Makao makuu ya Bima kupigwa Mnada!

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,772
8,955
Wanabodi,
ktk tembelea yangu kwa Michuzi nimekuta habari hii mpyaa ambayo imeniacha hoi!..
Inasemekana kuwa jengo hilo ambalo lipo kona ya mtaa wa Pamba na samora liko mbioni kupigwa mnada ili kufidia malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi wake toka mwaka 1997.
Jumla ya fedha zinazodaiwa ni Tsh billioni 3 = Usd 3/m. Fedha ambazo leo hii huwezi kwa bei za mtaani huwezi kujenga wa jengo kama hilo labda hata kununua kiwanja ktk maeneo hayo. What's going on?
Je, hilo shirika linaweza fanya kazi bila jengo ama ndio mufsilis... na kwa nini kampuni hiyo isi file voluntary petitions for relief kiasi kwamba wapate muda wa kuweza kulipa madeni hayo badala ya hukumu ya moja kwa moja kuua shirika hili.

Mwisho, nashindwa kabisa kuelewa kwa nini wakati wa utawala wa Mkapa wafanyakazi wengi wa mashirika ya Umma na wizara zake walikuwa hawapewi mishahara yao, toka walimu, madaktari, wizara na idara zake, manispaa na kadhalika kiasi kwamba madeni haya yamekuwa sababu ya kuzaa fitna.
Kwa habari zaidi soma:- http://www.issamichuzi.blogspot.com/
 
Mzee Mkandara, heshima yako Mzee

Nakumbuka mwaka jana wafanyakazi wa Shirika la Bima waliiomba tume ya kubinafsisha mashirika ya Umma "PSRC" kupeleka zabinu za kununua hilo shirika Bungeni ili zichambuliwe kwa uwazi. Kipindi hicho ilisemekana kuwa kampuni ya Heritage All Insurance Limited ndio ilikuwa imeshinda zabuni ya kufanya biashara ya Bima ya maisha kwa gharama ya shilingi bilioni tatu. Wafanyakazi walihisi kuchezewa faulu na wakaamua kuanzisha libeneke. Sijuhi kindumbwendumbwe chao kiliishia wapi.

Anyway, biashara ya Bima katika nchi yetu ni makubaliano ya imani kati ya mkata Bima na Shirika la Bima. Imani yenyewe inawekwa katika mkataba kuwa Shirika la Bima litamlipa mkata bima (Policyholder) pindi bima yake itakapoiva (at maturity). Bima ambayo ningependa kuizungumzia hapa ni ile ya maisha (Life insurance), ambayo ndio kwa kiasi kikubwa inafanywa na shirika letu la taifa la Bima.

Zamani Mashirika ya Umma na hata yale ya binafsi hayakuwa na namna bora ya kuwekeza pesa kama ilivyo sasa ambapo kuna “Stock markets”. Zamani fedha za policyholders (wakata Bima), kama ilivyokuwa kwa wateja wa NSSF na PPF, zilikuwa zinawekezwa katika real estate.

Shirika letu la taifa la Bima lilikuwa linaendesha biashara katika namna ambayo ambayo kuna wateja wapya wanaingia na wale wa zamani wanaendelea kulipwa kadri bima zao zinavyoiva (mature). Ili kuweza kuendelea kukidhi mahitaji ya kulipa bima zinazoiva from time to time, Shirika la Bima lililazimika kuwa na income stream fulani. Hivyo basi, majengo makubwa ya Shirika la Bima la Taifa yalijengwa na fedha za policyholders wa zamani, kwa hiyo si mali ya Serikali wala ya Shirika la Bima bali ni mali ya policy holders.

Kinachotokea ni kuwa yale majengo yanapangishwa kwa wateja na income stream inayotokana na rental charges ndiyo inayotumika kuthamanisha au kumatch madai ya bima zilizoiva na assets zilizopo kuwalipa hao policyholders wenye mature claims. Hivyo kimsingi majengo kama kitegauchumi (kama jina lake lilivyo), Mikocheni Flats, Jakaranda Arusha, NIC Mbeya, Diplomatic Flats Dar, Life House Dar, na mengine mengi, yote yalikuwa ni source of income kwa ajili ya kuwalipa policyholders na si mali inayouzwa wakati wa ubinafsishaji au kwa lengo la kufidia wafanyakazi.

Kwa mfano, kitu ambacho kingetokea katika ubinafsishaji (kama lingebinafsishwa) ni kuwa ambaye angeuziwa Shirika angepewa mikataba ya Bima (ambayo ni madai) na mali (zinazotoa rental income streams) zinazoambatana na thamani ya madai husika zinahamishiwa kwa mwekezaji mpya ambaye si "Estate Manager" bali ni mtaalam wa biashara ya bima. Bila shaka, hii ndio sababu iliyolifanya Shirika la Bima lidode bila kubinafsishwa kwa muda mrefu. Amini usiamini, kama haya majengo yasingekuwa yanamilikiwa na wakata Bima, basi viongozi wangekwisha changamkia tenda zamani kama walivyofanya kwa NBC na mashirika mengine.

Kitambo kulikuwepo na vuguvugu la kujaribu kuishawishi Serikali kuwa Shirika la Bima wangeachiwa wafanyakazi, kwamba Serikali iwatafutie mtaji waliendeshe Shirika kwa kuwa ni wazalendo. Pia zilikuwepo tetesi kama hizi za kutaka kuliuza jengo la Kitega Uchumi na majengo mengine yaliyopo mjini kwa vigogo fulani!!!. Ukweli ni kuwa jengo kama Life House lilijengwa na fedha za policyholders wa Bima ya maisha, ni mali yao. Kitega Uchumi lilijengwa na non-life policyholders, n.k. hivyo majengo hayo si ya Serikali bali ni ya policyholders. Sasa kama kuna tetesi za kuanza kuuza majengo, tafsiri yake ni kuwa biashara ya bima iwe liquidated ili atakapomaliza kulipwa mdai (claimant) wa mwisho, jengo liuzwe na bima husika iwe imekufa!!!

Bahati mbaya hali ya Shirika ni mbaya sana. Linashindwa kukidhi minimum regulatory requirements kwa maana ya capital base, licence and ability to settle claims within legally provided timeframe. Its management costs kwa sasa zina-account for more than 82% of the total operational costs!!! Shirika lilikuwa na net-equity of negative six billion na total required capital kuliwezesha walau lifikie kubalance vitabu vyake bila kuwa na hasara au faida ni karibu TShs. 70 billion (around 70 million USD).
 
HII NCHI PASUA KICHWA, SASA KWA WALE AMBAO BIMA ZAO ZIMEIVA KITAMBO NA BADO WANAZUNGUSHWA NINI ITAKUA HATIMA YAO.
KINGA IMEKUA MTAJI NA KILIO KWA WATU.
BIMA NI JANGA LINGINE LA TAIFA.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom