Makinda na CCM wanatengeneza bomu lenye uzito mkubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makinda na CCM wanatengeneza bomu lenye uzito mkubwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jibaba Bonge, Feb 11, 2011.

 1. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Katika kikao hiki kinachoendelea tunashuhudia mambo mengi ambayo hatukuyatarajia yatokee. Nashawishika kusema kwamba, kwa kujua ama kwa kutokujua, Makinda kama spika na CCM ambacho ni chama tawala kwa sasa , wanatengeneza bomu lenye uzito mkubwa ambalo litakapolipuka madhara yake yatakuwa makubwa sana kwa nchi yetu.


  Inavyoelekea spika Makinda ameamua ama anatii maelekezo ya wakubwa zake kulipelekesha bunge kwa manufaa ya ccm na kuliondoa katika mstari wa kuwa chombo huru kwa ajili ya kuisimamia serikali kwa manufaa ya wananchi. Hata kipofu anaona na hata kiziwa anasikia kwa jinsi maamuzi yanayofanywa chini ya Makinda yasivyokuwa na manufaa kwa taifa bali kwa ccm ili tu kuwakomoa Chadema! Kama ndani ya siku hizi chache bunge limekuwa hivyo sijui kwa miaka mitano litakuwaje!


  Pamoja na kuwa wabunge wa ccm, kama si wote basi wengi wao, wanafurahia maamuzi wanayoyachukua sasa kutokana na kuwa wao ni wengi hivyo wana nguvu ya kura, wanatakiwa kupima ‘impact’ ya maamuzi yao kwa wananchi waliowapeleka bungeni. Wakidhani wapiga kura wao wanafurahia maamuzi waliyoyafanya toka wameanza kikao hiki cha bunge, watakuwa wanajidanganya sana. Nimejaribu kufuatilia mazungumzo ya watu raia wa kawaida nikagundua kinachojengwa mioyoni mwao ni kuongezeka kwa uchungu na hasira juu ya maamuzi yaliyokwisha kufanywa.


  Hili ni bomu, tena kubwa la uzito wa juu. Uchungu na hasira vikisambaa kwa wananchi wengi na vikifikia ukomo wa kuvumilika hapo ndiyo inakuwa ‘enough is enough, come what may’. Mlipuko utakaotokea baada ya hapo kuutuliza ni vigumu sana. Ni hapo ambapo wananchi huwa tayari kufa kwa kuupinga utawala uliopo kutokana na maamuzi yaliyofanywa ambayo hayakuwa na manufaa kwa kwao.  Makinda asipoangalia anaweza akawa muasisi wa utengenezaji wa bomu hili. Ukichunguza bungeni kwa sasa, wabunge wa ccm wana furaha sana, wamewaweza wale wa chadema. Kwa bahati mbaya hiyo furaha ya wabunge wa ccm haipo kwa wananchi walio wengi. Hii ni hatari.  MAKINDA TAFADHALI RUDISHA BUNGE MAHALI PAKE USIJE UKALIINGIZA TAIFA KWENYE MACHAFUKO.
  USITUFANYE TUAMINI KUWA WANAWAKE HAWANA UWEZO WA KUONGOZA MABUNGE KWA UFANISI.
  KATAA KUWA MWANAMKE WA KWANZA KUTUMIKA KUANZISHA MACHAFUKO TANZANIA.
  MUOGOPE MUNGU KATIKA KILA MAAMUZI UNAYOYASIMAMIA
   
 2. BULLDOZZER

  BULLDOZZER Senior Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu you better be specific. Hasa kwa maamuzi yepi yanayohatarisha amani??
   
 3. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kumbe nawe umelione hili eeh!!!..... nilifikira ni mm pekeyangu nimeliona hilo but akumbuke kila chenyemwanzo kina mwisho wake
   
 4. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  huyo mama yupo kwenye payroll ya mafisadi na hiyo ndio kazi waliomtuma kuifanya na wala msitarajie zuri toka kwake, kwani mzee sitta alikua na kosa gani mpaka akina mkwere wakaamua kumpiga chini? watanganyika lazima tutafakari na tuchukue hatua mapema sana, hawa watu hawana nia njema na nchi yetu, tuandamane kumpinga huyo mama na ikiwezekana tuishinikize serikali na bunge ili mtu huyo ajiuzuru, kiukweli mama huyoni mtu wa kupanic panic na wala hana busara kama za mzee Sitta
   
 5. Tambara Bovu

  Tambara Bovu JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 19, 2007
  Messages: 586
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hizi tabia za kupeana majukumu kwa watu wasio na uwezo ndo sababu ya kutumika kizembe bila hata kutumia akili ya kuzaliwa.huyu mama anatuchafua wanawake,na kiti chake maalum cha uspika ambacho hajakitolea jasho.nami najua wanatengeneza bomu na nasubiri kwa hamu lilipuke kwani wananchi tumeshachoka
   
 6. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Huyu mama silisikia humu JF kuwa ni msagaji?:twitch:
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kuuumbe!!!!!
   
 8. THE GAME

  THE GAME JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2011
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  huyu mama ni fisadi toka hata ajachaguliwa na akionekana mapema vipindi vya nyuma enzi za Sita hafai ana uccm zaid,kilichobakia sisi wananchi tunaoteseka na kuburuzwa tuseme basi imetosha tuwaondoe madarakani turudishe amani na haki yetu iliyoporwa na mafisadi.
   
 9. S

  SUWI JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Maamuzi mengine kama spika yanahitaji busara kama alivyokuwa anafanya Samwel Sita.. Makinda yeye hana mda wa kutumia busara kila kitu kanuni.... huku akiwa amepaniki na kuonyesha hasira.. In short hafai kushika nafasi nyeti na muhimu kama ya uspika kwani atatupeleka kusiko..

  Makinda HAFAI KUWA SPIKA JAMANI ATOKE. Tunataka kuona bunge linalojadili mambo yenye tija kwa manufaa ya taifa sio kukomoana na kulipa visasi...... Mnachokifanya CCM hakitasaidia kurudisha imani ya wananchi kwenu bali kinazidisha chuki kubwa ambayo matokeo yake mtayaona siku si nyingi....
   
 10. MANI

  MANI Platinum Member

  #10
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,413
  Likes Received: 1,872
  Trophy Points: 280
  Uzuri ni kuwa matendo yote tunayaona kwenye tv na hivi watanzania tunaweza kuwa hatuwezi kuchagua kizuri kutokana na kibaya kwenye haya yanayotokea?
   
 11. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  What did you guys really expected from anna?
   
 12. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Bunge halitaweza kwenda mbali zaidi ya uwezo wa spika aliyepo kwenye kiti. Kumbuka wakati wa msekwa Hali ilikuwa mbaya kwenye mijadala! Akaja Sita, uwezo wake ulivyokuwa mkubwa kujua mambo bunge nalo likawa na uwezo mkubwa wa kujadili mambo! Kinyume na hapo itabidi watwangane ngumi ili waweze kwenda mbali zaidi katika majadiliano
   
 13. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Niliwahi kuandika humu JF kuwa Sitta wakati akiwa spika alitumia akili na busara sana kwa kuruhusu richmond kujadiliwa bungeni. CCM walimlaumu bila kujua kuwa aliwasaidia sana.
  Wakati ule habari za richmond zilivuma na ikawa hazieleweki. Shelukindo akasema tumeshindwa kuwapta baadhi ya watu ili tuwahoji kwenye kamati yetu. Wananchi wakawa hawaelewi kwanini baadhi ya watu wakaidi kufika mbele ya kamati ya bunge (nishati na madini), na wakati huo huo ikaeleweka kuwa richmond wamelipwa hela bila kutimiza kazi yao. Ikawa ni kama bomu fulani hivi ambalo haikujulikana litalipuka lini na wapi.
  Ile kamati ya mwakyembe iliporuhusiwa kutoa findings zake hadharani bungeni, lile bomu ikawa limeteguliwa kabla halijalipuka. Hakika wakati ule kama sitta angesema ayafunike hali ingekuwa mbaya;diyo maana watu wengi walifurahia yaliyotokea bungeni.

  Makinda na ccm wameshindwa kuuona ukweli huo, wakamuona sitta ni mbaya eti hakupaswa kuruhusu mjadala ule. Leo hii wanazuia mjadala ambayo ingekuwa na maslahi kwa taifa, wanatimiza matakwa ya ccm tu bila kujua huku nje ya bunge kukoje.
  Sioni makinda akijirekebisha haraka, hivyo bomu la sasa litalipuka tu. Si pinda, si makinda, si Jk ambaye yuko tayari kulitegua, wanalikwepa tua hatimae litalipuka.

  Kuna mtu aliwahi kuandika humu ndani juu ya maji kuwa siku zote huelekea bondeni; waweza kuyazuia kwa muda fulani, lakini inabidi uwe makini ili kabla hayavunja kingo, uyatengenezee njia unayotaka yapite, vinginevyo yakishabomoa yatakumba kila kitu njiani na maafa yatakuwa makubwa. Ugumu wa maisha kwa waTZ umekuwa wa kutisha, tumaini lao ni kuona bunge linawatetea na kuikaba serikali, kinachooneka sasa ni bunge kujenga uswahiba na serikali. Tumaini kwamba upinzani waliouchagua utaichunga serikali, umechakachuliwa kiasi kwamba seriakli yenyewe imejichagulia nani wa kuichunga. Maisha ni magumu, bei ya umeme juu, umeme wenyewe wa mgao hivyo uzalishaji unashuka, kipato hakuna lakini wabunge wanakaa siku tano kujadili hotuba ya rais ambayo hawawezi kupunguza wa kuongeza chochote, mamilioni yanakwenda ambayo mwananchi hanufaiki nayo!
  Hakika hili ni bomu, litakapolipuka litazidi la Tunisia na Misri.
   
 14. T

  Tanganyika Member

  #14
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makinda hatumii utashi wake kuendesha bunge bali ana-remotiwa!! Ndo maana anasimama upande wa ccm na serikali..........hili ni hatari na Matokeo yake nikuleta machafuko! Na wabunge waliyowengi wa ccm hawajui wanachokifanya bungeni kazi yao ni kupelekwa kama gari bovu. Wabunge wa CCM simamieni maslahi yataifa acheni kushabikia na kusimamia maslahi ya chama na kupuuza mambo muhimu ya kuleta faida kwa taifa........pia kuweni wepesi wa kukemea maovu ambayo serikali inafanya...........msipofanya hivyo kuna siku mtalipwa mnayoyafanya.
   
 15. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nadhani mchakato wa ANGUKO LA CCM na vibaraka wake akina Makinda na mafisadi wake umeshafikia mwisho. Ngoma ikilia saaana ujue inakaribia kupasuka.
   
 16. FiQ

  FiQ JF-Expert Member

  #16
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mwisho wao umefika, na maovu yao yatawarudia wenyewe
   
 17. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sita alikuwa anaelekea kuikomboa CCM, Kumbuka marehemu Kolimba alishasem CCM imepoteza dira, walipomkoroga Six wakaambulia 60% za nanihii. Sasa ndo kabisa, I can bet, with this new speaker, with this kind of push from CCM, I dont buy it that they will get even 30% kwa kuchakachua 2015. CCM Wake up, you are going to opposition.
   
 18. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #18
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,195
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  Naiona roho ya kuzimu inafanya kazi wazi wazi.
  Ndugu zangu walokole fungeni roho hiyo ilegeee na kuirudisha nguvu hiyo ya giza huko kuzimu iliko maskani yake semeni
  AMINA
  kwa ajili ya kutafuta huruma ya Mungu wetu kwa ajili ya wanaoonewa kwa jeuri pofu.

  Kuwaonea huruma kina mama waja wazito,wanaobeba watoto bila tumaini, waliodhulumiwa haki zao kwa jeuri ya kifisadi,wanaokufa kipindi hiki kwa maonevu yaliyo kithiri....ongeza kwenye maombi yako Mungu wetu ni moto ulao!
   
 19. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #19
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Who pays the piper determins the tune; hapana budi ikumbukwe kuna vigogo waliowekeza kwa kumwezesha mama huyo kukikwea kiti cha enzi. Itakuwa vigumu kwake kuwasaliti.
   
Loading...