Makato ya fire wakati wa kulipia road licence

jason

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
315
163
Wana jf naomba kufahamu kwa anayejua, yale malipo ya fire ya kati ya 30,000 had 50,000 yanayofanyika wakati wa kulipia road licence yapo kwenye bajeti? na je huwa kuna taarifa yoyote juu ya hayo makusanyo
 
mkuu uko sahihi ukienda kulipia kuna mchanganuo wanakupa na deposit slip mbili mkuu
 
Tanzania kuna mambo. Mtungi mpya wa kuzimia moto wa gari langu unauzwa Tsh 25000. Lakini ada yake ni TSH 40,000. WIZI MTUPU...!
 
Ukishalipa unapewa mtungi? Huu wizi katika Taifa letu umefikia kiwango cha kustaajabisha. Kama wameanza na mitungi, kuna siku tutapaswa kutozwa hadi malipo ya pancha na mengineyo. Kwani tulikataa uonevu wa aina hii kutakuwa tumemvunjia heshima nani?
 
Wana jf naomba kufahamu kwa anayejua, yale malipo ya fire ya kati ya 30,000 had 50,000 yanayofanyika wakati wa kulipia road licence yapo kwenye bajeti? na je huwa kuna taarifa yoyote juu ya hayo makusanyo

serikali dhalimu hii, kuna haja gani kumtoza mtu hiki kiasi ilhali magari yetu yana comprehensive, 3rd part covering fire and theft etc? wizi mtupu, na sijui hizi kodi zingine zinapitishwa wapi na je wabunge wetu wanalijua hili? mbona mnakaa kimya??
 
hata watudai kodi ya kucheka,bongo hatutaendelea kama madini,gesi na wanyama pori tunagawa bure. Vizazi vijavyo watachapa mboko makaburi yetu.
 
serikali dhalimu hii, kuna haja gani kumtoza mtu hiki kiasi ilhali magari yetu yana comprehensive, 3rd part covering fire and theft etc? wizi mtupu, na sijui hizi kodi zingine zinapitishwa wapi na je wabunge wetu wanalijua hili? mbona mnakaa kimya??
Nilitaka kujua tu kama lipo kama njia mojawapo ya mapato ya serikali maana hata stika za nenda kwa usalama nao ni wizi mtupu sasa hili la fire ni pesa nene je inakwenda wapi
 
Inaitwa fire inspection fee ada ya ukaguzi kwa maswala ya moto...si gharama ya kununulia mtungi unapaswa ndani ya week moja baada ya kupata licence yako uende ofisi za fire kwa ajili. Ya ukaguzi na upewe stika bure...

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
uko sahihi,wengi wanafikiri hii ni gharama ya fire ext tu,hii ni gharama ya ukaguzi wa gari lako kama liko salama[fire hazards like wiring etc],ukilipa hio hela tra unaenda fire station wanakagua gari lako na vifaa vya kuzimia moto ulivyonavyo[kama vime-expire wanauza pale au popote utakapo] na gari ikiwa ok wanakupa certificate free of charge
angalizo:nishakwenda pale mara kadhaa hakuna jipya,hata gari bovu linapata hio certificate
 
Stika za nini kama nimelipa fee ya ukaguzi, au ni kutambulisha kuwa nina tungi lililokaguliwa? Kama wakiona haliwezi kuzima moto inabidi nitoe fedha ingine kununua tungi jipya?
 
Hili linaniumiza kichwa haswa kwani juzi nimeenda kulipia Motor Vehicle ambayo nalipaga Tsh 100,000/ nikashangaa nadiwa Tsh. 150,000 baada ya kujumlishiwa na fire na penati.
Wizi mtupu!
 
Tanzania kuna mambo. Mtungi mpya wa kuzimia moto wa gari langu unauzwa Tsh 25000. Lakini ada yake ni TSH 40,000. WIZI MTUPU...!

Kwani ukilipia hiyo ada ya fire inspection wanakupa mtungi wa kuzimia moto? Ni wizi mtupu na sijui kwa nini wabunge hawaulizi hizo pesa zinatumikaje na zinakwenda wapi? Usikute tunachangia chama fulani? Hizo pesa za fire inspection tunazolipa kwenye budget hazimo kabisa? Hili suala tuliwahi kulizungumzia kwa kina hapa JF lakini hatukufikia muafaka wowote, kama kawaida ya Watanzania, ni kulalamika tu lakini hatuchukui hatua. Naona wamekwenda hatua moja zaidi wanalipa kwa bankslip mbili tofauti, last year nilizilipa kwa bankslip moja. Ukiwauliza pale TRA hiyo pesa ni ya nini hawakupi maelezo yoyote yanayoeleweka. Tatizo ni kwamba huwezi kukataa kulipa kwa kuwa imeunganishwa na road licence.

TRA watupe maelezo hizo pesa ni za nini hasa!!!!

Tiba
 
Mimi nimeamua kutolipia tena motor vehicle bora pikipiki iwe kama baiskeli. Nimekwenda kulipia naambiwa nilipie fire, jamani huu si wizi wa wazi? Fire na pikipiki wapi na wapi? Matokeo yake ni kuwa na idadi kubwa ya watu wasio lipia. Silipi ttttttena.
 
Waziri wa fedha kapandisha road license akijua kuna na fire. Mbona haja account hizo fedha za fire?
 
kuna watu wa zimamoto na uokoaji, wanapita maofisini na fomu za kujaza kwa ajili ya cerfiticate za fire za maofisi, je mwalijua hili? mimi nina ki fremu kimoja hapa kariakoo wamemiambia natakiwa kulipia 100,000..! Je tunakwenda wapi?
 
Siwezi kulipia fire inspection kwa buku 50 hata siku moja kama load lisence sawa wakinilazimisha natembelea hvyo hvyo tukakutane mahakamani haiwezekani nikatwe buku 50 bure tu kwenye tlb nalambwa ushuru wa barabara kwenye fuel nakatwa tena kodi ya barabara yani ni wizi wizi tu.
 
Stika za nini kama nimelipa fee ya ukaguzi, au ni kutambulisha kuwa nina tungi lililokaguliwa? Kama wakiona haliwezi kuzima moto inabidi nitoe fedha ingine kununua tungi jipya?
..Mtungi unanunua mwenyewe ile ni ada ya ukaguzi kama una kumbukumbu nzuri kabla ya utaratibu huu kulikuwa na utaratibu wa kulipa 5000 kwa saloon cars na 20,000 kwa station wagon(nisahihishe kwenye hizo tozo) kwa ajili ya kupewa stiker na kama hauna mtungi unauziwa pia...
 
Kwani ukilipia hiyo ada ya fire inspection wanakupa mtungi wa kuzimia moto? Ni wizi mtupu na sijui kwa nini wabunge hawaulizi hizo pesa zinatumikaje na zinakwenda wapi? Usikute tunachangia chama fulani? Hizo pesa za fire inspection tunazolipa kwenye budget hazimo kabisa? Hili suala tuliwahi kulizungumzia kwa kina hapa JF lakini hatukufikia muafaka wowote, kama kawaida ya Watanzania, ni kulalamika tu lakini hatuchukui hatua. Naona wamekwenda hatua moja zaidi wanalipa kwa bankslip mbili tofauti, last year nilizilipa kwa bankslip moja. Ukiwauliza pale TRA hiyo pesa ni ya nini hawakupi maelezo yoyote yanayoeleweka. Tatizo ni kwamba huwezi kukataa kulipa kwa kuwa imeunganishwa na road licence.

TRA watupe maelezo hizo pesa ni za nini hasa!!!!

Tiba

uko sahihi,wengi wanafikiri hii ni gharama ya fire ext tu,hii ni gharama ya ukaguzi wa gari lako kama liko salama[fire hazards like wiring etc],ukilipa hio hela tra unaenda fire station wanakagua gari lako na vifaa vya kuzimia moto ulivyonavyo[kama vime-expire wanauza pale au popote utakapo] na gari ikiwa ok wanakupa certificate free of charge
angalizo:nishakwenda pale mara kadhaa hakuna jipya,hata gari bovu linapata hio certificate
 
Kwani ukilipia hiyo ada ya fire inspection wanakupa mtungi wa kuzimia moto? Ni wizi mtupu na sijui kwa nini wabunge hawaulizi hizo pesa zinatumikaje na zinakwenda wapi? Usikute tunachangia chama fulani? Hizo pesa za fire inspection tunazolipa kwenye budget hazimo kabisa? Hili suala tuliwahi kulizungumzia kwa kina hapa JF lakini hatukufikia muafaka wowote, kama kawaida ya Watanzania, ni kulalamika tu lakini hatuchukui hatua. Naona wamekwenda hatua moja zaidi wanalipa kwa bankslip mbili tofauti, last year nilizilipa kwa bankslip moja. Ukiwauliza pale TRA hiyo pesa ni ya nini hawakupi maelezo yoyote yanayoeleweka. Tatizo ni kwamba huwezi kukataa kulipa kwa kuwa imeunganishwa na road licence.

TRA watupe maelezo hizo pesa ni za nini hasa!!!!

Tiba

kuna watu wa zimamoto na uokoaji, wanapita maofisini na fomu za kujaza kwa ajili ya cerfiticate za fire za maofisi, je mwalijua hili? mimi nina ki fremu kimoja hapa kariakoo wamemiambia natakiwa kulipia 100,000..! Je tunakwenda wapi?

Jeshi la zimamoto watakusaidia katika hili...nenda fire
 
Back
Top Bottom