Makinda azungumza na waandishi; afafanua jina lake, akataa kuomba radhi

HayaNHUUUUUUUUUUUUU cha msingi atoe uhuru sawa kwa wabunge na kulifanya liwe la democrasia.. hata aitwe Husein...
 
Yaleyale ya kikwete kusema picha yake haijatoka vizuri na kulazimika kupiga picha nyingine rasmi . Ni upuuzi kupoteza muda kwa mambo yasiyo na tija.
 
Hapo zero tu,jina lake linamsaada gani kwetu?Hata kama angeitwa anne kwa mkazo wa juu na kuandikwa kwa fontsize ya 360 Kwa matendo yake huyu mama zero tu.Pia hata vyombo vya habari kuumpa muda huo ni ukosefu wa kazi.Tangazeni ya muhimu acheni mdondo huo.
 
Kutoka Tanzania Daima

SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, amesema hataviomba radhi vyombo vya habari nchini kutokana na kauli yake ya kuwataka wabunge kusoma magazeti kama barua za kawaida.

Makinda alikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa nafasi aliyonayo ni nyeti na asipokuwa makini katika maamuzi yake taifa linaweza kuingia kwenye vurugu na amani kutoweka.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini Bagamoyo wakati akifungua semina inayowahusisha waandishi wa habari za Bunge iliyoandaliwa na ofisi yake.

Akiwa bungeni wakati wa mkutano wa pili uliomalizika mwishoni mwa Februari, Makinda aliwataka wabunge kupuuzia habari za magazeti baada ya moja ya gazeti la kila siku (sio Tanzania Daima), kuandika makala inayoeleza namna anavyokandamiza upinzani kwa kuruhusu ufafanuzi wa kanuni hali iliyosababisha wabunge wote wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.

Alisema kwa kujiamini kwamba hakutegemea kuona makala ya namna ile gazetini hivyo alichukizwa kwa maelezo kwamba waandishi hawazijui kanuni za chombo hicho na pia hawakumuuliza kilichotendeka.

“Wakati nakuja hapa nilitegemea kabisa kuulizwa swali hilo nimejiandaa kutoa ufafanuzi lakini siombi radhi na sitafanya hivyo… nilisikitika na kukasirika sana siku ile …..

kwanza sikutegemea. Mlitakiwa (waandishi) mfahamu kilichofanyika pale ni ufafanuzi wa kanuni tulizojitungia wenyewe hakuna kilichobadilika pale; Mbowe amebaki kuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani popote duniani akienda anatambulika hivyo.

“Mliandika kuwa nakandamiza upinzani bungeni, napenda niwaambie, kwanza sina upendeleo kwa nafasi yangu kama Spika; naweza kusababisha machafuko nchini… katika nchi yoyote kama kweli ningekuwa nafanya hayo mliyoandika amani katika nchi hii isingekuwapo mimi kama mimi ninaweza kuleta machafuko sasa tusiruhusu hali hiyo itokee…

“Kwa kweli siombi radhi kwa sababu huo ndio ulikuwa ukweli, sifungamani na upande wowote lakini pia kilichofanywa na Bunge siku ile pale ni kutoa tasfiri kwenye Kanuni ya 14 (2) toleo la mwaka 2007 inayohusu namna ya kuunda kambi ya upinzani na kuachia kila kitu wahusika wenyewe,” alisema Makinda.

Alisema kihistoria Bunge la vyama vingi lilianza mwaka 1995 na wakati huo lilipitisha kanuni ya kuunda kambi ya upinzani endapo upande wa upinzani ungefikisha asilimia 30 ya wabunge na kwa wakati huo kwa bahati vyama vya upinzani vilifanikiwa kufikisha wabunge 46 na hivyo kufikisha asilimia hiyo 30 iliyowawezesha kuunda kambi ya upinzani.

Kwa mujibu wa Spika huyo, mwaka 2000 vyama vya upinzani havikufanikiwa kufikisha asilimia 30 ya wabunge ndani ya Bunge, ndipo kanuni hiyo ilipobadilishwa na kuwekwa kanuni inayoruhusu chama cha upinzani kuunda kambi iwapo kitafikisha asilimia 12.5 ya wabunge wake wote.

Alisema mwaka 2005 Chama cha Wananchi (CUF) kilipata wabunge waliozidi asilimia 12 na hivyo kuwa na haki ya kuunda kambi ya upinzani ambapo chama hicho kiliunda kambi hiyo kwa kushirikisha vyama vingine vya upinzani ambavyo havikuwa na wabunge wengi.

“Tulichoshauri siku ile ni umuhimu wa kambi ya upinzani kuwa na ushirikiano katika majukumu yake kama ilivyo kwa mabunge yote duniani; Kiongozi wa Upinzani Bungeni mheshimiwa Mbowe, aliunda serikali yake kivuli na kuungwa mkono na Bunge zima kwa kuwa ana haki, hakukuwa na ukandamizaji pale ila tu kanuni zilitafsiriwa,” alisema Spika huyo wa kwanza mwanamke katika historia ya Tanzania.

Awali Makinda alisisitiza ushirikiano wa ofisi yake na vyombo vya habari kwa kutambua umuhimu wa jamii kupata habari sahihi za Bunge na kusema habari ni daraja kati ya mhimili huo na jamii huku akivipongeza kwa kazi nzuri.

Kuhusu tabia ya wabunge kuzomea na kupigana vijembe Spika alisema ikilinganishwa na mabunge mengine ya Common Wealth, Tanzania kuna utulivu hivyo wananchi wategemee makubwa zaidi kwenye mikutano ijayo kwa kutoa mfano wa Bunge la India.

“Jamani huko duniani kuna mabunge ambayo ukiona utajua kabisa kwamba hapa kwetu tumetuilia sana… mimi naruhusu hali hiyo iendelee lakini cha maana mbunge ajue wananchi wake wanataka nini kwanza.
 
Kinda maana yake ni mtoto,awe njiwa au binadamu. Makinda ni watoto.

Mh.Anna Makinda yeye hana watoto;kwa hiyo anajisikia vibaya sana anapoitwa Anna Makinda,ambayo mtu akitamka anatamka kama 'ana makinda'=ana watoto au 'hana makinda'=hana watoto.

Kwa maana hiyo kuambiwa kuwa ana watoto wakati hana inamuuma vilevile kusema ukweli kuwa hana watoto kuna muumiza zaidi.

Hii imepelekea abadili jina kwa nguvu na kujiita Anne Makinda ili kuondoa tafsiri ya moja kwa moja ya kiswahili inayomuumiza roho.
 
Labda ameona ni muda muafaka kutoa angalizo, maana amekuwa mashuhuri sasa, na jina lake lasemwa kila siku. Binafsi naona hayo majina yana maana sawa, lakini yako tofauti kisheria na katu huwa ukayatumia interchangeably. Anne atabaki kuwa Anne na Anna atabaki kuwa Anna. Huwezi kumwita Paul, Paulo au John, Yohana. La sivyo hata majina yetu ya asili kama Aliko, Mujuni, Lugano, Haika n.k pia tuyatafsiri.
 
She's real an iron lady ! Go bless you anne makinda.
<br />
<br />

Iron lady wa namna hii, baaaaaasi kazi ndani ya taifa hili bado ni mbichi. Ingelikuwa mtu anataka kusonga ugali ni sawa na kuwa na kuni bila sufuria wala maji, ni nini anategemea hapo na watoto wakiwa na njaa. Ktk nchi ya shida wananchi wa tz wamegoma kupelekwa, viongozi tafakarini alternativu ya route na siyo kuuza sura kwenye kamere. Ole wako uwe umepewa posho ya kodi yetu na uwe umetoa posho ya kodi yetu kwa waandishi wa habari kwa ajili ya huo upupu; karejeshe hilo fungu mara moja kabla hatujakushitaki kwa Mungu.
 
niwape hongera kwa mitazamo yenu,
kwani alikuwa wapi siku zote mpaka arekebishe jina leo?
 
a.jpg


Spika wa Bunge la Tanzania ametoa ufafanuzi kuhusiana na jina lake. Anasema jina lake ni Anne Makinda na wala sio Anna Makinda. Zaidi ya matamshi, kuna tofauti yoyote kati ya majina Anne, Ann, Anna na Hannah?

dah kweli Mungu anajibu maombi. Nilishamshauri mke wangu Anna akabadili jina mahakamani; ilikuwa inaniuma kweli kuona mke wangu mwenye mvuto anafanana jina na huyu mama mwenye sura kama kinyago cha mpapure.
 
a.jpg


Spika wa Bunge la Tanzania ametoa ufafanuzi kuhusiana na jina lake. Anasema jina lake ni Anne Makinda na wala sio Anna Makinda. Zaidi ya matamshi, kuna tofauti yoyote kati ya majina Anne, Ann, Anna na Hannah?

Naona shughuli za bunge zimepungua hauzi nyago kwenye Luninga zetu za Bongo ndo maana kaamua kuita press conference
 
a.jpg


Spika wa Bunge la Tanzania ametoa ufafanuzi kuhusiana na jina lake. Anasema jina lake ni Anne Makinda na wala sio Anna Makinda. Zaidi ya matamshi, kuna tofauti yoyote kati ya majina Anne, Ann, Anna na Hannah?

so what?
 
Back
Top Bottom