Makazi duni/slums yametamalaki katika miji na majiji mengi ya Afrika chini ya Jangwa la Sahara

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,471
46,002
Inakadiriwa karibia nusu(47%) ya wakazi wote katika miji na majiji Africa chini ya jangwa la Sahara wanaishi katika makazi duni sana au slums ambayo yana msongamano mkubwa, yamejengwa hovyo bila mpangilio na yenye huduma mbovu za mifumo ya maji safi na maji taka. Tandale, Manzese, sehemu za Mbagala, Kimara, Tegeta ni baadhi ya mifano ya sehemu za au zenye makazi duni.

Uongezekaji wa watu kwa kasi kuhamia katika miji na majiji haya ya Africa unasemwa kwamba unazidisha zaidi hali mbaya ya matatizo ya makazi duni ambayo tayari ipo kwa muda sasa.

Ukuaji wa kasi wa idadi ya watu Africa ni janga linaloendelea kuharibu na kuvuruga maendeleo na hali za kimaisha, unahitaji jitihada za dhati kudhibitiwa.
 
We elite uchwara naona umekuja tena na malalamiko yako ya kutaka watu wauwawe.

Hauliwi mtu hapa. Utakesha na ajenda zako za ibilisi.

Na yale machanjo yenu yenye sumu hayawezi kuwasaidia. Mtahangaika sana.

Na mimi nasema watu wazae kweli kweli. Lakini pia wafanye kazi, walime, wazalishe mali walishe watoto wao.
 
Japo waafrika tunaishi maisha duni kwenye slums na kunya porini na vichakani na IQ zetu kuwa na mushkel tuna uhakikia wa kwenda mbinguni na kuona ufalme wa baba.

"Heri wale wanaoishi maisha ya dhiki, huzuni na ufukara kwani watauona ufalme wa baba"
- Yesu mwenyewe.
 
Japo waafrika tunaishi maisha duni kwenye slums na kunya porini na vichakani na IQ zetu kuwa na mushkel tuna uhakikia wa kwenda mbinguni na kuona ufalme wa baba.

"Heri wale wanaoishi maisha ya dhiki, huzuni na ufukara kwani watauona ufalme wa baba"
- Yesu mwenyewe.
Wewe ndugu mmatumbi tambua kuwa fukara hakuzuii wewe kupata dhambi....wala sio kigezo cha kwenda mbinguni.
 
Back
Top Bottom