Makinda aanza kazi aliyotumwa

Kuna tetesi kuwa hoja binafsi ya Katiba iliyowasilishwa na Mh. Mnyika na ile ya Dowans ya Mh. Kafulila hazitajadiliwa katika kikao kijacho cha bunge kwa kisingizio cha kutoundwa kamati ya uongozi ya bunge yenye jukumu la kupitia hoja za serkali na wabunge binafsi na kuzitolea uamuzi..
Dalili hizo zimejitokeza baada pia ya spika mwanamama Makinda kusema ofisi yske haijapokea hoja binafsi ila imepokea taarifa tu za makusudio ya kuripoti hoja.

Binafsi nanusa harufu ya kutimia malengo ya waliomuweka hapo na ucheleweshaji wa makusudi ili maamuzi ya kibabe yapitishwe kwanza

Source: Nipashe Jumanne 18 January 2011

Ni kweli Mnyika hajawasilisha hoja bali ni kusudio tu. Kusudio lake halina tofauti na barua ya posa, kwa hiyo mpaka akijibiwa ndipo atoe mahari
 
Makinda, sidhani kama ana ubavu wa kufanya hivyo, na iwapo atafanya hivyo basi hoja hizo zitarudi kwetu wananchi tutawatia adabu JK na serikali yake, mwenzie kanyolewa yeye atie maji
 
Huyu bibi Makinda ni time-bomb. Atalipuka then sisi tutafanyia kazi remains zake. Ni zao na chombo cha ufisadi.
 
wakuu zile tetesi zimekuwa kweli...hoja hizo mbili zimetupwa kijanja eti suala la Dowans lipo mahakamani na na suala la Katba Raisi keshatoa maelekezo na yeye ni sehemu ya bunge! Je tutafika kweli kwa mtindo huu wa kuzimana Hoja? sasa bungeni wanaenda kujadili nini?
 
Hapo wanachochea moto na hasira siku zote "Ukiizima haki ya watu tena ya misingi kabasa kwa njia yote ile ya dhuluma, ulaghai, ubinafsi, na jeuri haki hiyo iliyodhulumiwa haifi itabaki hai mioyoni mwa wenye haki hiyo na hatimaye haitamuacha yeyote aliyeidhulumu akabaki salama kwa muda wote" NUKUU NI YANGU.
 
Makinda hana uwezo wa kuzuia demokrasia na mawazo ya watanzania eti kwa sababu yeye ni spika wa Bunge. Mapinduzi ya kifikra hayawezi kuzuiwa bungeni kwani yataenea nchi nzima. UDSM wamempiga mawe waziri, Mbeya (MIST) walimzomea waziri, Mbeya walimpiga mawe JK, Kyela walimfukuza Ridhiwani.Maandamano, migomo kila kona. Si lazima makinda akubali hoja hiyo hali tayari imeshakuwa mbaya. Kilichobaki ni kimoja tu; CCM kuondolewa kwa nguvu, nami naamini sooner or later this will happen!
 
Ukitaka kutoa mtihani kubaini kama Kiongozi anamapenzi ya dhati na nchi yake au la mpatie cheo ambacho hajakitolea jasho.
 
wakuu zile tetesi zimekuwa kweli...hoja hizo mbili zimetupwa kijanja eti suala la Dowans lipo mahakamani na na suala la Katba Raisi keshatoa maelekezo na yeye ni sehemu ya bunge! Je tutafika kweli kwa mtindo huu wa kuzimana Hoja? sasa bungeni wanaenda kujadili nini?

nchi za wenzentu wanajadili jinsi ya kujenga madalaja sis marumbano
 
JeyKey haya si malumbano ni hoja muhimu zinazogusa maslahi ya taifa na bungeni ndo mahali pake
 
nchi za wenzentu wanajadili jinsi ya kujenga madalaja sis marumbano
Na hayo 'madalaja' wanayojadiji kujenga ni kwa pesa za nani??We pesa za kuokotesha tu tulizo nazo zinafisadishwa alafu unataka watu wajadili kuweka nyumba paa wakati msingi umeporomoka!Be a thinker...usiwe kilaza kiasi hicho!
 
Lazima awatumikie mabwana zake!Na hiyo ni pamoja na kupotezea kila kinachoitishia ccm!Tatizo ni kwamba kulinyamazisha bunge sio kuwanyamazisha wananchi!Ni sawa na mtu anaemwaga mafuta ya taa ili kibatari kisiwake..bila kufikiria yatakwavyosambaa yakitupiwa njiti moja tu moto wake utakuwaje!
 
Anna Makinda asipokuwa makini bunge litamshinda na atapata fedheha, asiposimamia bunge kwa utaalamu na utashi wake akasikiliza waliyompeleka yatakuja kumtokea puani!! Ni mambo mengi ya hila tumeona CCM na serikali yake wanapanga wakitegemea out come itakuwa positive lakini inakuwa negative!! bado hawajifunzi........wakikataa kuwasikiliza wabunge watakataa kuwasikiliza na Umma? Yaliyojiri Tunisia na Misri si kupenda kwa raia bali walivumilia ikafika mwisho!! CCM inafikiri watanzania ni wajinga..........endeleeni kufikiria hivyo.

Kikwete unasema hujui wamiliki wa Dowans? kweli Mungu amekupiga upofu. Tubu kwa watanzania kaka yangu vinginevyo siku itakuja utake kutubu lakini wakati utakuwa umepita!!!!!!!
 
KWA AMRI ZAKE................. NA UGUMU WA HOJA ALIZOTUMWA KUZIBANIA................... nina wasiwasi kama atamaliza muda wa miaka 5. Lets wait and see...........



Makinda is a very stupid and used speaker i have ever had in the world.Ni kweli umeanza kazi uliyotumwa.
 
Anna makinda anaendesha bunge kibabe sana,muheshimiwa zitto anauliza swali(anatoa taarifa)kuhusu zain kwenda airtel kwamba kuna baadhi ya vitu avikufuatwa,nakatishwa na kuambiwa amechelewa kuota taarifa,sijui kama tutafika:
 
Back
Top Bottom