Makato ya simu yameongezeka au ni mtizamo wangu?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Ukihamisha fedha naona makato yamekuwa makubwa sana katika mitandao ya simu, mfano laki mbili na nusu wanakata elfu tano Jambo ambalo nitofauti na gharama za zilizokuwa zikitozwa kipindi Cha nyuma.

Je, gawio, Kodi na faini za mahakamani zinaweza kuwa zimechangia hili? Kwamba tumepokea faini la bilioni tano halafu mtoaji ndani ya mwezi anarejesha pesa hiyo na faida juu .......au mimi ndo naona hizi gharama nikubwa?
 
Hicho kipindi cha nyuma ulikua unakatwaje..?!? Labda tuanzie hapo..
 
Hujamsikia mkuu analalamika mapato ya ndani yameshuka? Anafurahi kwa Airtel kupeleka gawio kubwa? Mkuu hela lazima zitoke kwangu na kwako wala sio kwa hao wawekezaji, mkuu anafikiri anawakomoa kwa kuhitaji zaidi kutoka kwao akifikiri atawapunguzia faida kumbe wale wamemtangulia sana kibiashara, wana kata wananchi wake hakuna amna.
 
Kiufupi mkuu hajui duara la uchumi.
Uchumi ni sawa na watu atano waliojipanga kwenye safu....Wa kwanza (serikali) ampige wa pili (mzalishaji), wa pili ampige watatu (whole seller), watatu ampige wa nne ( retailer seller ) wa nne anambamiza konde la maana watano (consumer) na watano hana wa kumpiga., kwa hiyo yy ndo ataumia.

Dr Mpango analifahamu hilo bt hataki kusema
 
Ukihamisha fedha naona makato yamekuwa makubwa sana katika mitandao ya simu, mfano laki mbili na nusu wanakata elfu tano Jambo ambalo nitofauti na gharama za zilizokuwa zikitozwa kipindi Cha nyuma.

Je, gawio, Kodi na faini za mahakamani zinaweza kuwa zimechangia hili? Kwamba tumepokea faini la bilioni tano halafu mtoaji ndani ya mwezi anarejesha pesa hiyo na faida juu .......au mimi ndo naona hizi gharama nikubwa?
Yameongezeka
 
Leo tena nimeenda kutoa 600k, siku za nyuma nilitoa kwa 7500 ila leo imekuwa 8000.
 
Sasa hivi mambo ni kimya kimya...hata umeme naona kama umeongezeka bei maanA duh haukai kabisa...
 
Nilikuwa nakatwa 800 nikitoa buku 9 ila nikashtuka juzi kati imekuwa 900.

Hapo ndo niliposhtuka nikagundua ela inatafutwa popote ilipo, ila sasa ni kimya kimya.

sasa ongezeko la sh100 nalo ni nongwa..?
kwani petrol mwaka huo/wa 800 ilikua bei gani na sasa ni bei gani
 
Back
Top Bottom