Makapuku Forum

...This is Simba, wafuga kambale walianza mafunzo ya kuhesabu kiarabu wakijua Mnyama atafungwa sasa imebidi wasande, kila ukikutana na mtani heshima nyingi sasa.

kapuku burudika na kama hukuwa unajua Simba imefanya mauaji makubwa sana kuwahi kutokea katika karne ya 21. Nitawaletea picha sema kamera imeibiwa

 
Habari wana JF
Uzi huu ni kwaajili ya makapuku wote. Lengo ni kujadili changamoto zinazotukabili, pia Kupeana support katika mambo yetu hapa JF. Tupeane mbinu za kukabiliana na mambo yote humu.

Th Name JF Makapuku assistant Founder

Salute kwenu wakuu,
Lengo la huu uzi linatimia? Maana nimeperuzi kwa bidii ila sijaona majadiliano kuhusu challenges rather than greetings.

Please take it positively, sina maana hasi..
 
Salute kwenu wakuu,
Lengo la huu uzi linatimia? Maana nimeperuzi kwa bidii ila sijaona majadiliano kuhusu challenges rather than greetings.

Please take it positively, sina maana hasi..

...hii perusal umeifanya kwa muda gani? Ninachojua mimi, challenges zinaongelewa sana in a light way, sio kama Jukwaa la Siasa au GT. Hapa ni issue in a light touch maana maisha sio lazima yawe 'magumu'. wengi humu tunajadili masuala kiurahisi rahisi, na yapo mengi sana yanajadiliwa labda kama uliishia kufocus kwenye greetings peke yake.

Mfano mdogo tu, kuna ishu za korosho, ada na mipango ya kukamilisha mwanzo wa mwaka, hizi zilikuwa topical issue kwa 2019 kutaja machache.

Anyway, yapo majukwaa mengi na umefanya vema kunukuu post ya Bailly5 , ukiniuliza mimi, lengo limefikiwa na nimefaidika kisaikolojia na kiuchumi, na kijamii. Not on a defensive side, asante kwa kutembelea hapa na nitakuuliza tu kama Una Jipya?

Vinginevyo post yangu inayofuata ni kukuburudisha na muziki
 
Jamaa mmoja alikuwa amekaa zake sebuleni anasoma gazeti ghafla akapigwa frampen usoni na mkewe😂😂 JAMAA: vp tena mke wangu kulikoni😳😳 MKE: kwenye suruali yako wakati najiandaa kuifua nimekuta kikaratasi kimeandikwa "JENNY", unaweza kunieleza huyo JENNY ni nani kwako😬😬 JAMAA: aaah! wiki ilopita nilikuwa kwenye mashndano ya farasi, na Jenny ndo jina alobandikwa farasi wangu yaani farasi wangu aliitwa JENNY😌😌 MKE: sorry darling!👏🏼👏🏼 Siku iliofuata jamaa akiwa amekaa tena kochini huku akisoma gazeti, alishtukia amepigwa tena frampen ya uso "kwaang!" JAMAA: Uwiiiiiii! jamani mke wangu nini tena😪😪😳😳 MKE: farasi wako anakupigia simu😬😬😬
 
*Mwalimu mmoja aliita wanafunzi wake akawaambia''Kesho kila mwanafunzi aje na nyanya kulingana na idadi ya watu anaowachukia, Yaani kama unamchukia mtu mmoja uje na nyanya moja kama ni wawili basi njoo na nyanya mbili vilevile.* *Nyanya hizo mtazibeba kwenye mabegi yenu ya kubebea madaftari na vitu vingine vya shule* *"Wanafunzi wakakubali halafu kesho yake wanafunzi wakazibeba zile nyanya vizuri kabisa wengine walibeba moja,wengine mbili na wengine nyingi sana.* *Kama mwalimu alivyosema zile nyanya zikapewa majina ya watu ambao wanafunzi wanawachukia*. *Baada ya kuzipa hizo nyanya majina mwalimu* *akawaambia kila mwanafunzi azirudishie nyanya zake kwenye begi lake halafu aziache humo humo ndani ya begi kila siku awe anakuja nazo shuleni na kurudi nazo nyumbani.* *Baada ya siku kadhaa wanafunzi wakaanza kulalamika hasa wale waliobeba nyanya nyingi kuwa nyanya ni nzito sana na zinatoa harufu mbaya na zinaharibu vitu vyao vizuri walivyoweka kwenye mabegi yao* *Mwalimu akawaambia hivi ndivyo ilivyo mtu unapoweka watu usiowapenda moyoni* *kama mtu huwezi kuvumilia kukaa na harufu ya nyanya* *kwenye begi vipi kuhusu madhara ambayo moyo wako unayapata kwa kuubebesha mzigo wa chuki dhidi ya watu.?* *Moyo unapata madhara makubwa sana unapobebeshwa chuki kila wakati kila siku moyo unakuwa na chuki na hapo ndipo unaharibika* *na kusababisha kuharibu hata vitu vingine vizuri vilivyokoko moyoni mwako. Moyo ni kama lile begi la kubebea madaftari unahitaji kubeba vitu vizuri na visivyo na chuki ndani yake* *Safisha moyo kwa kusamehe wanaokukosea, jifunze kusamehe maana ni moja ya virutubisho vya moyo wako,Samehe kwa kila anayekukosea na kukukwaza.*
 
Hata kama hunipendi wewe ni mtu tu... ☹ Makampuni makubwa yananipenda hata kama sina hela vodacom, Airtel, Tigo wananiita mpendwaa😁😁😁 utaskia _Mpendwa mteja huna salio la kutosha_*🤣
 
FAHAMU: Hii nyumba ipo wilayani Mkinga(Tanga) ambapo inaleta utata wa kidiplomasia. Chumba kimoja kipo Kenya na chumba kingine kipo Tanzania (aliposimama NW Dkt. Damas Ndumbaro). Mwenye nyumba akitaka kula mirungi anakaa nje ya nyumba upande wa Kenya na askari wa Tanzania hawamfanyi kitu.
50759431_1120568488115705_1798284203002039341_n.jpg
 
Happy Valentines's day wadau wote wa Jukwaa hili. Upendo wangu kwenu ni sababu wewe ni mtu unayelifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kuwepo.

Furahia kama una nafasi na kama huna basi buruika maana it is almost furahiday

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom