Makapuku Forum

Mahakama Kuu Kanda ya Iringa iliyokaa kupitia kikao chake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe, imewahukumu Washtakiwa wawili Mwapulise Mfikwa (29) na Manase Mhada (25) kunyongwa hadi kufa kutokana na kukutwa na hatia ya kumuua Eva Merikion Mgaya (28) nyumbani kwake katika kijiji cha Ihanga wilayani Njombe.

Washtakiwa wao walitekeleza mauaji hayo baada ya kuvamia nyumbani kwa Eva walipofika kwa lengo la kuiba, akisoma hukumu hiyo Jaji Filmin Matogolo amesema tukio la mauaji lilitokea May 08, 2015 baada ya wawili hao kwenda nyumbani kwa Wilfred Vitus Ng’olo ambaye ni Mume wa marehemu wakiwa na bunduki iliyotengenezwa kwa njia za kienyeji ambapo walivamia, kuiba na kunyang’anya fedha .

Washtakiwa hao pia walichukua simu ya Mume wa marehemu na kumpiga risasi Eva Merikion Mgaya kifuani kwa kutumia bunduki hiyo na kusababisha kifo chake papohapo na kisha kutoweka mpaka walipokuja kukamatwa baada ya upelelezi juu ya mauaji hayo.
Screenshot_20211127-050835_Instagram.jpg
 
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Tuluongoi nchini Kenya ameamua kubuni mbinu ya kujishusha na kujichanganya na Wanafunzi pamoja kwa kuvaa sare za Wanafunzi na hata kula chakula wanachokula Wanafunzi ili kukabiliana na matukio ya vurugu na kudumisha nidhamu Shuleni.

Mbinu hiyo imeonekana kusaidia kwa kiasi kikubwa na Shule hiyo imekuwa na amani na ufaulu mzuri.
Screenshot_20211127-050956_Instagram.jpg
 
Chama cha soka Morocco kimewaahidi kuwapa Wachezaji wa Timu ya Taifa kila mmoja $ 54,000 (Tsh. milioni 124.3) iwapo watafanikiwa kuwa Mabingwa wa FIFA Arab Cup Qatar (November 30-December 18 2021) ambapo Bingwa wa michuano hiyo atachukua USD Milioni 5 (Tsh. Bilioni 11).
Screenshot_20211127-051106_Instagram.jpg
Screenshot_20211127-051127_Instagram.jpg
 
Serikali ya Kenya imetangaza masharti mapya ya corona leo ambapo Wasafiri wanaoingia Kenya wakitokea Afrika Kusini, Hong Kong na Botswana watatakiwa kukaa karantini na kutazamwa kwa ukaribu, hii ni baada ya ripoti za kirusi kipya cha corona kilichozuka kwenye Nchi zao.

Kirusi hicho hatari zaidi aina ya B.1.1.529 kwa sasa kimeripotiwa nchini Botswana na Hong Kong kikiwa kimesambazwa na Wasafiri waliotoka Afrika Kusini ambako kimeanzia, Wataalamu wa WHO watakutana leo kutathmini kirusi hicho na kuona kama watakipatia jina la kigiriki.
Screenshot_20211127-051746_Instagram.jpg
 
URENO HATIHATI KOMBE LA DUNIA
.
Ureno ya Cristiano Ronaldo imepangwa kukutana na mabingwa wa Euro Italia katika kundi moja kwa ajili ya mechi za mchujo kufuzu Kombe la Dunia 2022…
.
Hii hapa droo ilivyopanga mshindi katia ya
Portugal vs Turkey atakutana na mshindi kati ya Italy vs N. Marcedonia
.
Daah Kombe la Dunia mwakani bila Italy au Ureno …
Screenshot_20211127-052305_Instagram.jpg
 
Pablo aahidi kuwafunga Arrows
.
“Kila mechi ni tofauti na tutafanya mabadiliko ya wachezaji kwenye kila mechi kwani wachezaji wetu wote ni bora na tunafanya hivyo ili kuwapa muda wa kupumzika pia kuangalia nani na nani wanatufaa zadi lakini kiujumla tuko vizuri,”
.
“Nimewaona mashabiki wa Simba, wanaipenda sana timu na wanataka ushindi na mimi kwa kushirikiana na benchi la ufundi tupo hapa ili kuifanya timu ipate matokeo mazuri hapo Jumapili na katika kila mechi ijayo,” amesema Pablo.Pablo aahidi kuwafunga Arrows
.
“Kila mechi ni tofauti na tutafanya mabadiliko ya wachezaji kwenye kila mechi kwani wachezaji wetu wote ni bora na tunafanya hivyo ili kuwapa muda wa kupumzika pia kuangalia nani na nani wanatufaa zadi lakini kiujumla tuko vizuri,”
.
“Nimewaona mashabiki wa Simba, wanaipenda sana timu na wanataka ushindi na mimi kwa kushirikiana na benchi la ufundi tupo hapa ili kuifanya timu ipate matokeo mazuri hapo Jumapili na katika kila mechi ijayo,” amesema Pablo.Pablo aahidi kuwafunga Arrows
.
“Kila mechi ni tofauti na tutafanya mabadiliko ya wachezaji kwenye kila mechi kwani wachezaji wetu wote ni bora na tunafanya hivyo ili kuwapa muda wa kupumzika pia kuangalia nani na nani wanatufaa zadi lakini kiujumla tuko vizuri,”
.
“Nimewaona mashabiki wa Simba, wanaipenda sana timu na wanataka ushindi na mimi kwa kushirikiana na benchi la ufundi tupo hapa ili kuifanya timu ipate matokeo mazuri hapo Jumapili na katika kila mechi ijayo,” amesema Pablo.
Screenshot_20211127-053007_Instagram.jpg
 
IMEVUJA: Kwa mujibu wa mwandishi nguli wa Sky Sports, MatteMorreto, ameeleza kuwa tayari Orodha ya nafasi tatu za juu tuzo ya Ballon D'or 2021 ni kama ifuatavyo:
.
Messi
Benzema
Lewandowski
.
Amestahili Messi __?
Screenshot_20211127-053119_Instagram.jpg
Screenshot_20211127-053138_Instagram.jpg
Screenshot_20211127-053158_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

Nimemsikia Captain Khalid Aucho jana akisema ana mkataba wa miaka miwili na Yanga, ambao pia nilisema tangu ile siku anahusishwa na Simba

Lakini kwenye Interview yake Captain anasema "Nina mkataba wa miaka miwili ambao wao GSM wanaufahamu vyema" kifupi ni kuwa yeye kaletwa na GSM

Lakini Engineer Hersi alikana kuwa GSM haisajili wala kulipa mishahara ya Klabu, suala hilo lipo chini ya Yanga wenyewe, ila ukimsikiliza Aucho unapata taswira nyingine kabisa

Kama GSM sio sehemu ya Yanga, wanaufahamu vipi mkataba wa Captain Aucho?

Kilichopo ni bado kofia rasmi ya mkanganyiko Kati ya GSM na majukumu yake pale Yanga, GSM wa Namungo, GSM wa Coastal Union na GSM wa LIGI KUU (Mdhamini)

Ndipo hapo ule mjadala wa FAIR COMPETITION unakuwa na mashiko

Screenshot_20211127-053424_Instagram.jpg
 
Legend wa Soka na Rais wa Club ya Al Ahly ya Misri Mahmoud El Khatib (Bibo) ameshinda Uchaguzi Mkuu wa club uliyofanyika jana, Bibo amechaguliwa tena kuendelea kuwa Rais wa Al Ahly hadi 2025 kwa kura 19,362 huku Mpinzani wake Khaled Suleiman akipata kura 2,320.
Screenshot_20211127-135652_Instagram.jpg
 
Winga wa kimataifa wa Ureno Luis Nani (35) ametangaza kuondoka katika club ya Orlando City ya Marekani baada ya kuitumikia kwa miaka mitatu (2019-2021), Nani aliwahi kucheza Man United kwa miaka 8 (2007-2015).
Screenshot_20211127-135847_Instagram.jpg
 
Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wote nchini kuhakikisha wanasimamia suala la Wanafunzi kupumzika wakati wa likizo ili kuwapatia Watoto muda wa kujifunza masuala mengine ya Kijamii.

Waziri Ummy ameyasema hayo jana baada ya kupata maelekezo ya kisera kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknojia Profesa Joyce Ndalichako ambaye amemtaka kulisisitiza suala hilo ili Wanafunzi waweze kupata muda wa kupumzika kipindi cha likIzo

Akihutubia kwenye Mahafali ya 29 ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo Waziri Ummy amesema Watoto wanatakiwa kupumzika majumbani kipindi cha likizo ili waweze kusaidia kufanya kazi ndogondogo nyumbani, kusoma dini na kusaidia kufanya biashara ndogo za kuwasaidia wazazi pale wanapokuwa likizo.

“Sasa hivi elimu imegeuzwa kama biashara, Watofo wamekuwa wakisoma masomo ya ziada mpaka kipindi cha likizo, hawapumziki, pia Wazazi huchangia fedha kwa ajili ya masomo hayo ya ziada, Watoto hawafaulu kwa kusoma muda mrefu, hivyo nawaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanalisimamia hili”

Amesema Serikali imepanga muda wa vipindi wa saa 8 ikiamini muda huo Wanafunzi wataweza kujifunza kwa kina masomo yote yaliyopangwa kwa siku hivyo amewataka Wakurugenzi kuwaelekeza Wakuu wa Shule kusitisha masomo ya ziada mpaka saa mbili usiku, jumatatu hadi jumapili "naagiza kusitishwa mara moja kwakuwa hatuwajengi Watoto,tunawaharibu kwa kuwachosha kusoma muda wote bila kupata muda wa kupumzika"
Screenshot_20211127-140032_Instagram.jpg
 
UNAAMBIWA: Kikundi cha Wanasheria wanaotetea haki za Wanawake kutoka Nchi tatu za Jumuiya ya Afrika Mashari (Tanzania, Kenya na Uganda) wamepaza sauti wakitaka Wanaume wanaofanya kazi waanze kuwalipa mishahara kila mwezi Wake zao wasio na kazi.

Wakizungumza wakiwa nchini Uganda Wanasheria hao wamesema Wanawake wengi wamepoteza kazi na kukosa mitaji ya kuendesha shughuli kutokana na Corona na kujikuta wanafanya kazi nyingi za nyumba kama kupika, kufua, kuhudumia Wanaumd n.k hivyo wanastahili kulipwa.

Wanawake hao wamewaomba pia Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutunga Sheria na sera ambazo zitasimamia Wanawake kulipwa mshahara na Wanaume zao.
Screenshot_20211127-141055_Instagram.jpg
Screenshot_20211127-141124_Instagram.jpg
 
Katika mbio za UEFA msimu huu, Carlo Ancelotti na Real Madrid yake wanaenda mwendo wa pole kabisa ila wapo serious

Mzunguko wa pili hatua ya makundi wameuwasha sana, Luka, Casemiro na Kroos wote wapo kwenye form tena

Unawaona kama timu moja wapo tishio kwenye ubingwa??
Screenshot_20211127-141342_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

Taarifa kuhusu Clatous Chama kutoka kwa Watu wake wa karibu sana ni kuwa yupo katika hatua za mwisho za kuvunja mkataba na RS Berkane (Mutual Agreements)

Kabla ya Chama kuanza mazungumzo ya kuvunja mkataba aliwasiliana na Simba pekee, kuulizia uwezekano wa yeye kurejea nchini

Simba walibariki hilo ila waliweka wazi kuwa hawana pesa za kuvunja mkataba wake na Berkane hivyo suala hilo lipo juu yake kulimaliza, Chama aliridhia hilo

Mpaka kufikia leo hii, Chama na wakala wake wapo zaidi ya 90% ya kukamilisha uvunjaji wa mkataba kwa maslahi ya pande zote mbili na atakuwa huru

Tayari Simba wamemfungulia milango na kuandaa mshahara na marupu rupu yaleyale kama alivyoondoka, ikiwemo kodi ya nyumba Mikocheni, Dar Es Salaam

Mpango rasmi ni yeye kuwasili nchini mapema zaidi na huenda kabla hata ya derby ya Kariakoo (kama kila kitu kitakuwa sawa) kukamilisha mkataba wake, huku akianza kucheza mwezi January

Kama Simba itafuzu hatua ya makundi Shirikisho basi ataorodheshwa kwenye list kwa ajili ya michuano ya Kimataifa

Watu wake wa karibu wanasema Chama anaitazama Simba pekee, akitumia neno "In Tanzania, it's only Simba"

Mwamba wa Lusaka to Simba for the last dance IS ALMOST A DONE DEAL

Screenshot_20211127-141528_Instagram.jpg
 
Red Arrows wametua Dar
.
Red Arrows wametua Dar kuwakabili Simba, wakiwa na kikosi cha wachezaji 26.
.
Kikosi cha Arrow; magolkipa ni Charles Kalumba, Kenny Mumba na Yasin Mugabi, mabeki ni Elvis Bissong, Benedict Chepeshi, Tresor Tshibwabwa, Prosper Chiluya, Nikson Mubili, Kebson Kamanga na Chiteta Kwalombota.
.
Viungo ni George Simbayambaya, George Mandu, Allasane Diarra, Saddam Yusuph Phiri na Edward Tembo na kwa upande wa washambuliaji yupo Felix Bulaya, Alidor Kayembe, Joseph Phiri, Ricky Banda na James Chamanga.
Screenshot_20211127-141837_Instagram.jpg
 
Msuva: Wachezaji Yanga wajitume Ligi mbio ndefu
.
“Mchango wa Yanga kwangu ni mkubwa ndio maana kila nipatapo nafasi nimekuwa nikipenda kuwatembelea na kuongea na wachezaji wenzangu mawili matatu pamoja na viongozi.”
.
“Nimekuwa na mahusiano nao mazuri tangu niondoke. Kikosi kimebadilika sana na hata nyakati ni tofauti, nachokiona ni kuwa wanawatu ambao wanaweza kufanya makubwa, kikubwa ni kujitoa na kujituma kwa ajili ya timu maana ligi ni sawa na mbio ndefu, inahitaji hesabu za namna ya kuanza na kumaliza,” amesema Simon Msuva
.
Ikumbukwe Mara ya mwisho kwa Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ilikuwa ni msimu wa 2016/17 huku Msuva akiwa sehemu ya kikosi hicho ambacho kilitwaa ubingwa huo baada ya kujikusanyia pointi 68 sawa na Simba lakini utoafuti wa mabao ya kushinda na kufungwa uliwabeba Wananchi.
Screenshot_20211127-141924_Instagram.jpg
 
Kisa hujuma: Yanga Kupumzisha nyota wake
.
"Tutakuwa makini zaidi kwenye mechi yetu dhidi ya Mbeya Kwanza, tunajua mipango iliyopo, tutafanya hivi kujiweka katika nafasi salama kwa sababu tunahofia kupata kadi za njano na kupelekea baadhi ya nyota kuukosa mchezo dhidi ya Simba hapo Desemba 11, hili tumeshalifanyia kazi,"
.
"Tumebaini janja janja za wapinzani wetu kuwatafutia kadi za njano wachezaji wetu nyota, au kufanyiwa rafu za makusudi akiwamo, Khalid Aucho na wengine ili kushindwa kucheza mechi ijayo dhidi ya Simba,”
.
"Tumegundua na tunatarajia mechi yetu dhidi ya Mbeya Kwanza itakuwa na mabadiliko katika kikosi, baadhi ya nyota watapumzishwa kwa ajili ya kujiandaa na pambano letu dhidi ya Simba, tunawahakikishia mashabiki wetu tutarejea na pointi tatu kutoka kwa Mbeya Kwanza halafu Desemba 11, tabu iko pale pale dhidi ya Simba," amesema Hassan Bumbuli.

………………
Screenshot_20211127-142102_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom