Makao makuu ya wilaya huchaguliwa au kupangwa na nani?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makao makuu ya wilaya huchaguliwa au kupangwa na nani??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by DMussa, Jan 29, 2008.

 1. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wana JF mimi natatizwa na suala zima la uteuzi wa makao makuu ya wilaya. Kuna wilaya moja mpya ya Rorya ambayo iko mkoa wa Mara tatizo ni kwamba kuna mabishano na upinzani mkubwa juu ya eneo lipi liwe ndio makao makuu ya hiyo wilaya. Suali langu kubwa hapa ni kwamba nani haswa ndio mhusika mkuu katika kuteua/kuchagua au kuamua eneo kuwa makao makuu ya wilaya? Naomba ufafanuzi katika hili wananchi wenzangu maana huu uteuzi/uchaguzi naskia umeanza kuchukua sura ya RUSHWA......
   
 2. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2008
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,219
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Wenye dhamana ya kuchagua makao makuu ya wilaya ni wananchi wenye wilaya husika, kupitia kwa wawakilishi wao ambao ni madiwani. Sidhani kama serikali kuu ina maamuzi katika hili. Baraza la madiwani nadhani ndio wanaohusika na kuamua mahali ambapo kutakuwa na makao makuu ya wilaya, kwa kuangalia idadi ya watu katika eneo husika, ukaribu wa kusambaza huduma kwa tarafa na kata zote za wilaya husika (kwamba angalau makao makuu yawe katikati ya wilaya, kama inawezekana). Huwa kunatokea mara nyingi kwamba wanasiasa (hasa wabunge) hutaka kulazimisha makao makuu yawe mahali fulani, kwa matakwa yao, bila kuangalia vigezo vya kuweka makao makuu mahali fulani.
  Hili suala la Rorya kule Mara linashabihiana kabisa vurugu zilizotokea mkoani Iringa ambapo kulikuwa na mgawanyiko wa wananchi na viongozi wao kuhusu makao makuu ya wilaya mpya ya Kilolo, ambayo ilimegwa kutoka wilaya ya Iringa Vijijini!
   
Loading...