Makatibu Wakuu wa SADC wakutana Kinshasa, Tafsiri ya nyaraka za SADC katika Lugha ya Kiswahili kujadiliwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ( SADC) umefunguliwa leo tarehe 13 March 2023 jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambapo ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban.

2DAD7D51-8D64-4ABD-B4D3-BADB83F2258A.jpeg

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye ni Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC ngazi ya Makatibu Wakuu akiwa katika meza ya Tanzania wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa SADC unaofanyika Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Makatibu Wakuu, Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mtangamano wa Kikanda wa DRC, Balozi Songhu Kayumba amesisitiza umuhimu wa wajumbe kushiriki kikamilifu kwa kutoa maoni yatakayolenga kufanikisha utekelezaji wa agenda zitakazojadiliwa.

Makatibu Wakuu wanajadili agenda mbalimbali ambazo ni pamoja na hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Maamuzi ya Wakuu wa Nchi na Serikali waliyotoa katika Mikutano iliyopita.

9544D08F-DFF8-4A1D-9D0C-6982D6EA27F3.jpeg

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mtangamano wa Kikanda wa DRC ambaye ni Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu, Balozi Songhu Kayumba akisoma hotuba ya ufunguzi ya kikao hicho.

Tanzania inashiriki kikamilifu kwenye Mkutano huo na imejipanga kusukuma utekelezaji wa agenda ilizoziibua au kuziunga mkono katika mikutano iliyopita.

Agenda hizo ni pamoja na: ujenzi wa sanamu la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambalo litasimikwa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU);
Tafsiri ya Nyaraka muhimu za SADC katika lugha ya Kiswahili ambayo ni hatua muhimu ya utekelezaji wa matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye Jumuiya; Mpango wa Kanda wa Ununuzi wa Pamoja wa Bidhaa za Afya unaoratibiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Mkakati wa pamoja wa Kanda wa Kusimamia Sekta ya Mbolea.

537F8313-5EB8-4D87-B7FA-5A1CFA4CB817.jpeg

Wajumbe wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wanaoshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC, ngazi ya Makatibu Wakuu unaofanyika Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena L. Tax (Mb) anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri utakaofanyika kuanzia tarehe 18 hadi 20 Machi 2023 baada ya Mkutano wa Makatibu Wakuu kukamilika.
 
Elimu,Afya na usafirishaji wa bidhaa bado tatizo wao wanajadili sanamu si kila mtu ajenge sanamu lake Kama wanaona ni muhimu wao wajadili changamoto zinazokabili Nchi za Afrika wenzetu wanatumia legend za udereva kusafiri kwa Nchi zao wao wapo busy na vitu vidogo vidogo...
 
Waachane kabisa na ajenda hiyo na kama hawaamini waulize familia ya Mwalimu Nyerere. Mwl hakutaka mambo hayo hata ya Dodoma kina Makongora hawataki yake kutokea ya Saddam Hussein nk.
 
Sio sanamu la shujaa wa Afrika tena? Ni la Nyerere? Ha ha ha; Afrika noma sana.
 
Waachane kabisa na ajenda hiyo na kama hawaamini waulize familia ya Mwalimu Nyerere. Mwl hakutaka mambo hayo hata ya Dodoma kina Makongora hawataki yake kutokea ya Saddam Hussein nk.
Hapana,we don't have a problem with that. Kama wanataka kujenga sanamu,hatuna matatizo na hilo. Nadhani ilikuwa ni suggestion ya Kabudi.
 
Afrika bana
Bara giza lenye matatizo sugu mengi sana linakaa kwa pesa za kodi zetu kujadili sanamu?
Afrika hovyo mno
Aisei! Issue siyo sanamu ni wewe, mimi na next generation ijifunze uongozi unaojali na kulinda maslahi ya Afrika moja. Sanamu ni picha tu ktk literature....

Ingekuwa vipi kama Patrice Lumumba angelikuwa PM wa DRC kwa miaka mingi na kujenga taifa? Je, Maimai, M23, ADF wangetawala pori mashariki ya DRC? Ingekuwa vipi kama JK Nyerere asingeisaidia FRELIMO, SWAPO, ZANU PF, MPLA? Nk...😀😀😀. 🙏🙏🙏.
 
Back
Top Bottom