MAKAZI YALIYOJENGWA KIHOLELA (w) ILALA

MJINI CHAI

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
2,185
2,000
Wana Jf nawaombeni mwenye kujua hili anifafanulie, kuna makaratasi wenyeviti/watendaji wa Serikali ya Mitaa katika wilaya ya Ilala wamewagawia Mabalozi wa nyumba kumi kumi ili wawagawie wamiliki wa nyumba zilizojengwa katika maeneo yasiyopimwa ili wajaze na wawaachie wanafamilia watakaokuwa muda wote nyumbani ili wawapatie WADHAMINI walioteuliwa (sijui na nani?) ili WADHAMINI nyumba husika, Karatasi husika hanaonyesha inatoka Halmashauri ya manispaa ya Ilala ingawa haina Nembo, anuwani, muhuri, Tarehe wala sahihi.

naombeni msaada kwa hili maana isije kuwa kama KIPAWA uthamini wa majengo ulifanywa muda mrefu halafu wakaja lipwa wakati fedha yetu imeshuka dhamani.

Nawasilisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom