Makapuku Forum

“Makusanyo Ki-Mikoa, Mkoa wa Njombe umeongoza kwa kukusanya asilimia 113 ikifuatiwa na Mkoa wa Geita 107%, Mkoa wa Songwe asilimia 107 na Mkoa wa Lindi umekua wa mwisho kwa kukusanya asilimia 78 ukifuatiwa na Mkoa wa Simiyu 81% na Mkoa wa Singida 82%”

“Matumizi katika Miradi ya Maendeleo Taarifa zinaonesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa imeongoza kwa kuchangia asilimia 192.3 ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru asilimia 166 na Halmashauri ya Wilaya ya Newala asilimia 155”

“Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imekua ya mwisho kwa kuchangia asilimia 25.47 ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe asilimia 28 na Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli asilimia 28”

“Uchambuzi wa ufanisi wa Halmashauri katuka ukusanyaji wa mapato ya ndani, unaonesha Halmashauri 57 zimekusanya kwa 100% au zaidi ya makisio yake ya mwaka,Halmashauri 90 zimekusanya kati ya 80% hadi 99 na Halmashauri 37 zimekusanya kati ya 50% hadi 70” ———-Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu Dodoma
Screenshot_20210730-052953_GBInsta.jpg
 
Mbunge wa Mlimba Mkoani Morogoro, Godwin Kunambi, amefanikisha ujenzi wa Daraja la muda la mbao katika Mto Mngeta wenye mamba ambalo kwa muda mrefu limekuwa likihatarisha maisha ya wananchi wa Kata ya Mngeta, Kunambi amesema ujenzi wa daraja hilo la muda umegharimu Tsh. Milioni 31.

Wananchi wa Kata ya Mngeta kwa muda mrefu wamekuwa wakipata changamoto ya kivuko katika Mto huo wenye Mamba ambapo mara kadhaa wamesababisha vifo vya Wananchi waliokuwa wakivuka Mto huo kwenda upande wa pili kufanya shughuli zao za kila siku.

"Fabruary mwaka huu nilikuja hapa kujionea changamoto hii ya kivuko na nikawaahidi kwamba hakuna Mwananchi mwingine ambaye ataliwa na Mamba Mimi nikiwa Mbunge wenu, imani mliyonipa mimi na Rais wetu Samia Suluhu Hassan ndio ambayo imelipa leo ambapo sasa tumekamilisha ujenzi wa daraja hili la muda lililogharimu kiasi cha TSh. Milioni 31”———KUNAMBI

“Lengo langu kama Mbunge wenu ni kuhakikisha tunapata Daraja la kudumu ili kuondoa kero hii lakini kwa hatua hii ya kuweka kivuko cha muda ninaimani kuwa kutachochea maendeleo ya Wananchi wetu na kuongeza usalama kwa watumiaji wanaopita hapa”———- Kunambi
Screenshot_20210730-054202_GBInsta.jpg
Screenshot_20210730-054223_GBInsta.jpg
 
Mahakama ya kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) leo imemaliza kulisikiliza kesi ya rufaa ya Club ya Yanga dhidi ya Bernard Morrison.

Mara baada ya kumalizika kusikilizwa kwa kesi hiyo ambayo Morrsion anatuhumiwa kujiunga na Simba SC huku akiwa na mkataba Yanga SC, CAS itatoa uamuzi kwa mujibu wa taratibu zake kati ya sasa mpaka 24/08/2021
Screenshot_20210730-054538_GBInsta.jpg
Screenshot_20210730-054602_GBInsta.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linamshikilia kijana aitwae Dickson Mungulu kwa tuhuma za kujiteka na kujiumiza sehemu ya shingo na mguuni kwa makusudi ili aishawishi familia yake wakiwemo Wazazi na Ndugu kumtumia shilingi milioni tatu ambayo aliandika sms ili ionekane Watekaji ndio wanaitaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo amesema baada ya kumuhoji Mtuhumiwa alisema alikuwa anafanya hivyo ili aweze kupata kiasi hicho cha fedha kiweze kumsaidia kwenye madeni yanayomsumbua.

"Polisi ilipokea taarifa kutoka kwa Mtu mmoja ambae jina lake tunalihifadhi akidai Ndugu yake aitwae Dickson mwenye umri wa miaka 26 ametekwa na wamezipata taarifa kupitia sms iliyotumwa kutoka kwenye simu ya Dickson kwamba watume shilingi milioni 3 vinginevyo atauwawa"

"Baada ya kupokea taarifa hizo Polisi walifanya uchunguzi kwa kina na tarehe 28 July majira ya jioni tulifanikiwa kumpata Kijana aliyesadikika kwamba ametekwa eneo la Mworombo Arusha akiwa kwenye nyumba ya kulala wageni ambayo jina tumelihifadhi"

"Dickson aliemaliza shahada ya elimu katika Chuo Kikuu cha Makumira Arusha mwaka 2020 ilibainika alidanganya kwa kujiteka ili apate hiyo pesa ikamsaidie kulipa madeni, Polisi wanaendelea na upelelezi na ukikamilika jalada litapelekwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali kwa ajili ya hatua za kisheria, natoa wito kwa Vijana wenye tabia kama iliyooneshwa na Dickson Polisi haitowafumbia macho wote wanaopotosha umma na kutoa taarifa za uzushi kwa jamii"
Screenshot_20210730-054805_GBInsta.jpg
 
Polisi Mkoani Rukwa wanawashikilia Watu watatu kwa tuhuma za kufukua kaburi ambalo aliyezikwa hajaweza kufahamika mara moja na kuchukua kukata kichwa cha marehemu, kukiweka kwenye sufuria na kisha kukitelekeza juu ya kichanja cha vyombo nje ya nyumba ya Mtu mwingine.

Polisi wamesema wenye nyumba walianza kusikia harufu kali na walipotoka nje walikuta kichwa hicho kwenye sufuria wakafikisha taarifa kwa uongozi wa kijiji na Polisi wakafahamishwa.

Kamanda wa Polisi Rukwa William Mwampagale amesema "hili tukio limetokea kwenye Wilaya ya Sumbawanga, kile ni kichwa cha binadamu, tumebaini kwamba kuna kaburi la binadamu limefukuliwa ndio hicho kichwa kikakatwa, fuvu hilo tumelirudisha na kulizika palepale kwenye kile kiwiliwili japo bado kaburi hilo halijajulikana ni la nani"
Screenshot_20210730-055832_GBInsta.jpg
 
Polisi Mkoani Kilimanjaro wanamtafuta Mwanaume mmoja aliyesababisha mauaji ya Mke wake kutokana na ugomvi ambao ulitokea baada ya Mke huyo aitwae Fausta Silayo (22) kukataa kurudiana nae.

Kamanda wa Polisi Kilimanjaro Simon Maigwa ameiambia Amplifaya ya CloudsFM kwamba "Majirani wamesema mgogoro ulitokea baina ya wawili hao na Mwanaume alikua akilazimisha warudiane, walikua wametengana kwa muda na Mwanamke akarudi kwa Wazazi wao, huyu Mwanaume alikwenda kwao kuona kama wanaweza kusuluhisha lakini ikaonekana kwa matendo ya yule Mwanaume isingewezekana hivyo kwa hasira Mwanaume ndio akaamua kumchoma visu Mke wake"

"Baada ya Mwanamke kupiga kelele Mwanaume akatorokea migombani na unajua Rombo ni mpakani mwa Kenya na Tanzania, ametorokea Kenya lakini tunaendelea kumsaka na tutamkamata kwasababu anafahamika, tunashirikiana na Interpol, Mwanamke alijeruhiwa lakini baadae akafariki"
Screenshot_20210730-060052_GBInsta.jpg
 
Kuna habari mpya huko Tunisia sasa hivi ambapo Rais wa Nchi hiyo Cais Saied amependekeza kuwa mamia ya Watu Matajiri wanaoshukiwa kwa ubadhirifu/ufisadi waingie makubaliano na Serikali ya Nchi hiyo na kisha wapeleka fedha zao kufadhili Hospitali za umma, Shule na miradi ya maendeleo katika maeneo maskini ili kuepuka kuhukumiwa kwenda Jela.

Rais Saied alikutana jana usiku na Mkuu wa Shirika la Waajiri nchini Tunisia, Samir Majoul na kupendekeza mpango huo usio wa kawaida kwa Wafanyabiashara maarufu 460 wanaoshukiwa kufuja mabilioni ya dola katika miaka ya kabla ya vuguvugu la mapinduzi ya umma la mwaka wa 2011.

Rais Saied alikamata madaraka mapya ya kisiasa wiki hii na anajaribu kupambana na rushwa na ukwepaji kodi matukio ambayo yameuathiri uchumi wa nchi hiyo, Majina ya wafanyabiashara hao yapo kwenye ripoti iliyotayarishwa na Tume ya uchunguzi iliyoundwa baada ya vuguvugu hilo lililomuondoa madarakani aliyekuwa kiongozi wa kimabavu Zine El Abidine Ben Ali mwaka wa 2011.
Screenshot_20210730-060739_GBInsta.jpg
 
Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo amekutana na Rais wa sasa wa Taifa hilo Alassane Ouattara ikiwa ni zaidi ya miaka kumi baada ya vurugu za uchaguzi zilizolizonga Taifa hilo la Afrika Magharibi.

Mkutano huo uliosubiriwa kwa kiwango kikubwa, unatajwa kuwa ni jaribio la kupunguza mvutano wa kisiasa, ambazo zimekuwepo nchini Ivory Coast tangu kufanyika mkutano wao wa mwisho kwa Viongozi hao zaidi ya muongo mmoja uliopita pale ambapo Ouattara alimshinda Gbagbo katika uchaguzi wa rais.

Baada ya mkutano wao, Ouattara alisema wameona ni muhimu kurejesha hali ya uaminifu baina yao "Tumeamua ni muhimu kujenga hali ya kujiamini na kutafuta njia ya maridhiano ya Waivorycoast, hili ndio jambo la msingi na kuaminiana kwa kila mmoja wetu, matukio yaliopita yalikua na machungu, kulikuwa na vifo vingi, lazima tuyasahau hayo na kutazama hatma, kwa mshikamano na mapatano."

Gbagbo kwa upande wake alisema angependa rais huyo awaachie huru wale waliokuwa wakimuunga mkono ambao kwa sasa wapo magerezani Nchini humo, Gbagbo amerejea Ivory Coast hivi karibuni baada ya Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa ICC, kuyatupilia mbali mashtaka yake ya uhalifu dhidi ya binaadamu ya vurugu za baada ya uchaguzi ambazo zilisababisha watu 3,000 kuuwawa.
Screenshot_20210730-064732_GBInsta.jpg
Screenshot_20210730-064754_GBInsta.jpg
 
Mtangazaji hodari wa Tanzania Salim Kikeke amepanda Mlima Kilimanjaro na kufanikiwa kufika hadi kileleni.

Siku kadhaa zilizopita alisema———“Nimeona nipande Mlima kwasababu nikiwa kwenye Safari zangu Duniani kote nikiwaambia natoka Tanzania wananiuliza umewahi kupanda Mlima Kilimanjaro mara ngapi”

“Ni muhimu mambo kama haya kuyafanya mfano Mimi ninapopanda Mlima ninapouelezea nakuwa najua nazungumzia kitu gani”
Screenshot_20210730-132552_GBInsta.jpg
Screenshot_20210730-132612_GBInsta.jpg
Screenshot_20210730-132639_GBInsta.jpg
Screenshot_20210730-132657_GBInsta.jpg
Screenshot_20210730-132718_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom