Makatazo yangu na usia wangu juu ya kuchanganya vyakula

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,266
33,039
Nitatoa makatazo kidogo juu ya uchanganyishaji wa vyakula tofauti kwa wakati mmoja, kwani kuna baadhi ya vyakula ukichanganya (kula) kwa wakati mmoja huleta maradhi makubwa. Inshallah Mola atunusuru.

1.Mwenye kukusanya (kula) pamoja mayai na samaki hupata ugonjwa wa kiharusi na kupoza kwa viungo, kwahivo ni vibaya sana kula mayai na samaki kwa wakti mmoja.

2.Mwenye kula samaki na maziwa kwa wakati mmoja hupata ugonjwa wa ukoma na mabalaga.

3.Mwenye kukoga baada kula (kushiba) mtu kupata nimonia, kwani wakati wa kula hizi tundu zetu za jasho hujifungua, na wakati huo huo baada kula ukaenda kukoga basi maji huingia ndani ya mwili na kuweza kusababisha maradhi ya nemonia au pia kupooza kwa viungo

4. Mwenye kula Samaki fresh halafu na baada yake akaenda kukoga maji ya baridi husababisha maradhi ya kupooza.

5.Mwenye Kufanya tendo la ndoa (Sex) bila kutoa manii hii husababisha vijiwe katika kibofu cha mkojo, na ni lazima ukishamaliza tendo la ndoa (Sex) ukojoe japo kidogo.

6
.Mwenye kumuingilia (kufanya tendo la ndoa) mwanammke mwenywe hedhi husababisha kupata maradhi ya ukoma.

7.Mwenye kuota (akatokwa na manii )asikoge, na baadae akafanya tendo la ndoa na mkewe, husababishwa kuzaliwa kwa mtoto mwendawazimu au mtoto aliepumbaa.

Dumisha afya yako kwa kuacha uvivu na pia kujaza tumbo (chakula na vinyaji), Mtume S.A.W amesema kunywa pale unapoona kiu, kula pale unapoona njaa na pia usile ukashiba ila ule ili uondoe ile njaa na kiu ilokuwa nayo kwani nyumba ya maradhi ni kulijaza tumbo.

Kunywa maji unapokua na kiu , kula chakula cha mchana na ujishoonye kidogo baada kula, na kula chakula cha usiku na utembee kidogo kiasi hatua mia kabla ya kulala pia uende chooni kabla ya kulala, na ni lazima mtu ale chakula cha usiku japo kidogo kwani kutokula chakula cha usiku kunazeesha..

Tabibu ambae aliishi wakati wa Mtume S.A.W Al Harith Kalda alisema mambo manne hudhuru kiwiliwili nayo ni:-
Jimai Sex(Kufanya tendo la ndoa) ikiwa umeshiba kwahivo haifai kufanya tendo la ndoa baada ya kula lazima usubiri chakula kisagike ndipo

ufanye tendo la ndoa, kukoga baada ya kula tu, kula Qadid (nyama iliyokaushwa kwa jua) na pia kufanya tendo la ndoa na vizee.Kabla ya kufa tabibu huyu aliwakusanya watu wake na kuwapa maelezo yatakayowafaa nayo aliwaambia kuwa: Msioe wanawake ila wale waliokuwa shababu

yaani wenywe umri mdogo, wala msile tunda ila lilowiva na jitahidini kusafisha maida kila mwezi kwani hutoa balaghamu, pia aliwaambia msile dawa ila mkiwa wagonjwa, wala msile chakula ila mkitafune sana mpaka kiwe laini, wala msizuie mkojo wala usile chakula ikiwa huna njaa na

tahadhari kula ambacho meno yako hayawezi kutafuna ili maida yako isije kushindwa kufanya kazi,na wala usifanye tendo la ndoa ukiwa huna hamu ya kulifanya, na la muhimu zaidi usitoe damu yako bila sababu ya msingi.

Mambo matano hudhoofisha kiwiliwili:-
Kufanya tendo la ndoa kwa sana, kuwa na hamu nyingi au kujitamanisha, kunywa maji mengi kabla ya kula, na kula sana vitu vikali mfano embe mbichi nakulala usingizi mwingi

Mambo manne hutia unyonge macho:
Kutizama mambo machafu, kUtizama aliyesulibiwa, kutizama tupu ya mwanammke, kukaa ukawa umeipa maungo kibla.

Mambo matatu huzidisha akili:
Kuacha maneno mengi (Hadithi ya Mtume inasema: Ni bora kukaa kimya ukiwa huna maneno ya maana), Kupigwa mswaki mara kwa mara, na kukaa na wanazuoni na watu wema.

Mambo matano hukondesha au hata kuua:
Kua mkono mtupu (huna kitu), Kufarikiana au kutengana na uwapendao, Kumeza machungu au kuvumilia machungu, Kukataa nasaha, na kucheka watu wenye akili.

Mambo yanayotia nguvu kiwiliwili:
Kuvaa nguo laini kwa mfano kanzu, kula chakula kizuri, na kunukia harufu nzuri.. hii kunukia kwa wanawake sio kwamba wajitie manukato watokapo njee laah! hii yaani kuwa msafi kutonuka jasho na mambo mengine mengine na kama unataka kunukia manukato basi uwe upo nyumbani tu.

Mambo manne huleta rizki:
Kufanya ibada usiku, kuleta istighfaar kwa wingi, kuzoea kutoa sadaqa, na Kumtaja Allah S.W mwanzo wa siku na mwisho wa siku.

Mambo manne yanayozuia rizki:
Usingizi wa asubuhi, Kufanya ibada kwa uchache, Wivu/chuki, na Khiyana..

Kufanya uchache katika kitu chenye kudhuru ni bora kuliko kufanya wingi cha kitu chenye kufaa.

Kwahivo tujitahidini kuyaacha hayo mambo madogo madogo yanayosababisha maradhi makubwa mno. Kwani afya ni neema kubwa alituruzuku Mola wetu, mtu haithamini afya yake mpaka pale ugonjwa utakapompata ndio hujui neema ya afya.

HAYA NDIO MAUSIA YANGU MAKUU UKIYAFUATA MARADHI YATAKUWA MBALI NA WEWE INSHALLAH...
 
Matabibu takribaan wote wamewafikiana kwamba mambo sita husababisha maradhi mengi sana:

1. Kukithirisha jimai. Kufanya tendo la ndoa sex
2. Kunywa maji usiku mwingi.
3. Kulala kidogo sana wakati wa usiku.
4. Kulala sana wakati wa mchana.
5. Kula tena baada yakwisha kushiba,
6. Kuuzuia mkojo.

Mtu yataka anywe maji anaposhikwa na kiu, ahakikishe kwamba maji ni safi na bora ya maji ni maji yalio baridi na ubaridi usie baridi unayoumiza iwe baridi ya kiasi na atoe nje ya glass. Na anywe mara 3 asifululize kunywa maji moja kwa moja kwani husababishwa kuumwa na Ini. Na lazima ukianza kunywa upige bismillah na ukimaliza useme alhamdulillah.
Usinywe maji yalio moto ila kwa udhuru maalum wala usinywe maji yalitoiwa katika chombo ambacho hakioneshi maji ndnai yake kwa mfano glass nyuesi au chupa nyeusi, kwani ni hatari huenda ikawa kuna vijidudu ndani ya maji.
Kunywa maji asubuhi kabla hujala chakula na pia ukiamka usingizini uzuri
kunywa japio nusu glass ya maji kwani hupunguza joto la matumbo.

Usinywe maji ya baridi baada kula matunda vyakula moto vyakula venye chumvi nyingi navyakula venye sukari nyingi.

Mtu akiwa anapumzika ama atakua amejinyoosha ama amekaa tu au amepumzika kwa namna yoyote ile, lakini haitakiwi adumu katika hali moja tu mpaka achoke. Isiwe mfano kalala au kuka tu mpaka achoke lazima ajibadilishe kwani huweza kuleta madhara katika kiwiliwili chake.

Usingizi ni utulivu wa viungo kuwa viungo vote huwa havishughuliki na chochote kwa mfano macho huwa yamefumba masikio hayasikii kwahivo viungo vyote vimetulia.
Usingizi una faida mbili moja ni kuwa viungo kustarehe na kutulia baada ya kupata tabu siku nzima na pia ubongo unatulia na kupata raha ya nafsi kwa shida ya na tabu za fikra hamu na mengineo. Kwahio ukiwa katika usingizi unakuwa katika hali ya raha sana.

Faida ta pili ni kwamba harara (joto) jingi huingia katika kiwiliwili wakati wa usingizi na hiyo harara hufanyisha msaada wa kukisaga chakula matumboni.
Kiasi kizuri cha usingizi ni muda wa madaa sita hadi nane ama mchana hata muda wa nusu saa ama saa moja unatosha.

Mtu kukaa muda mrefu macho wakati wa usiku haifai kuupoteza bure amesema Sayyidna Omar R.A " Mimi sipendi kumuona mtu amekaa ovyo hana kazi yoyote hajishughulishi na kazi ya kidini wala kidunia" kwahio mtu ni vema kulala kwani ni pia katika ibada kuliko kukaa bila kazi yoyote wakati wa usiku.

Haifai kula baada ya kwisha kushiba kwani Mtume anasema " Usile ila unapokuwa na njaa na usile ukashiba" kwnai huumiza mashine inayosagia chakula na pia amesema Mtume s.a.w " Nyumba ya maradhi ni tumbo"

Hamna kitu kibaya kama mtu kuzuia mkojo, kwnai husababisha maradhi ya vijiwe katika kibofu cha mkojo

Jimai yataka pale mtu ambapo anahisi shauku na hamu, kwahivyo akiwa katika hali hiyo ya kuhisi anahitaji jimaii itafaa ayatoe kwa njia ya kihalali yaani kufanya tendo la ndoa kwani wakati huo akiyazuia manii kunaweza kumsababishia maradhi.Na pia ikiwa atayatoa kwa njia isiyo ya tendo la ndoa (masterbation) basi huenda akajisababishia maradhi ya mifupa.

Wala jimai haikuwekewa wakati maalum, ila wakati wake ni pale mtu anapohisi hamu na manii yako tayari hata kama ni mwaka mzima mara moja huna shauku.

Ama wale wengine wenye tabia ya damawii ikiwa wanaweza basi pia yataka wasizidi wikii moja mara mbili au mara tatu tu na iwe siku mbali mbalihaifai kufanya mara mbili kwa siku moja kwani kisha huweza kusababisha madhara makubwa. Na wenye kufanya jimai sana humletea uzee upesi na homkosesha nguvu na kutokwa na nywele za mvi katika umri mdogo.

Amepokea Jaffar Bin Muhamad kwa babayake kutoka kwa Ali Bin Abi Talib amesema kuwa Mtume s.a.w amesema: " Mtu akifanya jimai asioge mpaka (kwanza) akojoe asipofanya hivo hurudi mabaki ya manii na huweza humsababishia maradhi makubwa yasiokuwa na dawana akimaliza jimai ajipumzishe.
Imepokewa kwa mtu mzee ambae aliishi miaka mia na hamsini na akawa na afya nzuri na mwenye shawaha kubwa akaulizwa juu ya kuwa na umri mkubwa na shahawa yake bado ina nguvu akasema: "Mimi sikuchanganya chakula juu ya chakula na sikufanya jimai ila baada ya kuwa na hamu na nikimaliza jimai hupunguza harakati zangu kwa siku hiyo.

Jimai nzuri ni mwishio wa usiku kwani jimai mwishi wa usiku ni kama dawa ya kiwiliwili ama jimai mwanzo wa usiku sio nzuri kwani maida huwa bado imejaa chakula. Na matabibu wanasema haifai kunywa maji ya baridi baada kufanya jimai.
 
Nitatoa makatazo kidogo juu ya uchanganyishaji wa vyakula tofauti kwa wakati mmoja, kwani kuna baadhi ya vyakula ukichanganya (kula) kwa wakati mmoja huleta maradhi makubwa. Inshallah Mola atunusuru.

1.Mwenye kukusanya (kula) pamoja mayai na samaki hupata ugonjwa wa kiharusi na kupoza kwa viungo, kwahivo ni vibaya sana kula mayai na samaki kwa wakti mmoja.

2.Mwenye kula samaki na maziwa kwa wakati mmoja hupata ugonjwa wa ukoma na mabalaga.

3.Mwenye kukoga baada kula (kushiba) mtu kupata nimonia, kwani wakati wa kula hizi tundu zetu za jasho hujifungua, na wakati huo huo baada kula ukaenda kukoga basi maji huingia ndani ya mwili na kuweza kusababisha maradhi ya nemonia au pia kupooza kwa viungo

4. Mwenye kula Samaki fresh halafu na baada yake akaenda kukoga maji ya baridi husababisha maradhi ya kupooza.

5.Mwenye Kufanya tendo la ndoa (Sex) bila kutoa manii hii husababisha vijiwe katika kibofu cha mkojo, na ni lazima ukishamaliza tendo la ndoa (Sex) ukojoe japo kidogo.

6
.Mwenye kumuingilia (kufanya tendo la ndoa) mwanammke mwenywe hedhi husababisha kupata maradhi ya ukoma.

7.Mwenye kuota (akatokwa na manii )asikoge, na baadae akafanya tendo la ndoa na mkewe, husababishwa kuzaliwa kwa mtoto mwendawazimu au mtoto aliepumbaa.

Dumisha afya yako kwa kuacha uvivu na pia kujaza tumbo (chakula na vinyaji), Mtume S.A.W amesema kunywa pale unapoona kiu, kula pale unapoona njaa na pia usile ukashiba ila ule ili uondoe ile njaa na kiu ilokuwa nayo kwani nyumba ya maradhi ni kulijaza tumbo.

Kunywa maji unapokua na kiu , kula chakula cha mchana na ujishoonye kidogo baada kula, na kula chakula cha usiku na utembee kidogo kiasi hatua mia kabla ya kulala pia uende chooni kabla ya kulala, na ni lazima mtu ale chakula cha usiku japo kidogo kwani kutokula chakula cha usiku kunazeesha..

Tabibu ambae aliishi wakati wa Mtume S.A.W Al Harith Kalda alisema mambo manne hudhuru kiwiliwili nayo ni:-
Jimai Sex(Kufanya tendo la ndoa) ikiwa umeshiba kwahivo haifai kufanya tendo la ndoa baada ya kula lazima usubiri chakula kisagike ndipo

ufanye tendo la ndoa, kukoga baada ya kula tu, kula Qadid (nyama iliyokaushwa kwa jua) na pia kufanya tendo la ndoa na vizee.Kabla ya kufa tabibu huyu aliwakusanya watu wake na kuwapa maelezo yatakayowafaa nayo aliwaambia kuwa: Msioe wanawake ila wale waliokuwa shababu

yaani wenywe umri mdogo, wala msile tunda ila lilowiva na jitahidini kusafisha maida kila mwezi kwani hutoa balaghamu, pia aliwaambia msile dawa ila mkiwa wagonjwa, wala msile chakula ila mkitafune sana mpaka kiwe laini, wala msizuie mkojo wala usile chakula ikiwa huna njaa na

tahadhari kula ambacho meno yako hayawezi kutafuna ili maida yako isije kushindwa kufanya kazi,na wala usifanye tendo la ndoa ukiwa huna hamu ya kulifanya, na la muhimu zaidi usitoe damu yako bila sababu ya msingi.

Mambo matano hudhoofisha kiwiliwili:-
Kufanya tendo la ndoa kwa sana, kuwa na hamu nyingi au kujitamanisha, kunywa maji mengi kabla ya kula, na kula sana vitu vikali mfano embe mbichi nakulala usingizi mwingi

Mambo manne hutia unyonge macho:
Kutizama mambo machafu, kUtizama aliyesulibiwa, kutizama tupu ya mwanammke, kukaa ukawa umeipa maungo kibla.

Mambo matatu huzidisha akili:
Kuacha maneno mengi (Hadithi ya Mtume inasema: Ni bora kukaa kimya ukiwa huna maneno ya maana), Kupigwa mswaki mara kwa mara, na kukaa na wanazuoni na watu wema.

Mambo matano hukondesha au hata kuua:
Kua mkono mtupu (huna kitu), Kufarikiana au kutengana na uwapendao, Kumeza machungu au kuvumilia machungu, Kukataa nasaha, na kucheka watu wenye akili.

Mambo yanayotia nguvu kiwiliwili:
Kuvaa nguo laini kwa mfano kanzu, kula chakula kizuri, na kunukia harufu nzuri.. hii kunukia kwa wanawake sio kwamba wajitie manukato watokapo njee laah! hii yaani kuwa msafi kutonuka jasho na mambo mengine mengine na kama unataka kunukia manukato basi uwe upo nyumbani tu.

Mambo manne huleta rizki:
Kufanya ibada usiku, kuleta istighfaar kwa wingi, kuzoea kutoa sadaqa, na Kumtaja Allah S.W mwanzo wa siku na mwisho wa siku.

Mambo manne yanayozuia rizki:
Usingizi wa asubuhi, Kufanya ibada kwa uchache, Wivu/chuki, na Khiyana..

Kufanya uchache katika kitu chenye kudhuru ni bora kuliko kufanya wingi cha kitu chenye kufaa.

Kwahivo tujitahidini kuyaacha hayo mambo madogo madogo yanayosababisha maradhi makubwa mno. Kwani afya ni neema kubwa alituruzuku Mola wetu, mtu haithamini afya yake mpaka pale ugonjwa utakapompata ndio hujui neema ya afya.

HAYA NDIO MAUSIA YANGU MAKUU UKIYAFUATA MARADHI YATAKUWA MBALI NA WEWE INSHALLAH...

acha uzushi wako. sayansi ya wapi hiyo?! au mambo yetu yale.... (loliondo)?
 
Mzizi hongera kwa darsa ila haya ni makatazo yako au desturi za waislam toka enzi za mtume wenu?
 
acha uzushi wako. sayansi ya wapi hiyo?! au mambo yetu yale.... (loliondo)?
Mkuu wewe ulitakiwa usome tu kisha uyache kama yalivyo si kusema nimeyatoa kwenye Vitabu vya Sayansi. ukiweza chukuwa hukuweza ache, au nikwambie Kwa Kiingereza? Make It or Break It
 
‘Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji hutoa ishara (indicators), tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa, hauumwi, una kiu, usiitibu kiu kwa madawa – dr. Batmanghelidj'.

Hakuna asiyejuwa kuwa maji ni UHAI. Yaani uhai wetu ni maji, bali hilo linashindikana kwa sababu tunasubiri kiu ndipo tunywe maji tena maji ya baridi kama unavyosisitiza wewe!. ukilima bustani kwa kawaida husubiri saa nane mchana jua likiwa kali ndipo uimwagilie maji, bali utadamka asubuhi na mapema ndipo umwagilie maji. kadharika huwezi kutembea kilomita nyingi na gari na maji yakaisha katika injini na ushuke tu uongeze maji, bali utasubiri kidogo injini ipowe ndipo uongeze maji!.

Ndivyo tunavyopaswa kufanya katika miili yetu. kimsingi laiti watu wote wangetambuwa kuwa maji yana kazi gani mwilini, vitanda vingi vya wagonjwa mahospitalini vingekuwa havina watu. Tunasisitiza watu kunywa maji robo lita robo saa au nusu lita nusu saa kabla ya kila mlo na kisha kuhesabu masaa 2 au 2 na nusu kila baada ya mlo na kunywa tena robo au nusu lita tena ya maji ya kawaida katika joto la kawaida.

Halafu thread hii imekaa kidini zaidi, kumbuka humu kuna watu wa dini mbalimbali hivyo si vema kuunganisha sana na mafundisho ya dini fulani kuwafundisha watu wa dini zote au wale wasio na dini kabisa.

