Makete: Wananchi waazimia kumfukuza mwananchi anayetuhumiwa kuwaingilia wanawake kishirikina

kilagalila

JF-Expert Member
Nov 8, 2018
320
154
images (10).jpg

Wananchi wa kitongoji cha Ikonda bondeni kijiji cha Ikonda wilayani Makete mkoani Njombe wamemfukuza mkazi aliyehamia katika kitongoji hicho akitokea kijiji cha Ilevelo Bw. Mateso Mbilinyi wakimtuhumu kuwaingilia kimwili kwa njia ya ushirikina baadhi ya wanawake wa kitongoji hicho.

Katika mkutano wa kitongoji hicho uliofanyika kwenye kitongoji hicho wananchi wameelekezea tuhuma kwa Bw. Mateso wakisema amekuwa akiwaingilia kimwili kwa njia za ushirikina huku akipita mtaani na kujisifia kwa vitendo hivyo.

Kaimu Afisa Mtendaji kata ya Tandala Robert Nko kwenye mkutano huo ameanza kuhoji uhalali wa mtuhumiwa kuishi katika kijiji cha Ikonda kama alifika na barua ya utambulisho kutoka kijiji cha Ilevelo.

"Wewe ndio unaitwa Mateso Pius Mbilinyi sio,kilichokutoa Ilevelo ni nini?alihoji mtendaji "ni kutaka kutafuta kipato changu"alijibu bwana Mateso,"Uliondoka kwa usalama kule?alihoji mtendaji tena,"Niliondoka kwa usalama ndio maana wakaniandikia mpaka kibali ninacho"alijibu tena Mateso"ni mahojiano yaliyokuwa yakiendelea baina ya mtendaji na mtuhumiwa.

Wananchi nao wakatoa maoni yao kuhusu tuhuma za mtuhumiwa huyo.

"Utakuta tunaenda mpaka kanisani tunaenda kupokea sakrameti ya watu halafu huku mtaani tunaharibu na usiku tunakuja kuingiliwa,na huyu mtu anatamka kwa kujiamini hata kama nimefanya hivyo mtanifanya nini" alisema mmoja wa wakazi wa kitongoji hicho.

Wengine wamezungumzia hali hiyo wakimtaka mtendaji kufuata taratibu zote za mtuhumiwa huyo kurudishwa alikotoka, huku wakisisitiza walivyosikia ikitangazwa kuwa endepo atapatikana akamatwe apelekwe akiwa hai.

Bw. Mateso Mbilinyi ni mtuhumiwa akizungumza kuhusu tuhuma hizo mbela ya wananchi amesema tuhumu dhidi yake si za kweli na kwa kuwa alishatuhumiwa katika kijiji alichotoka cha Ilevelo kwa tuhuma kama hizo, amesema hata hizi anazopewa ni kwa kuwa jina lake limechafuliwa toka mwanzo kwamba yeye ni mshirikina.

Amesema pamoja na hayo yupo tayari kutii maagizo ya wananchi hao wanaomtaka aondoke kijijini hapo.

"Mimi utakuta tumeingia huku kijijini tunakosana basi,kulingana na jina langu nyumbani lilitoka kuwa mimi ni mshirikina basi wamenichukulia hilo hilo kunikomesha,mtendaji wa kata mimi sitakuwa na mengi zaiidi ninongea mengi mbele yenu niko ladhi kutoka hapa sijajenga nyumba ila nimejenga Mlevela ndio kwetu"alisema Mateso Mbilinyi.

Katika mkutano huo Balozi wa eneo lake ametolea ufafanuzi utata uliojitokeza kuhusu barua ya utambulisho aliyokuja nayo mtuhumiwa katika kijiji cha Ikonda akitokea Ilevelo.

"Niliambiwa huyu mtu hajaja kukaa amekuja kimatibabu anaumwa mke wake nikasema kwa hiyo ana mda gani,akasema ana mda mchache ataondoka ila akisema anataka kupanga vibalua nitakwambia"alisema balozi moja ya maswali aliyohoji wakati akiuliza juu ya ujio wa Mateso Mbilinyi katika kitongoji hicho.

Kaimu Afisa mtendaji kata ya Tandala Robert Nko amesema serikali watatii maagizo ya wananchi kwa kumuandikia barua ya kuondoka kijijini hapo kwenda alikotoka na watafuata taratibu zote za serikali ili kumfikisha salama kijijini hapo.

Kitongoji cha Ikonda bondeni kipo karibu na hospitali kubwa ya Ikonda inayomilikiwa na taasisi ya kidini, na ikiwa maarufu kutokana huduma zinazotolewa na kusababisha wageni wengi kutoka nje ya wilaya na mkoa kufika kwa ajili ya matibabu.
 
Nimechoka nikaishiwa nguvu. Atii, watu wenda zao kanisani na kula sakramenti huku walifinyangwa usiku. Hii mbona hatari?

Je, Mungu siku hizi kazeeka au?

Kwanini baba Paroko au Kasisi mkuu asiwanyime hizo sakramenti zake hao wamama walioliwa usiku?? Yaani mtu kafikishwa kileleni usiku na si mumewe halafu unakuja sema hukufurahia?

We Paroko/kasisi rudi chuoni ukasome tena
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom