Makato ya kutoa pesa ni makubwa, 14% ya unachotoa sio fair

sanalii

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,431
5,072
Yaani kwenye elfu kumi unatakiwa uwe na elfu kumi na moja na mia nne. Hii ni kubwa sana. Wahusika waliangalie kwa kweli maana tena hii tofauti na hata chat zao zinavyoonesha.
Screenshot_20191125-193903.png

Hii ni tigopesa
 
Yaani kwenye elfu kumi unatakiwa uwe na elfu kumi na moja na mia nne. Hii ni kubwa sana. Wahusika waliangalie kwa kweli maana tena hii tofauti na hata chat zao zinavyoonesha.View attachment 1272428
Hii ni tigopesa
ingawa makato makubwa ila njia hii ya kutuma na kupokea pesa kwa simu ni rahisi sana na inaokoa muda na gharama kubwa zaidi..
 
Wahuni tu wametuona watanzania vilaza hatuna umoja wa kulalamika ndiyo Mana wanafanya wanavyo jua wao.
Huenda tusiajirike tena ktk nchi za nje kwa namna tunavyohandle mambo yasiyofaa. Wengi hatujijui tunataka nini kiwe au kuelekea wapi. Vuruvuru.
 
Kwa uelewa wangu jinsi wanavopigwa kodi na Mzee ndivo nawo wanavopanda tra na lesen mnajua wanavowapiga?
 
Mkuu fafanua vizur , hiyo 14% ni kwa kiasi chochote utakachotoa hata ukitoa 100,000?
Kwa maana ninachojua 1400 unatozwa tu kwa unapotoa chini ya 20,000 yaani kuanzia 10,000 mpaka 19,000, mfano;- %14 ya 50,000 = 7000, lakin kiasi kinachokatwa ni 2,700 au ulikuwa unalenga 10,000 tu.
 
Back
Top Bottom