Makinda achukuliwe hatua gani kumdhalilisha mbunge? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makinda achukuliwe hatua gani kumdhalilisha mbunge?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FADHILIEJ, Feb 14, 2011.

 1. FADHILIEJ

  FADHILIEJ Senior Member

  #1
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Wana JF naomba nisaidieni,ikithibitika kuwa ni kweli Pinda ametoa taarifa ambayo sio sahihi,na hivyo kulidanganya bunge,je Spika aliyemwambia mh.Lema ameonyesha utovu wa nidhamu atapaswa achukuliwe hatua gani?
   
 2. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hakuna kanuni inayohusu adhabu kwa spika
   
 3. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  WataPindisha taratibu na kuleta Mizengwe(o) ila kulifutilia mbali kabisa suala la WM kuwa muongo, kwani inajulikana kasema uongo!!!
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa kosa hili napendekeza Makinda apewe uanachama wa klabu ya lile kundi dogo la wakina R.A lililo juu ya sheria.
   
 5. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Shida ni kwamba tumeshika makali. Ila ipo siku, kwa sasa hakuna kitakachofanyika kwani wanaweza kukaa bungeni na kutunga kanuni siku hiyo hiyo. Huwafahamu!
   
 6. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Huyu mama Anna Makinda aka 'alikwina' ndiye chanzo cha matatizo Tanzania kwa sasa...!
  Na nchi bila bunge lenye uongozi makini, ni nchi iliyokwishakufa...., Hapa anatekeleza maagizo ya CCM na siyo kanuni za bunge - maana yaelekea kabisa kuwa anapanic, hazijui au hazikumbuki na analazimishia aonekane ni mkali au anakomaa kumbe ni ukosefu wa busara, akili na uongozi.

  Tanzania yote inahitaji kuundwa upya, na hii bila shaka dalili zote zinaonyesha kuwa kuna mianya mingi ya nguvu ya umma kuchukua uongozi, ikiwa ni pamoja na kutokea ktk anguko la mhimili huu, Bunge! Wananchi wanapoteza imani haraka sana, na hatima yake haitabiriki..
   
 7. M

  Mutakyamirwa JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 4,873
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  Kwa hali ilivyo ni vigumu kuchukuliwa hatua yoyote kwa kwa Mawaziri au Spika wa serikali iliyopo madarakani. Kinachoonekana kwa sasa ni Viongozi kulindana wao kwa wao. Hali hii sijui itaishalini.

  Cha msingi ni wananchi/zaidi wapinga kura kuona makosa wanayoyafanya viongozi na kuchukua hatua zinazostahili-hii ni pamoja na maandamano/kauri za kutaa vitendo viovu na zaidi uchaguzi ufikapo wasipokee Rushwa wala kurubuniwa kwa njia yoyote hile. Kinachosikitisha sasa nikuwa hata kama mkondo wa sheria ungefuatwa bado haki haionekani kutendeka.
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,636
  Likes Received: 4,746
  Trophy Points: 280
  Mbona siku nyingi huyu alikwima ni senior member of the bongo billioners club. Huoni macho yake yalivyokuwa mekundu kwa kunywa damu za watanzania?
   
 9. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Huyu mama hatekelezi matakwa ya CCM. Utii wake wa kwanza anauelekeza kwa wale waliompatia kiti cha enzi huku wakijua kwamba ni spika dhaifu ambaye elimu yake inatia mashaka na hata uwezo binafsi ni wa ovyo. Najiuliza nchi hii itakuwa katika hali gani baada ya miaka mitano ya utawala wa namna hii!
   
Loading...