Makinda azungumza na waandishi; afafanua jina lake, akataa kuomba radhi

Hi ni moja ya tabia za kinadada kubadilisha majina yao yaonekane ya kizungu.,kwa mfano christina anataka aitwe tina...akaona aitoshi akamua ajiite tyna....ni usistaduu tu....bad to happen kwa spika wetu..
 
Hivi watanzania wana shida na jina lake au wanataka kuona anachangia kuboresha maendeleo ya nchi yetu kwa kupunguza mizengwe pale mjengoni? jina lake linatuhusu nini sisi? kwani tunatoa passport?
 
Nchi itaendelea kudumaa kwa miaka mingi sana, kwa viongoz wa aina ya Makinda, jeikei(msanii), Pinda, Taison na ndg zake kina Chiligat.
 
Tunasubiri kwa hamu mwongozo wake kuhusu utaratibu inapotokea mtu mzito kama waziri mkuu kulidanganya bunge!
 
Duh, jina lake linatusaidia nini tena huyu mama kweli hatuna Spika. TZ kazi kweli kupata development.
 
a.jpg


Spika wa Bunge la Tanzania ametoa ufafanuzi kuhusiana na jina lake. Anasema jina lake ni Anne Makinda na wala sio Anna Makinda. Zaidi ya matamshi, kuna tofauti yoyote kati ya majina Anne, Ann, Anna na Hannah?
Jina ni uamuzi wa mtu na kama Spika anataka aitwe kwa jina fulani na aitwe hivyo asitukanwe kwa kutumia haki yake!
 
Duh, jina lake linatusaidia nini tena huyu mama kweli hatuna Spika. TZ kazi kweli kupata development.
Hata JF hatuna watu. Tunakosa nini kwa yeye kutujuvya aitwe vipi? Si hasha hilo lilikuwa swali aliloulizwa na mwandishi.

Tunarukia jina lakini tunashindwa kumuuliza mtoa mada anaetuuzia kichwa cha mbuzi badala ya mbuzi mwenyewe. Hiyo mada inazungumzia;
1. Mahojiano na waandishi
2. afafanua jina lake, ilikuwaje?
3. Akataa kuomba radhi , kwanini na juu ya nini?
Tunaruka tu na kumtusi mama wa watu!
 
TOFAUTI NI NINI SASA?
nILIFIKIRI ANATAKA KUBADILI KUTOKA MAKINDA LIWE WATOTO WA NDEGE?
Hata mimi nashangaa!Wakubwa wetu upuuzi, sisi wenyewe upuuzi tutafika wapi? Kama anaona jina ni issue na iwe hivyo kwake isiwe kwetu kiasi cha kutoleana kashfa.
 
hehehe kama kawaida yetu,wana jf anapotokea mwana ccm anajadiliwa basi hiyo mada hata kama haina kichwa wala miguu tutaivalia njuga,mbona kunamambo mengi mema ya kutuletea maendeleo hatuyavalii njugaaaaaa?
 
Too much Seminars in this poor country! Seminar in Bagamoyo!! then!!? can't we employ "Askali wa Mianvuli" who can master the battle field immediately and focus forward without directive seminars? unless its for the substitutive income generating means to complement basic needs and social gathering with madame Anna or as she like Anne.
 
Waandishi wambana Spika Makinda Send to a friend Saturday, 12 March 2011 09:57 digg

Mwandishi Wetu, Bagamoyo
KAULI ya Spika kutaka wabunge wasome magazeti kama barua, imemtia matatani baada ya waandishi wa habari jana kumtaka awaombe radhi kwanza, ili watekeleze ombi lake la kuvitaka vyombo vya habari, viwe kiungo kati ya Bunge na wananchi.
Hata hivyo Spika Anne Makinda, aligoma kuomba radhi na kwamba alitoa kauli hiyo katika mazingira ambayo, hakuamini kama vyombo vya habari vingeweza kutoa taarifa aliyodai kuwa haikumtendea haki.
Katika mkutano wa pili wa Bunge la Kumi mjini Dodoma, Makinda aliishambulia makala iliyoandikwa na gazeti hili kuhusu mabadiliko ya kanuni za Bunge, zilizogusa kambi ya upinzani bungeni ambayo wabunge waliitumia kama marejeo, akisema "magazeti yasomwe kama barua".

Lakini jana akifungua semina ya siku mbili ya waandishi wa habari za Bunge, makinda alibanwa na waandishi wakimtaka aombe radhi muda mfupi baada ya spika huyo kueleza kuwa vyombo vya habari, ni nguzo muhimu na kiungo kati ya Bunge na wananchi.
"Mheshimiwa spika leo umetaka vyombo vya habari viwe kiungo kati ya Bunge na wananchi, lakini katika Bunge lililopita uliwataka wabunge wasome magazeti kama barua ukimaanisha hayana umuhimu, unaweza kufuta kwanza kauli hiyo au kuomba radhi kabla hatujatekeleza ombi lako,," alihoji mmoja wa washiriki wa semina hiyo.


Akionekana kutaharuki Spika Makinda alijibu,"nilijua ntakumbana na swali hili na nimejiandaa vema, sio kuomba radhi bali kutoa ufafanuzi."Nilifedheheshwa na habari ile, waliandika kinyume na ilivyo, walisema mimi ninakandamiza upinzani. Hapana mimi natakiwa kutoegemea upande wowote kwani nikitenda yaliyoandikwa naweza kuvuruga amani ya nchi. Spika peke yake anaweza kuvuruga amani ya nchi," alisema

Spika Makinda alifafanua kuwa kilichofanyika haikuwa kubadili kanuni za Bunge bali kutafsiri.

"Tulitafsiri kanuni ya 14(2) ambayo inasema kambi rasmi ya upinzani inaundwa na wabunge wote wa upinzani. Zamani ilikuwa kambi rasmi ya upinzani inatengenezwa na asilimia 30 ya wabunge, lakini hili halijawahi kutekelezeka kwa kuwa mwaka 1995 wabunge wa upinzani walikuwa 46 ambao ni chini ya asilimia 30 na mwaka 2000 hawakufikia hata asilimia 2. Bunge likalazimika kubadilisha kanuni na kuwa asilimia 12.5 ya wapinzani inaweza kuunda upinzani," alifafanua.

Lakini akitoa mada katika semina hiyo mwandishi nguli wa habari, Jenerali Ulimwengu, alisema kuwa kauli ya Spika kutaka wabunge wasome magazeti kama barua ni makosa."...Kwa maoni yangu Spika Makinda aliposema wabunge wasome magazeti kama barua alikosea," alisema Ulimwengu.Katika semina hiyo Spika Makinda alisema kuwa kanuni za Bunge zitafanyiwa mabadiliko makubwa katika kipindi hiki cha bunge la kumi.

"Tunaenda kufanya mabadiliko makubwa ya kanuni, na hivyo kambi rasmi ya upinzani haitakuwa tena issue ya kuumiza kichwa..," alisema Makinda.Alisema pia kwamba katika Bunge lijalo Sheria ya Vyombo vya Habari inatarajiwa kufikishwa bungeni tayari kujadiliwa na kwamba wadau watapata nafasi ya kushiriki katika mijadala yake.
Kuhusu Katiba, Makinda alisema mchakato huo ni muhimu na kwamba vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kuwaelimisha na kuwapa taarifa wananchi kuhusu mabadiliko hayo ili nao washiriki katika uandikaji katiba hiyo
 
Hata afanyeje yeye atabaki kuwa Anna tu hata kama ataenda mahakamani hatubadilishi ng'ooooo!!! Tangu lini kwenye Kiswahili tukatamka Anne? Mama Aibuuuuuuuuuuuu!!!!!!!! Asubiri pale atakapokuwa anaongea na Wathungu ndo wamwite Anne kwetu ni Anna (AnaMakinda!!!)
 
a.jpg


Spika wa Bunge la Tanzania ametoa ufafanuzi kuhusiana na jina lake. Anasema jina lake ni Anne Makinda na wala sio Anna Makinda. Zaidi ya matamshi, kuna tofauti yoyote kati ya majina Anne, Ann, Anna na Hannah?

Really its doesn't matter because she is now one of the criminals in Tanzania. Anyone who's working for Rostam and defend interests of corruptions and stealing from its people is referred to as Makindas.
 
nakumbuka miaka ya 80 pale mzee John Malecela alipojiita Abdallah Menlicela eti kisa apate kiduchu toka kwa mfalme wa UAE bila aibu akaumbuka mbele Mwalm Nyerere. Nahs kuna diri hicho kbb kmepata huko ughaibuni. Kama vp na ww Anna Semamba Makinda andika hv...!
ANNA WEMBAMBA M-K*ND*. Labda litakupendeza na uzd kuwatetea mafsad hapo mjengoni.!!
 
Back
Top Bottom