Makinda hakufaa kuwa Spika wa Bunge la Tanzania, hazielewi Hansard

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,545
1,250
Mwanzo wa Anna Makinda katika nafasi ya Uspika unaonyesha kuwa hakufaa kuwa Spika. Kama hawezi kusoma na kuzielewa kumbukumbu sahihi za bunge ni sababu tosha ya kumfanya asifae kuwa Spika wa bunge la Tanzania. Kwa kusema kwake kuwa hajui maana ya neno fisadi zaidi ya mwizi wa mme wa mtu inaonekana ama hazisomi Hansard au akisoma haelewi, na hivyo hafai kuwa Spika. Neno fisadi linaeleweka vizuri katika siasa za Tanzania kuwa ni mwizi mkubwa wa mali za umma, mali za wananchi wa Tanzania. Zaidi ya kufahamika vizuri miongoni mwa raia wa kawaida wa Tanzania neno fisadi limetumika mara nyingi katika kumbukumbu sahihi za bunge yaani Hansard likiwa na maana hiyohiyo ya wizi mkubwa wa mali za umma. Makinda anaposema fisadi ni mwizi wa mke wa mtu ina maana viongozi wa serikali ya CCM wanatumia ofisi za serikali kuiba wake za watu?

Neno ufisadi linametumika mara sita katika Hansard ya tarehe 15.02.2008. Lipo kurasa za 53 (mara mbili), 54 (mara mbili), 47 (mara moja), 59 (mara moja). Vilevile neno ufisadi limetumika katika Hansard ya tarehe 31.01.2008 katika ukurasa wa 74. Zaidi ya hapo neno ufisadi limetumika katika Hansard ya tarehe 28-29/11/2007 na linaonekana ukurasa wa 84. Anna Makinda akasome kurusa hapa chini. Zaidi ya kutumika katika siasa za Tanzania neno ufisadi na mafisadi limetumika pia katika nchi za Afrika Mashariki hususani Kenya likiwa na maana hiyohiyo ya wizi wa mali za umma. Kwa kumkumbusha linaambatanisha pia video inayoelezea mapambano ya ufisadi wa wizi wa mali za umma nchini Kenya. Tena Mwai Kibaki anasema wezi wa mali za umma hawafai kuishi. Sasa inakuwaje leo Spika wa bunge la wananchi wa Tanzania aseme kuwa hajui ufisadi ni nini? Kwa kauli yake hiyo hakufaa kuongoza chombo cha wananchi wa Tanzania. Bunge siyo chombo cha mafisadi ni chombo cha wananchi.

1. http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/HS-10-11-2008.pdf, 15.02.2008
2. http://www.parliament.go.tz/POLIS/PAMS/Docs/HS-10-3-2008.pdf, 31.01.2008
3. http://www.parliament.go.tz/bunge/docs/richmond final.pdf


YouTube - Kibaki Apinga Ufisadi
 

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,536
2,000
Unless kama alikuwa anatania bse huyu kwenye mbio za mwenge Njombe aliwai toa tamko kuwa hakuna haja ya kuwasafisha mafisadi sasa alimaanisha wanaotembea na waume za watu?
 

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,545
1,250
Unless kama alikuwa anatania bse huyu kwenye mbio za mwenge Njombe aliwai toa tamko kuwa hakuna haja ya kuwasafisha mafisadi sasa alimaanisha wanaotembea na waume za watu?

Kinachoshangaza kama hasomi Hansard, au kama anasoma hazielewi kwa nini amekubali kuwa Spika? Kwanza alikuwa naibu wa Spika miaka mitano bado hajui kilichoandikwa kwenye Hansard, hakufaa kuwa Spika. Kwa hiyo bunge linaweka kumbukumbu sahihi za Hansard kuelezea wanaume viongozi wa Serikali ya CCM waliotumia ofisi za serikali kuiba wake za watu?
 

Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,817
0
Atigi

mie kiswahili tu kimenitatiza. 'Hakufaa' kwani wadhifa wake wa uspika ushaisha?
 

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,545
1,250
Atigi

mie kiswahili tu kimenitatiza. 'Hakufaa' kwani wadhifa wake wa uspika ushaisha?

Gaijin, unapendekeza niandike Makinda hafai? nilifikiria hivyo, ila sasa alimeshakuwa Spika tayari ndio maana nikasema hakufaa.
 

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,545
1,250
Hakufaa kuchaguliwa kuwa spika au hafai kuwa spika ..........:)

Kutokana na matamshi yake kuwa fisadi anayemjue yeye ni mwizi wa mke wa mtu wakati neno hilo limetumika bungeni na lipo kwenye Hansard ambazo yeye kama naibu Spika wakati ule alitakiwa kuwa anazisoma na kuzielewa basi unaweza kusema Hafai kuwa Spika. Nilifikiria kutumia hilo neno hafai, ila sasa ameshakuwa Spika, so nikasema hakufaa, implying hakufaa kuchaguliwa kuwa Spika. Ila naweza kuweka sahihisho lako ikiwa unaona neno hafai ni zuri zaidi badala ya hakufaa. Je unapenda nifanye hayo masahihisho?
 

Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,817
0
Atigi kaka nimekuelewa

hakuna lazima ya kubadilisha, ujumbe kwa wengi nafikiri unafika japokuwa mvuto kwa wapenda usahihi unapungua.

Anne Makinda hakufaa kuwa Naibu Spika na sasa hafai kuwa Spika :)
 

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,545
1,250
Atigi kaka nimekuelewa

hakuna lazima ya kubadilisha, ujumbe kwa wengi nafikiri unafika japokuwa mvuto kwa wapenda usahihi unapungua.

Anne Makinda hakufaa kuwa Naibu Spika na sasa hafai kuwa Spika :)

Mvuto ni muhimu pia, ngoja nifanye the needful
 

LoyalTzCitizen

JF-Expert Member
Sep 15, 2010
2,178
2,000
Inabidi tubadirishe katiba na itetee kwamba Spika lazima awe ameoa au ameolewa! ili kupata strong and dedicated candidates without any possible phobia or bias against opposite sex! kuna strong suggestion kwamba watu single huwa wanastruggle (psychologically) katika position nyeti kama yake yeye Muheshimiwa spika
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom