Makinda kamtukana Jk na atamdhalilisha Pinda!!

Nilisha sema kitambo kwamba huyu mama anaudhalilisha jinsia yake na inafaa wenye jinsia hiyo wamkee maana ukiwaangalia kwenye uwanja wa uhuru ndio walio athirika zaidi !
 
Masahihisho kidogo Mzalendo. Ni Mama MAKINDA na siyo MAKIMBA kama ulivyoandika na kurudia mara kadhaa. Makimba kwa lugha ninayo ifahamu, japo sijui kama ni rasmi, yana maana isiyo nzuri sana.

TATA huyo sio kama hajui ni MKEREKETWA sana ndio maana akaona hilo jina liwe hivyo. Nikweli unavyosema hilo jina lina maana fulani yaani, MAV....... halafu makubwaaaa!!!! au sio Tata.
 
Ni kweli kuwa CCM haitaondolewa na chama chochote kingine cha kisiasa. Ila wananchi wakiamua kikuondoa hakutakuwa na wa kukinusuru. Kosa kubwa wanalofanya CCM ni kudhani kuwa adui wao mkubwa ni vyama vya upinzani. Kumbe adui mkubwa wa CCM ni CCM yenyewe.

Kwa Bara sio rahisi kuiondoa CCM madarakani kwani wengi wa watu huko ni waoga na wanafiki. nafikiri labda itawezekana baada ya miaka isiyopungua ishirini.

Na kwanza CCM itaanza kuondolea zanzibar ndio Bara muweze.

fuateni nyayo za CUF zanzibar na mikakati yao. Kwani huo ni mbuyu inahitajika hekma ya hali ya juu sana kuing'oa
 
Kwa Bara sio rahisi kuiondoa CCM madarakani kwani wengi wa watu huko ni waoga na wanafiki. nafikiri labda itawezekana baada ya miaka isiyopungua ishirini.

Na kwanza CCM itaanza kuondolea zanzibar ndio Bara muweze.

fuateni nyayo za CUF zanzibar na mikakati yao. Kwani huo ni mbuyu inahitajika hekma ya hali ya juu sana kuing'oa


Miaka ishirini?
 
Kwa Bara sio rahisi kuiondoa CCM madarakani kwani wengi wa watu huko ni waoga na wanafiki. nafikiri labda itawezekana baada ya miaka isiyopungua ishirini.

Na kwanza CCM itaanza kuondolea zanzibar ndio Bara muweze.

fuateni nyayo za CUF zanzibar na mikakati yao. Kwani huo ni mbuyu inahitajika hekma ya hali ya juu sana kuing'oa

Una maana ndoa ya mkeka? HAPANA, ungeniambia JINO KWA JINO ningekuelewa lakini kuwekwa kimada hapana.
 
hawa viongozi wa ccm wamekuwa watu wa kupishana kauli kila kukicha, nafikiri hawana ushirikiano kila mtu anasema anachotaka, alafu baadaye wanajikanusha. pinda yuko kivyake ANA yuko kivyke, kadhalika jk. tusubiri tuone anguko la chama siku si nyingi.
 
navyoona chamsingi ni kila mtu kuwajibika katika nafasi yake bila kujali maslai ya chama kwakua utakuwa na support nzuri toka nguvu ya umma na wapenda maendeleo wote. natumai kunasiku hawa watu sisiem) wataulizwa kama wanachokifanya ni sahihi nakama nihaki kwa watu waliopewa dhamana ya kuwaongoza.
 
Huyu mama makinda amewekwa pale na mafisadi ili kulinda maslahi ya mafisadi na chama chake,ndiyo maana utamuona ni mtu mwenye jazba wakati wote hata kabla ya kusikia nini mbunge wa upinzani anataka kukisema,na huwa hana hata chembe ya busara kwenye maamuzi yake.kama asipo angaalia basi mwisho wa sisiem na serikali yake ya kifisadi umekaribia kwa saaana tuu!!!.wee mwacheni tu aendelee kuwatetea na kuwakumbatia hao mafisadi.
 
Anna Makinda amefanikiwa kupata uspika kwa juhudi za Rostam, hivyo anapata maelekezo toka kwa Rostam.
Na Rostam hawapi 'watu' wake nafasi, anawaburuza, si mnaona ya Mkulu? Ndio maana lazima achemshe.

Ila Makinda anadhalilisha;
1.. kiti cha uspika,
2.. serikali (kwa kuwaziua mawaziri wasijibu ili wasichemshe),
3.. waziri mkuu (kumzuia Lema asitoe ushahidi Bungeni, akidhani anamuokoa waziri mkuu Pinda),
4.. wanawake kwa ujumla (kwa yeye kukosa uwezo wa kuongoza Bunge)
 
Nakushangaa sana hivi CDM na ww ukiwa ni kibaraka wao mna jipya ?
Du kweli jamaa yangu umesema, leo wabunge wamepewa 90m/= za ma VX/GX/V8 sisi tunagombana humu jukwaani na njaa zetu na matusi kibao.
2015 haipo mbali tutachuja pumba na makapi kupata unga kelele ya nini?
 
nje ya mada?

SIMTAMBUI JK KAMA NI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
A%20S%20103.gif
 
CCM itaondolewa madarakani na kizazi kipya, hata watumie hila na nguvu kiasi gani, muda wao ulishapita, wakajisahau kukirithisha kizazi. Obama kule Marekani aliwekwa na kizazi kipya ambacho hakina habari na mambo ya utumwa wala uhafidhina wa wazazi wao, waliweka matumaini yao kwa kijana wa Kijaluo wakafanya uamuzi.

Yaliyotokea Tunisia na Misri na yanayoendelea kwenye mataifa hayo ya Kiarabu ni suala la kizazi kipya kuchukua nafasi yake kwa nguvu baada ya kuona wazee ni ving'ang'anizi, hawabadiliki na waliokubuhu kw aufisadi huku wao wakiendelea kuteseka pasipo sababu.

Mazingira ya kizazi kutumia nguvu yako wazi Tanzania, wazee (CCM) ni ving'ang'anizi, hawabadiliki na mafisadi waliokubuhu, vijana wametelekezwa pasipo sababu ya msingi, nguvu ya umma ni lazima. Kisha tujiulize ni ipi hiyo nguvu ya umma iliyopo, jibu ni kizazi kipya.
 
.......Kwa dalili ninazoziona mimi nahisi CCM inaweza kudhalilika sana kipindi hiki kupitia spika Makinda

Nimenukuu mstari huo hapo juu, Mimi nasema CCM haijaanza leo kudhalilika na kila siku inadhalilika, ila naona wametengeneza mazingira ya kudhalilisha UWEZO wa MWANAMKE zaidi kipindi hiki kwa kumpa huyo mama uspika.




Ndugu zangu naona mnaanza kuzisahau siasa za CCM. Naomba niwakumbushe mambo haya:-
1. CCM wana tabia ya kupindisha upepo ili wafunike scandal [Mfano ni scandal ya RICHMOND na jinsi ilivyofunikwa kwa kutumia BOT; EPA na KIWIRA - RICHMOND ni fedheha kubwa kuliko hizo tatu]
2. CCM walimtumia chenge kuhamisha upepo ili wamuondoe 6 kwenye kiti cha enzi. [CHenge asingeyasema yale aliyoyasema 6 angewasumbua kumuondoa]
3. Makinda anachofanya ni kutuchanganya ili kumpa nafasi EL apenyeze siasa zenye malengo ya Urais.
WAKATI MWINGINE WANASIASA HUTUMIA LUGHA ZA KUVUTA SHUTMA UPANDE WAO ILI WANAYEMTAKA APITE. Hivi sasa attention zote zimeelekezwa kwa Makinda na siyo utendaji wa JK na serikali yake!! just wtach it closely.
 
Back
Top Bottom