Makatibu Wakuu kusaini kiapo cha Maadili hadharani

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,680
149,874
Hii ni moja ya habari katika magazeti ya leo ambapo inasema Makatibu Wakuu wote watatakiwa kusaini Kiapo cha Maadili hadharani.

Chanzo:Magazetini kupitia Channel 10.

Mawaziri je?
 
Last edited:
hata wakina Chenge, Tibaijuka walisaini kiapo cha maadili,,kama mtu ni mwizi ni mwizi tu hata ale kiapo cha namna gani hataacha..nawajua makatibu wakuu wateule wa magufuli zaidi ya kumi ambao ni wezi, walarushwa wakubwa.
 
Tuache unafiki waliomkosesha urais Lowasa ni kelele za chadema na magazeti ya mwanahalisi.

Madhara ya kumwita fisadi kwa miaka 10 ,,siyo tu yamemgharimu lowasa mbali hata chadema heshima yao imeshuka sana mbele ya macho ya watu wenye akili
 
Hii ni moja ya habari katika magazeti ya leo ambapo inasema Makatibu Wakuu wote watatakiwa kusaini Kiapo cha Maadili hadharani.

Chanzo:Magazetini kupitia Channel 10.

Mawaziri je?
Mkuu, JK mwenyewe alisaini kiapo chake 2005 na 2010 hadharani tena uwanja wa taiga na TV zote za nchi hii zilionyesha na hata zile maarufu duniani clips hizo wanazo. Lakini jee yeye na wenzake waloapa wametufanya nini na sisi jee tumekuwa na cha kufanya dhidi yao?
Nasema kwa moyo mweupe kabisa serikali hii ya sasa inataka kuleta usanii lakini haina wasanii mahiri kama ile iliyopita ambayo imeendesha usanii kwa miaka 10 bila kushtukiwa na wengi mpaka pazia linafungwa ndio watu wanashtuka alaaaa! Kumbe ilikuwa comedy?
 
Kuapa hakusaidii kitu bora wangesema tu nisipolitumikia taifa kwa uaminifu nitimuliwe amiin
 
Kumbukeni nyie mnaomtuhumu Chenge ipo siku mbowe atabadili gia angani ,na Chenge kutangazwa kugombea urais kupitia chadema.
 
Tuache unafiki waliomkosesha urais Lowasa ni kelele za chadema na magazeti ya mwanahalisi.

Madhara ya kumwita fisadi kwa miaka 10 ,,siyo tu yamemgharimu lowasa mbali hata chadema heshima yao imeshuka sana mbele ya macho ya watu wenye akili
Maneno kuntu, huwezi kumuita mtu fisadi kwa miaka 10 halafu wewe huyo huyo unakuja baadae kumsafisha kwa kusema mfumo mzima ni mbovu na huyo mtu ni safi!!, watanzania walio wengi wana akili timamu na maamuzi yao siku zote ni ya kuheshimiwa.
 
hata wakina Chenge, Tibaijuka walisaini kiapo cha maadili,,kama mtu ni mwizi ni mwizi tu hata ale kiapo cha namna gani hataacha..nawajua makatibu wakuu wateule wa magufuli zaidi ya kumi ambao ni wezi, walarushwa wakubwa.
Hata Sumaye na Lowasa waliwahi kula kiapo cha maadili
 
Back
Top Bottom