Make Money Blogging: Unashida yoyote hapo?

NgimbaErick

Member
Mar 31, 2020
43
125
Heyo!

Kama umekuwa na changamoto kwenye swala la kutengeneza pesa online kupitia blog, niulize hapa ntakupa ushauri kutokana na experience yangu.
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
13,324
2,000
Nafanyaje kuongeza traffic kwenye blogspot ukiachana na kushare ?

Je, kama ni SEO inawezekana ?
 

NgimbaErick

Member
Mar 31, 2020
43
125
Nafanyaje kuongeza traffic kwenye blogspot ukiachana na kushare ?

Je, kama ni SEO inawezekana ?
Kuna njia nyingi za kuongeza traffic kwenye Blog yako, zipo ambazo za kulipia na za bure.
 • Unaweza ukatumia platforms kama Google Ads, Facebook ads, n.k kuwafikia watu wengi zaidi ambao wanapenda kuona taarifa kama unazotoa kwenye blog yako, ila tu njia hizi utahitaji kulipia .. raha yake ni kwamba zitakuletea watu wengi ndani ya muda mfupi.
  • Pia watu hao watakao tembelea Blog yako wanaweza wakawa watu wako wa kudumu, endapo ukitumia email marketing kuwafanya wawe updated na kila taarifa utakazokuwa ukizitoa kwenye blog yako.

 • Njia nyingi unayoweza ukatumia ni Youtube, watu wengi sana ni wavivu wa kusoma, hivyo unaweza ukawa unatumia chance hii kutengeneza video fupi za post zako, na ukawa unaweka link ya post zako kwenye description kule youtube kisha ukawaambia watu wawe wanatembelea blog yako kupata mambo mengi zaidi.
  • Jitahidi sana Kuifanya Blog yako iwe na post fupi na zinazoeleweka, watu wanapenda vitu vinavyoenda kwenye point moja kwa moja.

 • Njia nyingi unayoweza kutumia ni SEO, kama ulivyouliza.... ndiyo, seo ni kitu kikubwa sana kuzidi vyote hapo, kwanza inakuletea traffic bila gharama yoyote ya ziada, pili traffic wanakuwa ni quality kwa sababu wametafuta wenyewe, na tatu inadumu mda mrefu bila gharama ya ziada.
  • Kusema ukweli ukiwa master wa seo, umeshashinda sana, kwasabu SEO sio kitu kidogo.

EXTRA: Jifunze Kutumia Email Marketing, ili uweze kukusanya Emails za watu wanaokutembelea, na ujenge email list ambayo itakuwa ni list ya traffic wa kudumu... ina maana kila utakapoweka post watu wako utakuwa ukiwapa taarifa kupitia email zao.
- Jitahidi hapa kwenye Email Marketing uwe na njia za kipekee, maana wengi utakuta wanaweka tu " signup for my newsletter"... hii kitu kama ni mchanga kwenye blogging haitakusaidia kukuza email list yako... kitu ninachokushauri tumia njia ya kutoa VITU VYA BURE na ubadilishane na email, unaweza ukatoa Kitabu cha pdf , Kozi Fupi, Coupons, n.k ... inachanganya kidogo lakini ni kitu kizuri sana kitakachokutengenezea traffic wa kudumu.
 

NgimbaErick

Member
Mar 31, 2020
43
125
Vp matangazo ya admob kwenye app je yanalipa fresh

Sent using Jamii Forums mobile app
No! sidhani kama yanalipa vizuri cha kwanza watu wengi hawapendi apps zenye matangazo, labda cha kufanya uwe na version yenye matangazo pamoja na Premium Version ya app yako ambayo watu wataweza kulipia kiasi flani kwa mwezi ili wasiwe wanapata hayo matangazo. Hapo unaweza ukapata pesa nzuri kidogo kupitia Premium package ya app yako.
 

NgimbaErick

Member
Mar 31, 2020
43
125
Ni vipi mtu anapata pesa kutokana na blog?
Kuna namna tatu kubwa ninazokahamu.
 1. Kupitia Matangazo ya watu wengine kwenye blog yako.
 2. Kupitia Affiliate marketing, kwamba unakuwa kama dalali wa bidhaa za watu wengine lakini ni vizuri wenyewe ukawa unazitumia. Kisha wanakulipa kwa kila bidhaa yao itakayouzika kupitia wewe.
 3. Kupitia bidhaa zako mwenyewe.
 

NgimbaErick

Member
Mar 31, 2020
43
125
Unaweza kutupa darasa kidogo ,unatumia kampuni gani na unquza physical or digital goods?
Ahsante
Mimi naendesha blog ya mafunzo ya kutengeneza websites.

Natumia Programs Mbali Mbali. ila kwa sasa natumia sana Commision Junction, kupata commision kupitia Domains za namecheap.

inamaana kwenye mafunzo ninapomueleza mtu kutengeneza website, domain ni kitu muhimu so namrahisishia kuinunua kupitia namecheap na mimi napata commision akitumia link yangu kununulia.

alafu aff. marketing ni nzuri sana kwa bidhaa za digital, kwa sababu zinacommision kubwa sana, na yote ni kwa sababu hata vendor wa bidhaa hana haja ya kuunda bidhaa zaidi ya moja kuwauzia watu wengi, so yuko tayari kutoa commision mpaka 100%.
 

Thomas10

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
409
1,000
Blogs unazozisema ndio hizi zinazoweka habari ya siku3 zilizopita kweny front page
Heyo!

Kama umekuwa na changamoto kwenye swala la kutengeneza pesa online kupitia blog, niulize hapa ntakupa ushauri kutokana na experience yangu.
 

Ibrahim augustine

JF-Expert Member
Nov 28, 2017
435
1,000
Mimi naendesha blog ya mafunzo ya kutengeneza websites.

Natumia Programs Mbali Mbali. ila kwa sasa natumia sana Commision Junction, kupata commision kupitia Domains za namecheap.

inamaana kwenye mafunzo ninapomueleza mtu kutengeneza website, domain ni kitu muhimu so namrahisishia kuinunua kupitia namecheap na mimi napata commision akitumia link yangu kununulia.

alafu aff. marketing ni nzuri sana kwa bidhaa za digital, kwa sababu zinacommision kubwa sana, na yote ni kwa sababu hata vendor wa bidhaa hana haja ya kuunda bidhaa zaidi ya moja kuwauzia watu wengi, so yuko tayari kutoa commision mpaka 100%.
Mkuu nimeipenda hio je blog yako ni ya kiswahili au kiingereza?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom