Makapuku Forum

Screenshot_20211027-091112_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20211027-091133_Opera%20Mini.jpg
 
Waziri wa Nishati, January Makamba amefanya mazungumzo na Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Abu Dhabi (ADNOC), amefanya kikao hicho na Mkurugenzi Mkuu wa ADNOC, Ahmed Bin Thalith na walijadili masuala mbalimbali ikiwemo kudumisha uhusiano baina ya Tanzania na Abu Dhabi katika sekta.
Screenshot_20211027-143140_Instagram.jpg
 
Wakili wa utetezi, Fridolin Gwemelo katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya na wenzake sita, Fridolin ameweka pingamizi kupokelewa kama kielelezo cheti kilichowasilishwa mahakamani na shahidi wa saba wa jamhuri ambaye ni ofisa wa Tehama wa benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Jofrey Abimael Nnko.

Cheti hicho kinaonyesha Sabaya na wenzake walivyorekodiwa katika benki ya CRDB tawi la Kwa Mrombo, Januari 22 kati ya saa 10:09 hadi saa 11:05 ambacho kilikabidhiwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Wakili Gwemelo ambaye anawatetea mshitakiwa wa tatu na nne katika kesi hiyo, mbele ya hakimu mkazi, Patrisia Kisinda amenieleza mahakama kuwa, cheti hicho hakionyeshi ubora wa vifaa na mfumo uliotumika.
Screenshot_20211027-143342_Instagram.jpg
 
• Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Kamshna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhani Kingai ametoa ushahidi wa maelezo ya mshtakiwa wa pili Adam Kasekwa katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Kingai ametoa ushahidi huo leo Jumatano Oktoba 27, 2021 kwa hatua ya mwisho katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Screenshot_20211027-143542_Instagram.jpg
 
No Chama No Party !!
.
Kocha wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini, mechi ya mwisho wakati anafungwa na Simba alisema hakufungwa na Simba alifungwa na Chama.
.
Simba bila Chama msimu huu tangu uanze hawajashinda katika uwanja wa Mkapa na wamefunga goli moja tu..
.
Wapinzani wao Polisi Tanzania msimu huu wapo kileleni ushindi wa asilimi : WWW

Screenshot_20211027-144113_Instagram.jpg
 
“Nitangulie kusema kuwa Mungu ndiyo kila kitu, siamini kama leo naondoka Simba. Kwangu ilikuwa familia na najua mashabiki wananipenda sana, ikitokea nafasi ya kurudi pasipo na shaka niterejea (akibubujikwa na machozi).”

- Adel Zrane, Mtaalamu wa Mazoezi ya viungo.
Screenshot_20211027-144308_Instagram.jpg
 
Van De Beek azipa urahisi Juve, Everton, Newcastle
.
Kiungo wa Manchester United, Donny van de Beek, 24, ameripotiwa kuwasilisha ombi la kutaka kuondoka kwenye timu hiyo katika dirisha lijalo la majira ya baridi na katika kuhakikisha suala hilo linafanikiwa amebadilisha wakala kabisa.
.
Fundi huyo kutoka Uholanzi anawindwa na Everton, Newcastle na Juventus ambazo zilitaka kumsajili katika dirisha lililopita, lakini hazikufanikiwa. Kushindwa kuondoka kwenye viunga hivyo katika dirisha lililopita ndiko kumemfanya Van de Beek ajiunge na kampuni nyingine ya uwakala ambayo anaamini itakamilisha dili lake la kusepa Manchester United.
.
Mkataba wake wa sasa unamalizika 2023 na amekuwa hapati nafasi ya kutosha kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United hali inayosababisha atamani sana kuondoka kwa kuhofia kwamba atapoteza namba kwenye timu ya taifa.
Screenshot_20211027-144709_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

SIMU YA PROFESA, SIMBA VS POLICE TANZANIA

Dakika kadhaa kabla ya mchezo nilipata wasaa wa kuzungumza na Professor na dakika chache baada ya mchezo nimezungumza nae

Prof leo alinipa kazi nikasome kazi ya Msomi mmoja anaitwa Robert Brimmer kutoka Chuo kikuu cha Winthrop na Joni Boyd,PhD, CSCS!

Wasomi hawa wa Sayansi ya michezo waliandika kitu kuhusu mambo 9 Makocha hufanya wanaporithi timu ya mpira wa miguu!

Nianze na point ya pili inasema "Focus forward, glance back" ni wazi Kocha Hitimana anafahamu kutakuwa na ukosoaji mkubwa wa Simba hii dhidi ya Simba zilizopita, atautazama msimu uliopita kama sehemu ndogo ya kuujenga msimu huu

Profesa wangu anasema "use something from last season but just a piece of the puzzle not the landscape of the picture" ni wazi kwa mechi ya leo Kocha anatazama kidogo cha msimu uliopita na kujenga picha yake ya msimu huu

Point ya tatu inasema "change what you can control" badili kile ambacho unaweza kukidhibiti, hapa kuna basics na fundamentals! Leo tumemuona Hitimana, hajakibadili sana kikosi, hajaweka sana vitu vipya, anashikilia basics kwanza, ndicho anaweza fanya kwasasa

Mwisho ni "keep concepts simple" mbinu zake lazima ziwe nyepesi ili wachezaji wamuelewe kirahisi sana, hii inasaidia wachezaji wasicheze kwa kufikiria sana na watacheza wakiwa na uhuru, kama leo kwenye transition Simba chini ya mstari ilisalia na mabeki wawili tu!

Profesa alimaliza kwa kuniambia, hii project imeanza upya, tegemea kuona ikipoteza au kushinda kwa mbinde, ndio mpira wa miguu na zama mpya zimeanza, muhimu alama tatu
Screenshot_20211028-042730_Instagram.jpg
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imetupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na Wakili wa utetezi, Fridolin Gwemelo katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita la kutaka cheti kilichowasilishwa Mahakamani na shahidi wa saba wa jamhuri ambaye ni ofisa Tehama wa benki kisipokelewe, taarifa kamili kwenye Youtube ya millardayo.
Screenshot_20211028-043008_Instagram.jpg
 
"Wizara iliwapatia zawadi mliporejea mkala chakula cha usiku pamoja na nakumbuka nami nikapiga simu, sasa leo nami nitawapatia zawadi kuna vijisenti vya mafuta vitapita kwa Wachezaji na Makocha wao, lakini Kuna Timu huko nyuma ilishinda walipewa viwanja wote lakini wanaoleta makombe (Twiga Stars ) hawakupewa sasa leo nitawapatia Watoto wangu wa Twiga Stars viwanja vya kujenga Dodoma, najua baadhi yenu itakuwa ngumu kujenga Dodoma lakini pokeeni viwanja kwanza"

"Nawapa viwanja kwasababu na nilisema siku ile maneno yangu yakaenda yakageuzwa, nilisema Vijana hawa wakicheza itafika wakati watachoka lazima tuwajengee future yao, tukiwapa viwanja wakafanikiwa kujenga huko mbele hawatopata shida na pa kukaa, akiwa nyumbani kwake hata Mtu akila ugali na ndimu ni kwake" ——— Rais Samia Ikulu Dar es salaam leo
Screenshot_20211028-043259_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom