Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 152,998
- 453,891
Dereva wa Bodaboda Rogers John Kesi (17) mkoani Kilimanjaro ameuwawa na Abiria aliemkodisha kwa ajili ya kumpeleka nyumbani kwake, RPC Amon Kakwale amethibitisha.
“Ilikua ni May 10 2021 saa kumi na mbili alfajiri Polisi tulipata taarifa za kuuwawa kwake, alikodiwa kituoni Kiborloni na Mteja kumpeleka kwenda nyumbani kwake Mnazi Shani Tours, baada ya kufika Abiria ambae ni Mtuhumiwa aliingia na Rogers nyumbani ili kumuonesha mzigo wa kuubeba”
“Wakati Rogers akiwa kwenye harakati za kuuchukua mzigo huo ambao ni meza, Abiria ambae ndiye Mtuhumiwa aitwae Sifaeli maarufu Godson (21) Mmasai alimtokea kwa nyuma na kumpiga nyundo kichwani kwake na Marehemu akadondoka chini”
“Baadae Sifaeli alichukua waya na kumnyonga nao na alipohakikisha kwamba Rogers amekata roho alimpigia simu Rafiki yake wakashirikiana kuubeba mwili na kuuweka kwenye mifuko ya sandarusi, wakauweka kwenye pikipiki hiyohiyo na kwenda kutelekeza kandokando ya barabara kuu ya Moshi -Himo” ——— RPC Kakwale.