me give an example, Nancy Pelosi (first female to lead House of Representative in United States. Listen to small clips when she was at work,

  This woman is tough and resilient to help the people not only her party. Makinda stop look for models in fail states in Africa or from Rostam Aziz. ​
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Apendelee ccm marangapi? Chadema wanabanwa kuwasilisha hoja zao kila siku.
   
 10. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mama yuko sawa
   
 11. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #11
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Mh Spika usitake kutuaminisha kuwa wewe ni mtu safi wakati umenunuliwa na mafisadi
  huu unafiki unaotuletea hautakusaidia
  ni aibu kwa mama kama ww kumaliza siasa vibaya hivi.
  spika sita nakukumbuka sana
   
 12. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  ZE HONARABo huyu simwanini sana.

  naona kauli na matendo haviendani hata kidogo
   
 13. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Dadavua yupo sawa ki vipi? Acha ushabiki wa kitoto
   
 14. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mama sisi yetu macho na masikio. Kikao cha pili tumeona umechemsha, kama umejifunza kitu badirika, nafasi ya kujisahisha unayo. ukiamua kuokota makopo wewe tu! Mungu akusaidie ubadirike mama, nchi zi mali ya ccm, ni yetu sote. April katende haki.
   
 15. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hana la kujifunza. Hakuna matumaini yoyote kwa kwa hili jimama kuendesha bunge kama bunge. Kawekwa hapo si kwa kubahatisha, na so far na-perfom excellent kwa kazi aliyotumwa. Haki ni msamiati ambao kwenye dictionary ya mafisadi haijingizwa. Na ndiyo kamusi aliyopewa Makinda.
  Asichojua ni kuwa kuna countdown siku za mafisadi. Lakini kama vile ana machale bcoz anaota kuokota makopo.
   
 16. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,655
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Mbuzi ni mbuzi tu hawezi kuwa simba, Makinda ni fisadi tu na atabaki kuwa fisadi hadi mwisho wa dunia.
   
Loading...