Samahani kama nitakuwa nimekukwaza.
maji ni uhai, uhai ni maji, bila kunywa maji ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni.
maajabuyamaji2.artisteer.net
 
Mzizi hongera kwa darsa ila haya ni makatazo yako au desturi za waislam toka enzi za mtume wenu?
Utajaza mwenyewe nimesema kwenye Kichwa cha habari (Makatazo yangu na Usia wangu) Sijasema Makatazo ya Mtume ninafikiri kiswahili unakijuwa? Nimetumia Lugha ya Taifa sikutumia kiingereza hiyo ni source yangu ukiweza chukuwa hukuweza Acha
Make It or Break It
 
‘Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji hutoa ishara (indicators), tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa, hauumwi, una kiu, usiitibu kiu kwa madawa – dr. Batmanghelidj'.

Hakuna asiyejuwa kuwa maji ni UHAI. Yaani uhai wetu ni maji, bali hilo linashindikana kwa sababu tunasubiri kiu ndipo tunywe maji tena maji ya baridi kama unavyosisitiza wewe!. ukilima bustani kwa kawaida husubiri saa nane mchana jua likiwa kali ndipo uimwagilie maji, bali utadamka asubuhi na mapema ndipo umwagilie maji. kadharika huwezi kutembea kilomita nyingi na gari na maji yakaisha katika injini na ushuke tu uongeze maji, bali utasubiri kidogo injini ipowe ndipo uongeze maji!.

Ndivyo tunavyopaswa kufanya katika miili yetu. kimsingi laiti watu wote wangetambuwa kuwa maji yana kazi gani mwilini, vitanda vingi vya wagonjwa mahospitalini vingekuwa havina watu. Tunasisitiza watu kunywa maji robo lita robo saa au nusu lita nusu saa kabla ya kila mlo na kisha kuhesabu masaa 2 au 2 na nusu kila baada ya mlo na kunywa tena robo au nusu lita tena ya maji ya kawaida katika joto la kawaida.

Halafu thread hii imekaa kidini zaidi, kumbuka humu kuna watu wa dini mbalimbali hivyo si vema kuunganisha sana na mafundisho ya dini fulani kuwafundisha watu wa dini zote au wale wasio na dini kabisa.

Samahani kama nitakuwa nimekukwaza.
maji ni uhai, uhai ni maji, bila kunywa maji ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni.
maajabuyamaji2.artisteer.net
Kama Watu wanajuwa kuwa ni Maji ni uhai kwanini wewe umeweka hiyo Thread yako inayozungumzia Masuala ya Maji? Usingweka tu ingekuwa ni bora tu Mnakuja kuharibu Thread za Watu mumetumwa nini? Thread yako hii hapa kama Gazeti la Uhuru https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/180457-unaogopa-kolesteroli-helemu.html
 
Thibitisha hiyo namba 7 kwa maelezo ya kisayansi
Jaribu kufanya kama una Mke lakini, lala usiku mapema kisha uote ndoto ya kama unafanya mapenzi na Mke wako kisha utoe Manii ndani ya huo usingizi wako ,kisha unapo amka muingilie mke wako halafu akishika mimba utapata majibu yake. Kama huamini fanya utafiti nimetoa changa moto hakuna hizo Mahospitalini wala hao Wana Sayansi hawana hizo Chanzo ni mimi Mzizimkavu hauchimbwi Dawa.
 
acha uzushi wako. sayansi ya wapi hiyo?! au mambo yetu yale.... (loliondo)?

Madrasah (Arabic: ﻣﺪﺭﺳﺔ, madrasah pl.
ﻣﺪﺍﺭﺱ, madāris) is the Arabic word (of Semitic
origin; viz Hebrew midrash) for any type of religious
educational institution. It is variously
transliterated as madrasah, madarasaa,
medresa, madrassa, madraza, madarsa,
medrese etc.
 
Jaribu kufanya kama una Mke lakini, lala usiku mapema kisha uote ndoto ya kama unafanya mapenzi na Mke wako kisha utoe Manii ndani ya huo usingizi wako ,kisha unapo amka muingilie mke wako halafu akishika mimba utapata majibu yake. Kama huamini fanya utafiti nimetoa changa moto hakuna hizo Mahospitalini wala hao Wana Sayansi hawana hizo Chanzo ni mimi Mzizimkavu hauchimbwi Dawa.

WE noma, mzizimkavu usiochimbwa dawa!!!. ''kama una Mke lakini, lala usiku mapema kisha uote ndoto ya kama unafanya mapenzi na Mke wako kisha utoe Manii ndani ya huo usingizi wako ,kisha unapo amka muingilie mke wako halafu akishika mimba utapata majibu yake'', hakuna ukweli wa jambo hili, hii ni sawa na kuamini kuwa jua likiwaka wakati mvua inanyesha simba anazaa!, au ukiwa mjamzito na unakula mayai mtoto atazaliwa bila nywele!. ni mara ya pili sasa nasoma ukibishana vikali na viewers, umeandika mwenyewe hapa ili tusome na tutoe maoni yetu, usichukie kama mmoja wetu anakujibu tofauti na matarajio yako.
 
Madrasah (Arabic: ﻣﺪﺭﺳﺔ, madrasah pl.
ﻣﺪﺍﺭﺱ, madāris) is the Arabic word (of Semitic
origin; viz Hebrew midrash) for any type of
educational institution, whether secular or
religious (of any religion). It is variously
transliterated as madrasah, madarasaa,
medresa, madrassa, madraza, madarsa,
medrese etc.
Asante buji buji na wewe lete Kutoka katika Kanisa kwenye Mafunzo ya Bwana YESU Kristo Muokozi wa Wakristo.
 
WE noma, mzizimkavu usiochimbwa dawa!!!. ''kama una Mke lakini, lala usiku mapema kisha uote ndoto ya kama unafanya mapenzi na Mke wako kisha utoe Manii ndani ya huo usingizi wako ,kisha unapo amka muingilie mke wako halafu akishika mimba utapata majibu yake'', hakuna ukweli wa jambo hili, hii ni sawa na kuamini kuwa jua likiwaka wakati mvua inanyesha simba anazaa!, au ukiwa mjamzito na unakula mayai mtoto atazaliwa bila nywele!. ni mara ya pili sasa nasoma ukibishana vikali na viewers, umeandika mwenyewe hapa ili tusome na tutoe maoni yetu, usichukie kama mmoja wetu anakujibu tofauti na matarajio yako.
Mkuu Elimu ya ndani hiyo huwezi Kuipata mimi nimesoma kwenye vitabu vya wasomi wa wa Zamani wa Mwaka 1200 A.D baada ya YESU Kristo huwezi kupata kwa Wana sayansi wa siku hizi Mwalim wangu ni huyu mimi

IBN SINA
ABU ‘ALI AL-HUSAYN (980-1037)

Hebu Msome hapa hapa chini bonyeza hapa Ibn Sina
Ibn Sina (Avicenna) is one of the foremost philosophers in the Medieval Hellenistic Islamic tradition that also includes al-Farabi and Ibn Rushd His philosophical theory is a comprehensive, detailed and rationalistic account of the nature of God and Being, in which he finds a systematic place for the corporeal world, spirit, insight, and the varieties of logical thought including dialectic, rhetoric and poetry.

Central to Ibn Sina's philosophy is his concept of reality and reasoning. Reason, in his scheme, can allow progress through various levels of understanding and can finally lead to God, the ultimate truth. He stresses the importance of gaining knowledge, and develops a theory of knowledge based on four faculties: sense perception, retention, imagination and estimation. Imagination has the principal role in intellection, as it can compare and construct images which give it access to universals. Again the ultimate object of knowledge is God, the pure intellect.

In metaphysics, Ibn Sina makes a distinction between essence and existence; essence considers only the nature of things, and should be considered apart from their mental and physical realization. This distinction applies to all things except God, whom Ibn Sina identifies as the first cause and therefore both essence and existence. He also argued that the soul is incorporeal and cannot be destroyed. The soul, in his view, is an agent with choice in this world between good and evil, which in turn leads to reward or punishment.
Reference has sometimes been made to Ibn Sina's supposed mysticism, but this would appear to be based on a misreading by Western philosophers of parts of his work. As one of the most important practitioners of philosophy, Ibn Sina exercised a strong influence over both other Islamic philosophers and medieval Europe. His work was one of the main targets of al-Ghazali's attack on Hellenistic influences in Islam. In Latin translations, his works influenced many Christian philosophers, most notably Thomas Aquinas

Soma pia zaidi kwenye Wikipedia bonyeza hapa Avicenna - Wikipedia, the free encyclopedia WanaSayansi wanamjua huyo kuwa ni
Philosopher
 
Hasira za nini au mpaka maelezo kama haya yatolewe na mzungu. Uliza kabla ya kupinga kisha upinge baada ya kutokubaliana na majibu, si unaanza kupinga halafu unauliza!
 
Hasira za nini au mpaka maelezo kama haya yatolewe na mzungu
Uliza kabla ya kupinga kisha upinge baada ya kutokubaliana na majibu
si unaanza kupinga halafu unauliza!
Ebu waambie wewe Wanangojea mpaka aje Mzungu awaambie kuwa kutumia Kibatari wakati wa umeme ukikatika kunaleta madhara ndipo wataamini lakini tukawaambie sisi waswahili wanaleta ubishi Eboo someni jamani Msilete ubishi usiokuwa na elimu mimi nina soma na nina Vitabu vyangu najisomea hata huyo Daktari wa hospitali akiviona ananiogopa na kuniuliza umevipata wapi hivyo vitabu?
 
WE noma, mzizimkavu usiochimbwa dawa!!!. ''kama una Mke lakini, lala usiku mapema kisha uote ndoto ya kama unafanya mapenzi na Mke wako kisha utoe Manii ndani ya huo usingizi wako ,kisha unapo amka muingilie mke wako halafu akishika mimba utapata majibu yake'', hakuna ukweli wa jambo hili, hii ni sawa na kuamini kuwa jua likiwaka wakati mvua inanyesha simba anazaa!, au ukiwa mjamzito na unakula mayai mtoto atazaliwa bila nywele!. ni mara ya pili sasa nasoma ukibishana vikali na viewers, umeandika mwenyewe hapa ili tusome na tutoe maoni yetu, usichukie kama mmoja wetu anakujibu tofauti na matarajio yako.

F.P,
huyu jamaa ni hopeless
 
Haya Mambo 6 niliyoyatoa hapo juu nendeni hata kwa Ma daktari mukawaulize nimewaruhusuni

1. Kukithirisha jimai. Kufanya tendo la ndoa sex
(Kufanya mapenzi na wanawake wengi yaani zinaa, au pia una mke basi wewe unafanya nae Mchana na Usiku kila siku basi ukae ukijuwa wewe Mwanamme utazeeka upesi utaonekana Mzee wakati wewe bado ni kijana na mwili pia utaadhoofika utakosaanguvu na afya pia waweza kupata Ukimwi ukizidisha mambo ya zinaa.

2. Kunywa maji usiku mwingi. Kunywa maji usiku mwingi kwa mfano saa tisa usiku au saa kumi usiku unaweza kupata maradhi ya gafla. Ukinywa utaje jina Mungu uombe dua yako yoyote ile ya kumtaja Mungu. Na unywe fundo 3 kwa pumzi 3 yaani mara tatu glasi moja usinywe kama unakimbizwa.

3. Kulala kidogo sana wakati wa usiku. Kulala kidogo wakati wa usiku pia kunasabibishwa kupatwa na maradhi inatakikana Mtu apate japo usingizi wa masaa 6 kwa Mtu mzima na kwa mtoto masaa 8 ulale ili mwili upumzike.

4. Kulala sana wakati wa mchana. kulala mchana sana kunaleta pia maradhi.

5. Kula tena baada yakwisha kushiba, Pia kula tena wakati umeshiba kunaleta ugonjwa wa kuvimbirwa na tumbo.

6. Kuuzuia mkojo. Kujizuia mkojo wakati unatakiwa uende kukojoa haswa kwa wakati umelel usingizi mkojo umekushika unauzuia unawezwa kupatwa na ugonjwa Vijiwe kwenye Figo

HAYA TENA NIMETOA CHALLENGE NENDENI KAWAULIZENI MA PROFESSOR NA MA DAKTARI WENU HAYO MATATIZO NLIYOYAWEKA WANAYAJUWA? Chanzo ni MziziMkavu
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom