Makinda azuia watu kutumia barabara; yafunguliwa baadaye | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makinda azuia watu kutumia barabara; yafunguliwa baadaye

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Iteitei Lya Kitee, May 14, 2011.

 1. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2011
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Saturday, 14 May 2011

  Joseph Zablon

  SPIKA wa Bunge, Anne Makinda anadaiwa kufunga njia inayounganisha eneo la Kijitonyama na Sinza, Dar es Salaam na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji.Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na baadhi ya wakazi wa sehemu hiyo zimeeleza kuwa kutokana na kufungwa kwa njia hiyo, sasa wanalazimika kutumia dakika 45 kufika Sinza kwa miguu badala ya dakika tano hadi 10 walizokuwa wakitumia awali.

  Mkazi wa eneo hilo, Juma Mbegu alieleza kuwa njia hiyo imefungwa katika Mtaa wa Sahara, jirani na Kituo Kidogo cha Polisi cha Mabatini: "Njia hiyo imefungwa eti kuruhusu ujenzi wa nyumba yake ya ghorofa moja. Unajua mtu hadi agundue kuwa njia hiyo imefungwa, inambidi atembee kama dakika tano hivi ndipo akutane na uzio wa mabati."

  Kwa mujibu wa Mbegu, kibao kilichowekwa mwanzoni mwa Mtaa wa Sahara jirani na Kituo hicho cha polisi kuonyesha kuwa barabara imefungwa, nacho kina utata kwani watu wengi wanajua kuwa imefanyika hivyo kwa magari pekee. Alisema kufungwa kwa njia hiyo inayopita jirani na Kiwanja namba 630 katika Kitalu namba 47, kinachomilikiwa na Makinda, kumesababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo na vitongoji vyake.

  Mkazi mwingine ambaye hakutaka kutajwa gazetini alisema kutokana na kufungwa kwa njia hiyo, watu wanalazimika kuzunguka hadi Barabara ya Shekilango eneo la Afrika Sana, ili kufika eneo la Mori, mwendo ambao ni takriban dakika 45.

  Kauli ya uongozi wa Mtaa
  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kijitonyama, Philip Komanya alipoulizwa jana kuhusu suala hilo alisema hana taarifa ya kufungwa kwa njia hiyo."Sina taarifa na ndiyo kwanza nasikia kwako. Mbona hawajanifahamisha?" alihoji mwenyekiti huyo na kuongeza:"Njia hiyo imekuwa ikitumika pia wakati wa mvua kwani njia inayounganisha ile inayopita katika Kituo Kidogo cha Polisi Mabatini, huwa haipitiki kutokana na ubovu."

  Mwenyekiti huyo alisema anachojua ni kuwa Mei mwaka jana, wakazi wa eneo hilo kwa kumtumia Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wao, Athanas Mapunda waliwasilisha maombi ya kutaka kufungwa kwa njia hiyo kwa sababu za kiusalama, ombi ambalo hata hivyo, lilikataliwa.

  "Walileta ombi la kutaka hilo lifanyike lakini kikao cha kamati ya maendeleo ya kata kilikataa ombi hilo kwa sababu ni njia pekee katika eneo hilo ambayo inaunganisha maeneo mawili tofauti," alisema.

  Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, aliwashauri watafute jinsi ya kufanya ikiwa ni pamoja na kuweka lango la kuingilia katika mtaa huo na walinzi.

  "Pia nilishauri waweke muda wa kupita kwa watu wote na muda wa kupita wenyeji tu. Niliwaambia waweke geti, walinzi na waaandike muda wa mwisho kupita kwa watu wa kawaida lakini siyo kufunga njia."

  Mwenyekiti huyo aliahidi kufika katika eneo la tukio kujionea kinachoendelea akieleza kuwa kisheria, kabla ya kufunga barabara hiyo, mmiliki alipaswa kuwasiliana na ofisi yake.

  "Ngoja nifike hapo baadaye nitakupigia. Unajua wakati mwingine kuna watu huwa wanatumia njia za mkato kwenda manispaa kuomba vibali bila kushirikisha mamlaka nyingine halali. Huu ni ukiukwaji wa utaratibu na ni kinyume kabisa na misingi ya utawala bora."

  Kauli ya Spika
  Spika Makinda alipigiwa simu kutoa ufafanuzi wa madai hayo. Hata hivyo, mara baada ya mwandishi kujitambulisha kwake na kabla ya kumweleza lolote alisema: "Naomba niacheni kwanza. Wasiliana na katibu, tafadhali sana."

  Alipodokezwa kuwa suala lenyewe halihusu ofisi yake, bali yeye binafsi tena ni kuhusu kudaiwa kufunga barabara na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo, alikata simu.Baadaye Msaidizi wa Spika, Herman Berege alipiga simu na kukiri kufungwa kwa barabara hiyo akisema hatua hiyo imefikiwa kwa sababu za kiusalama na bosi wake alifuata taratibu zote.

  Alisema Makinda alipeleka maombi ya kufanya hivyo katika Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni ambako kwa kuwashirikisha maofisa wa mipango miji na watendaji wengine, walikubali kuifunga njia hiyo. Alipoelezwa kauli ya mwenyekiti wa mtaa kwamba maombi hayo yalipelekwa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata lakini yakakataliwa, msaidizi huyo wa Makinda alisema si kweli.

  "Tulikwenda na hadidu za rejea za kikao kilichopitisha uamuzi wa kufungwa kwa njia hiyo na makubaliano yalikuwa ama yawekwe matuta, ziwekwe nguzo kuzuia magari au uzio. Barabara hiyo ilikuwa lazima ifungwe kuzuia vitendo vya uhalifu."Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya Spika Makinda kutaka aishi nyumbani kwake awapo Dar es Salaam badala ya kukaa hotelini kwa gharama za Serikali.

  "Lengo la mheshimiwa ni zuri tu, kunusuru pesa ya Serikali ambayo ingetumika kulipia anapoishi," alisema na kuongeza:"Alikopa kutoka taasisi tofauti ili kujenga nyumba hiyo na kulingana na hadhi yake, watu wa usalama waliona kuna haja ya kuifunga njia hiyo."
  "Nasisitiza kwamba utaratibu ulifuatwa na kama manispaa hawajaifahamisha serikali ya mtaa, hilo si kosa lake (Spika)."
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Haya bwana....walala hoi watakoma mwaka huu!!
   
 3. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Kweli hii nchi mwenye nacho anafaidi!!
   
 4. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Huyo ndiye Mh Spika, Mb wa KUPIGIWA KURA!
   
 5. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Haya bwana huyu ndiye sUpika wetu hANNA MAKINDA ameonyesha upendo wake kwa majirani zake je tulio mbali nae siku akiamua sijui itakuwaje
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  May 14, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Natamani nikayang'oe kwa mikono yangu miwili hayo mabati, lkn nagundua kuwa sikai mitaa hiyooo, yeye nani mpaka azuie raia wema kutumia barabara ambayo ni haki yao kimsingi? halafu anajiita spika wa jamhuri ya Muungano(kama bado upo) huku akiwapoka watu haki yao ya msingi, nchii hii kweli hakuna utawala wa sheria
   
 7. mbweleko

  mbweleko Senior Member

  #7
  May 14, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 157
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hivi kumbe suluhisho ni kufunga njia kwa sababu za kiusalama na sio kuongeza ulinzi pamoja na kukamata wanaofanya uhalifu kwenye njia hiyo!! Yani eti na yeye(spika) akakubali njia hiyo ifungwe, huyo ni kiongozi/kiranja wa wawakilishi wa wananchi!! Asilimia kubwa ya viongozi wetu ni vilaza,yani vilaza kwelikweli,inasikitisha sana!
   
 8. Tympa

  Tympa Member

  #8
  May 14, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hii inasibitisha jinsi gani wadanganyika tunavyopenda amani(hata kama hakuna haki). Simshangai huyu spika kwani ubabe ni jadi yake. Nashauri wananchi tuungane tumkamate kwani anataka kuhatarisha amani kwa wanasinza.
   
 9. Ole

  Ole JF-Expert Member

  #9
  May 14, 2011
  Joined: Dec 16, 2006
  Messages: 751
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hivi ni kwa nini kila spika anapochaguliwa ni lazima ajengewe nyumba na pesa za walipa kodi?
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  BARABARA iliyokuwa imefungwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda katika eneo la Kijitonyama, Dar es Salaam, imeifunguliwa.Barabara hiyo inayounganisha maeneo ya Sinza na Kijitonyama ambayo inapita nje ya nyumba anayoijenga imeanza kupitika jana lakini ulinzi umeimarishwa katika eneo hilo.

  Makinda alifunga barabara hiyo na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na watumiaji wengine kwa kile kilichodaiwa kuwa sababu za kiusalama.

  Barabara hiyo imefunguliwa siku moja baada ya gazeti hili kuripoti kufungwa kwake. Kibao kilichokuwa kinaonyesha kuwa imefungwa, kimeondolewa.Mwandishi wa gazeti hili alifika katika eneo hilo na kukuta kibao cha kuifunga kikiwa kimeondolewa lakini ulinzi wa askari polisi ukiwa umeimarishwa

  “Kaka weka kamera yako katika mkoba, picha hairuhusiwi eneo hili. Askari wa doria wakikukuta na hiyo kamera hapa huenda ukapata matatizo," alisema msamaria mwema mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina na kuongeza kuwa polisi wamekuwa wakifanya doria eneo hilo usiku na mchana.

  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kijitonyama, Philip Komanya alisema barabara hiyo imefunguliwa jana ingawa alidai kuwa suala hilo limemletea matatizo.“Habari za huku mbaya, hali si shwari na ile barabara imefunguliwa,” alisema.

  Komanya alisema hali katika mtaa wake si shwari kuhusiana na suala hilo akidokeza kwamba juzi alikuwa na kikao na wajumbe wake wa Serikali za Mitaa lakini hakutaka kueleza kwa undani walichojadili.

  Hatua ya kufungwa kwa barabara hiyo ililalamikiwa na wakazi wa eneo hilo na wengine waliokuwa wakiitumia kwa kuwa iliwalazimu kuzunguka hadi Barabara ya Shekilango eneo la Afrika Sana ili kufika eneo la Sinza Mori kwa kutumia takriban dakika 45 badala ya kati ya dakika tano mpaka 1o kupitia hapo.

  Alhamisi iliyopita gazeti hili lilimkariri Komanya akisema Mei mwaka jana wakazi wa eneo hilo kwa kumtumia mjumbe wa serikali ya mtaa wao, Athanas Mapunda, waliwasilisha maombi ya kutaka kufungwa kwa njia hiyo kwa sababu za kiusalama ombi ambalo lilikataliwa.

  Hata hivyo, Msaidizi wa Spika, Herman Berege alisema kuwa bosi wake alifunga barabara hiyo baada ya kufuata taratibu zote.Alisema Makinda alipeleka maombi Manispaa ya Kinondoni ambako kwa kuwashirikisha maofisa wa mipango miji na watendaji wengine walikubali kuifunga njia hiyo.

  Alisema: "Barabara hiyo ilikuwa lazima ifungwe kuzuia vitendo vya uhalifu."Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya Spika Makinda kutaka aishi nyumbani kwake awapo Dar es Salaam badala ya kupangishiwa na serikali hotelini."Lengo la mheshimiwa ni nzuri tu, kunusuru pesa ya serikali ambayo ingetumika kulipia anapoishi," alisema.

  Source: Mwananchi.

  My take: Dillusional!!! The sooner our leaders get real the better.
   
 11. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #11
  May 16, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Ili kuish Dar lazima afunge kwanza barabara? Na kabla ya kuwa Spika alikuwa haishi Dar?

  Nadhani viongozi wakikaa madarakani muda mrefu wanalewa sana madaraka.
   
 12. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #12
  May 16, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  issues kama hizi ndizo zilitakiwa zibebewe bango na JF

  imagine mtu angeenda pale akapiga picha kisha inafunguliwa FB account na petition...JF nako kunawashwa moto...then tungeona changes

  Ahhhh let me go back to my sleep maana I was dreaming
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  May 16, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi hatuna serikali?
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  May 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  POWER OF A MEMBER OF RULING PARTY

  Sunday, 15 May 2011 21:48

  [​IMG]

  Spika wa Bunge, Anne Makinda

  Joseph Zablon
  BARABARA iliyokuwa imefungwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda katika eneo la Kijitonyama, Dar es Salaam, imeifunguliwa.Barabara hiyo inayounganisha maeneo ya Sinza na Kijitonyama ambayo inapita nje ya nyumba anayoijenga imeanza kupitika jana lakini ulinzi umeimarishwa katika eneo hilo.

  Makinda alifunga barabara hiyo na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na watumiaji wengine kwa kile kilichodaiwa kuwa sababu za kiusalama.

  Barabara hiyo imefunguliwa siku moja baada ya gazeti hili kuripoti kufungwa kwake. Kibao kilichokuwa kinaonyesha kuwa imefungwa, kimeondolewa.Mwandishi wa gazeti hili alifika katika eneo hilo na kukuta kibao cha kuifunga kikiwa kimeondolewa lakini ulinzi wa askari polisi ukiwa umeimarishwa

  "Kaka weka kamera yako katika mkoba, picha hairuhusiwi eneo hili. Askari wa doria wakikukuta na hiyo kamera hapa huenda ukapata matatizo," alisema msamaria mwema mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina na kuongeza kuwa polisi wamekuwa wakifanya doria eneo hilo usiku na mchana.

  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kijitonyama, Philip Komanya alisema barabara hiyo imefunguliwa jana ingawa alidai kuwa suala hilo limemletea matatizo."Habari za huku mbaya, hali si shwari na ile barabara imefunguliwa," alisema.

  Komanya alisema hali katika mtaa wake si shwari kuhusiana na suala hilo akidokeza kwamba juzi alikuwa na kikao na wajumbe wake wa Serikali za Mitaa lakini hakutaka kueleza kwa undani walichojadili.

  Hatua ya kufungwa kwa barabara hiyo ililalamikiwa na wakazi wa eneo hilo na wengine waliokuwa wakiitumia kwa kuwa iliwalazimu kuzunguka hadi Barabara ya Shekilango eneo la Afrika Sana ili kufika eneo la Sinza Mori kwa kutumia takriban dakika 45 badala ya kati ya dakika tano mpaka 1o kupitia hapo.

  Alhamisi iliyopita gazeti hili lilimkariri Komanya akisema Mei mwaka jana wakazi wa eneo hilo kwa kumtumia mjumbe wa serikali ya mtaa wao, Athanas Mapunda, waliwasilisha maombi ya kutaka kufungwa kwa njia hiyo kwa sababu za kiusalama ombi ambalo lilikataliwa.

  Hata hivyo, Msaidizi wa Spika, Herman Berege alisema kuwa bosi wake alifunga barabara hiyo baada ya kufuata taratibu zote.Alisema Makinda alipeleka maombi Manispaa ya Kinondoni ambako kwa kuwashirikisha maofisa wa mipango miji na watendaji wengine walikubali kuifunga njia hiyo.

  Alisema: "Barabara hiyo ilikuwa lazima ifungwe kuzuia vitendo vya uhalifu."Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya Spika Makinda kutaka aishi nyumbani kwake awapo Dar es Salaam badala ya kupangishiwa na serikali hotelini."Lengo la mheshimiwa ni nzuri tu, kunusuru pesa ya serikali ambayo ingetumika kulipia anapoishi,"
   
 15. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #15
  May 16, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Safi...waandishi wa habari mnafanya kazi zenu. Tungepata mtu anayeuliza maswali magumu na kufanya kipindi kama Current Affairs, ingekuwa raha kweli!
   
 16. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #16
  May 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Joseph Zablon
  BARABARA iliyokuwa imefungwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda katika eneo la Kijitonyama, Dar es Salaam, imeifunguliwa.Barabara hiyo inayounganisha maeneo ya Sinza na Kijitonyama ambayo inapita nje ya nyumba anayoijenga imeanza kupitika jana lakini ulinzi umeimarishwa katika eneo hilo.

  Makinda alifunga barabara hiyo na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na watumiaji wengine kwa kile kilichodaiwa kuwa sababu za kiusalama.

  Barabara hiyo imefunguliwa siku moja baada ya gazeti hili kuripoti kufungwa kwake. Kibao kilichokuwa kinaonyesha kuwa imefungwa, kimeondolewa.Mwandishi wa gazeti hili alifika katika eneo hilo na kukuta kibao cha kuifunga kikiwa kimeondolewa lakini ulinzi wa askari polisi ukiwa umeimarishwa

  “Kaka weka kamera yako katika mkoba, picha hairuhusiwi eneo hili. Askari wa doria wakikukuta na hiyo kamera hapa huenda ukapata matatizo," alisema msamaria mwema mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina na kuongeza kuwa polisi wamekuwa wakifanya doria eneo hilo usiku na mchana.

  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kijitonyama, Philip Komanya alisema barabara hiyo imefunguliwa jana ingawa alidai kuwa suala hilo limemletea matatizo.“Habari za huku mbaya, hali si shwari na ile barabara imefunguliwa,” alisema.

  Komanya alisema hali katika mtaa wake si shwari kuhusiana na suala hilo akidokeza kwamba juzi alikuwa na kikao na wajumbe wake wa Serikali za Mitaa lakini hakutaka kueleza kwa undani walichojadili.

  Hatua ya kufungwa kwa barabara hiyo ililalamikiwa na wakazi wa eneo hilo na wengine waliokuwa wakiitumia kwa kuwa iliwalazimu kuzunguka hadi Barabara ya Shekilango eneo la Afrika Sana ili kufika eneo la Sinza Mori kwa kutumia takriban dakika 45 badala ya kati ya dakika tano mpaka 1o kupitia hapo.

  Alhamisi iliyopita gazeti hili lilimkariri Komanya akisema Mei mwaka jana wakazi wa eneo hilo kwa kumtumia mjumbe wa serikali ya mtaa wao, Athanas Mapunda, waliwasilisha maombi ya kutaka kufungwa kwa njia hiyo kwa sababu za kiusalama ombi ambalo lilikataliwa.

  Hata hivyo, Msaidizi wa Spika, Herman Berege alisema kuwa bosi wake alifunga barabara hiyo baada ya kufuata taratibu zote.Alisema Makinda alipeleka maombi Manispaa ya Kinondoni ambako kwa kuwashirikisha maofisa wa mipango miji na watendaji wengine walikubali kuifunga njia hiyo.

  Alisema: "Barabara hiyo ilikuwa lazima ifungwe kuzuia vitendo vya uhalifu."Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya Spika Makinda kutaka aishi nyumbani kwake awapo Dar es Salaam badala ya kupangishiwa na serikali hotelini."Lengo la mheshimiwa ni nzuri tu, kunusuru pesa ya serikali ambayo ingetumika kulipia anapoishi," alisema.

  Source: Gazeti la Mwananchi, Mei 16, 2011

  VIONGOZI WA TANZANIA WANATUPELEKA KUBAYA!!!
  [​IMG][​IMG]
   
 17. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #17
  May 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  0 #8 joseph magagula 2011-05-16 08:34 Huyu mama anapenda sana kujifanya kama mwanamke mjeuri tena asiyependa kurekebishwa ama kuwekwa katika njia iliyo sawa yaan yeye sidhan kama ana mume maanakama anye basi mume wake ana kazi sana kwan mwanamke huyu anaonyesha FINAL SAY anayo yeye na sio mwingine
  na nyie watendaji wa idara za serilak jueni kuwa kuna leo na kesho acheni kubweteka na walio katika uongoz mana mnawasahau wanaolipa kodi zao kwan ndio wanaoteseka hukumnazidi kuwakumbatia tu wenye vyeo,tukigoma kulipa kodi hao wenye vyeo vyao hata vya kurithishana kama Makamba family wataisho kwel?
  UFISADI TANZANIA KUISHA NI KAMA VILE KUJENGA GHOROFA KWENYE MAJI
  Quote
  0 #7 baba hance 2011-05-16 08:34 MWACHENI AIFUNGE, SI MLIMPA KURA ZENU WENYEWE...? HIYO NDIYO SHUKRANI YAKE KWENU WAPIGA KURA...
  Quote

  0 #6 mwankuga 2011-05-16 08:00 Hii ndio aina ya viongozi tulionao,ambao wanajali matumbo yao.Shame on you Madam Speaker
  Quote

  +5 #5 Sam 2011-05-16 06:30 Ni viongozi wa namna gani ambao si sehemu ya jamii?? Viongozi walio maadui na jamii hawatufai hata kidogo. Viongozi wanaotaka kuabudiwa kama Anna Makinda, Yusufu Makamba, na wengineo hawafai kuongoza jamii yeyote huru na iliyostaarabika ! Hivi karibuni
  Makamba aliwahi kuripo[NENO BAYA] kuwazuia watu wanaomzunguka kupata huduma ya maji, hali hiyo ilipelekea usumbufu mkubwa kwa majirani. Sasa huyu Makinda naye amekuja kivingine na staili ya kufunga barabara.

  Sasa naelewa kwa nini hawa wanaojiita viongozi hawajali matatizo yetu wananchi wa kawaida, wao ni kawaida kuunganishiwa umeme na maji moja kwa moja tena bila usumbufu huku wananchi wengine wakiikosa hiyo huduma, Hawa "wafalme" hawaijui adha ya "kuzungushwa" Tanesco,Dawasco na katika ofisi zingine za serikali ukiitaka huduma. Haohao viongozi wana majenereta, na matanki makubwa majumbani mwao( Simtank lita 50,0000) tabu ya umeme wa mgao na maji kwao ni hekaya tu, ni habari wasioijua na wasiotaka kuisikiliza!

  Wanapewa ulinzi kuliko wa Obama, wanaishi katika makasri makubwa kuliko lile la Osama la Abbottabad, adha ya kufungwa barabara wataijua wapi, adha ya vibaka mitaani kwao ni jambo lisilowahusu!

  Kweli Tanzania tuna wafalme na si viongozi. Familia ya Nyerere iliishi pale Msasani miaka mingapi bila kuwa hata na uzio (mpaka tajiri Mengi akajitolea kumjengea uzio, ambapo Nyerere alikataa)

  Unaweza ukaona aina ya viongozi tulionao sasa, ni viongozi wa kujijengea uzio wa ukuta mrefu kuzunguka makasri yao, ni ya aina ya viongozi ambao wako tayari hata kufunga barabara ili kuwadhibiti raia wengine "wasumbufu"
  Ni viongozi hawa hawa miezi michache nyuma walipita kwetu wakiomba kura, huku wengine wakipiga mpaka magoti, wengine wakitoa"shikamoo" kwa wananchi, wengine wakilia ili mradi tu wapewe kura!

  Lakini leo, baada ya kuingia madarakani...???
  Quote

  0 #4 ahmed 2011-05-16 05:58 Mwananchi hongera kwa kufichua UFISADI wa SPIKA.Wanadai usalama kwani hawakulijua suala hilo kabla hawajauza nyumba za serikali osterbay na seaview?
  Wanaharakati tutapambana na MAFISADI HADI KIELEWEKE
  Quote

  +3 #3 Mary 2011-05-16 04:30 Quoting Bakari:
  Viongozi wetu wamekuwa "MIUNGU", wacha tuone mwisho wetu utakuwaje!​
  iko siku yao tu, wanaodhani kuwa nchi ni ya kwao..kwani yeye nani uyu makinda?yani huo uspika utadhani amekuwa rais wa dunia P U M B A V U kabisa
  Quote

  +3 #2 Bakari 2011-05-16 04:25 Viongozi wetu wamekuwa "MIUNGU", wacha tuone mwisho wetu utakuwaje!
  Quote

  +6 #1 mwamba 2011-05-16 03:51 MAKINDA HAKUFUATA TARATIBU ZOTE NDIO MAANA AMEWAHI AMEFUNGUA KWA HARAKA KUOGOPA KUUMBULIWA,ALIK UWA AMETUMIA NGUVU YA CHEO..VIONGOZI WA TANZANIA WANADHANA POTOFU.HUFIKIRIA AKIWA NA CHEO BASI AMEKUWA JUU YA SHERIA ZOTE.HAPA MAREKANI UTASHANGAA HATA KAMA NI MEYA AU WAZIRI AKISHAMKUTA MTU KWENYE FOLENI HAWEZI KUMPITA LAKINI TZ KIOGNOZI ANAKUWA mungu MTU,KWANINI? MAKINDA NI MJEURI ANAJIFANYA ANAJUA SANA,HATAKI KUREKEBISHWA..UTAFIKIRI MCHAWI!!! WACHAWI NDIO WAJEURI KIASI HICHO.
  Quote  Refresh comments list
  Add comment
   
 18. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #18
  May 16, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  duuuuuuuu,Mama nawe umeingia ktk malumbano na wananchi,kama ni swala la usalama ni bora usikae eneo hilo kuliko kuwafanya wananchi walio wengi kupata tabu kwa matakwa yako wewe mtu mmoja,hata kama ni kiongozi wa mhimili mkubwa hapa Tanzania lakini si vyema ukaleta kelo kwa walio wengi

  Binadamu wote ni sawa na watanzania na wamoja usiturudishe nyuma kwa kutaka tufuate matakwa yako ambayo yanawaumiza wengi
   
 19. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #19
  May 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,347
  Trophy Points: 280
  Haka kamama lazima ni ka kigagula
   
 20. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #20
  May 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Huyu mwenziye alianza hivyohivyo....Mrs Gbagbo

  [​IMG]
   
Loading...