Uchaguzi 2020 Makao Makuu ya ACT-Wazalendo yazingirwa na Polisi, watu watatu Wakamatwa. Wanyimwa dhamana

mkalamo

JF-Expert Member
Sep 7, 2013
324
347
Muda huu watu waliojitambulisha kuwa ni maafisa wa jeshi la Polisi kutoka makao makuu, wamezingira ofisi ndogo ya makao makuu ya Chama cha ACT-Wazalendo yaliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam kwa minajili ya kumkamata afisa wa Chama hicho Dotto Rangimoto, anayehusika na usambazaji wa Taarifa za Chama katika mitandao ya kijamii.

Awali maafisa hao walitaka kumchukua Rangimoto bila ya kuonyesha vitambulisho vyao hali iliyozua tafrani ya maneno baina yao na watu waliotaka wajitambulishe.

Mpaka sasa maafisa hao hawajaeleza ni makosa gani wanamuhusisha nayo, huku wakihimiza kutaka kukagua ofisi nzima ya chama hicho kwa madai ya kutafuta simu inayotumiwa na Rangimoto katika mitandao ya kijamii.

Hata hivyo maafisa hao wameshindwa kuonyesha kibali cha ukaguzi na kwa sasa wamewapigia wenzao kwa ajili ya kuongeza nguvu katika eneo hilo.

UPDATES;

=====

Arodia Peter, Afisa Habari.. Dotto Rangimoto Kijana afisa msaidizi kitengo cha habari na Afisa kampeni kimataifa, Dahlia Majid, Wamechukuliwa na Polisi. Dotto anashikiliwa kwa Makosa ya Kimtandao

UPDATES 26/09/2020
IMG-20200926-WA0024.jpg
IMG-20200926-WA0025.jpg
 
Huu ni uhuni na unyanyasaji tu. kwani hao polisi kule Arusha walimtorosha aliyekuwa mkuu wa mkoa Mrisho Ghambo alipokuwa anakamatwa na takukuru kwa kutoa rushwa wakati wa kinyanganjiro cha kura za maoni ili kupata mgombea ubunge.

Kitendo hicho kilimfanya atumbuliwe yeye pamoja na mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa wilaya. Pia kitendo hicho kilifanya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha kuhamishiwa ccp moshi.

Mtoa rushwa huyo - Ghambo pamoja na makosa yote hayo, huyo ndiyealiyepitishwa na ccm kugombea ubunge wa Arusha mjini.
 
Na anayetafutwaa au na wanaomtafuta anayeshukiwa kufanya uharifu?

Jiulize, Kwa nini hujatafutwa wewe?

Penda Amani uishi Kwa hiyo Amani

Hivi kupenda amani ni kutokumweka bwana yule mkao wa kurejea kwao kwa mujibu wa sheria?

Ni wazi kuwa kwa sababu hawa wako mstari wa mbele kwenye kumrejesha bwana yule kwao kwa mujibu wa sheria basi hawataki amani, hivyo wanastahili kusumbuliwa sumbuliwa hivi.

Oct. 28 si mbali. Tofauti ya wapenda haki na majahili ni kuwa, hakutalipizwa kisasi.
 
Makao makuu ya ACT yamehama toka Kijitonyama kwenda Magomeni??
 
Back
Top Bottom