Makanisa ya Pentecoste yanaogopa nini kukaguliwa? Mzee wa upako hiyo ni sheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makanisa ya Pentecoste yanaogopa nini kukaguliwa? Mzee wa upako hiyo ni sheria

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, May 13, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,605
  Likes Received: 5,780
  Trophy Points: 280
  PASTOR LUSEKELO
  KUKAGULIWA NI MOJA YA SHERIA WALA SIO UADUI;;KAMA HIVYO BASI NA SERIKALI MSIRUHUSU KANISA KUPITISHA VITU OVYO BANDARINI BILA KULIPIA WAKATI AWATAKI KUKAGULIWA
  JE NINI KINACHOWAOGOPESHA KUKAGULIWA??

  KIONGOZI wa Kanisa la Maombezi la GRG la Ubungo Kibangu, Dar es Salaam, Anthony Lusekelo amesema kauli ya baadhi ya makanisa ya Pentekoste kupinga kukaguliwa imetolewa kwa nia njema na si kwamba wanatafuta uadui na Serikali.

  Alikuwa anazungumzia kauli ya Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa la Kipentekoste Tanzania (PCT), Dk. David Mwasota, ambaye alipingana na msimamo wa baadhi ya makanisa ya kutotaka kukaguliwa kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

  Lusekelo kwenye maoni yake, alisema kwanza yeye licha ya kuwa ni Mpentekoste, lakini si mwanachama wa PCT hivyo akasisitiza kuwa Dk. Mwasota hana mamlaka ya kuyasemea makanisa ambayo si wanachama wake.

  “Sijawahi kuwa mwanachama wa PCT na sina mpango wa kuwa mwanachama wa umoja huo, hivyo Dk. Mwasota hana mamlaka ya kutusemea sisi,” alisema Mchungaji Lusekelo.

  Pia alisema kitendo cha baadhi ya wachungaji kutoa maoni kuhusu baadhi ya sheria wanazoona kuwa ni kandamizi sio dhambi kwani sasa hivi Tanzania inajiandaa kupata Katiba mpya, hivyo kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni sehemu anayoona kuwa ina mushkeli.

  “Hili la kupinga kukaguliwa ni msimamo wetu na tutalitetea kwenye Katiba mpya. Kufanya hivyo sio uadui dhidi ya Serikali ila ni kuwaandaa watu hasa waumini wa makanisa hayo kushiriki katika mjadala huo,” alisema Mchungaji Lusekelo.

  Alisema kitendo cha makanisa au misikiti kusajiliwa pamoja na vyama vya kijamii ni udhalilishaji hivyo akasema kwamba ndio maana wao wameona kuwa kuna haja ya kupiga kelele ili sheria hiyo irekebishwe.

  “Makanisa au misikiti ni taasisi muhimu huwezi kuzilinganisha na vyama vya kijamii, sasa kwa nini zisajiliwe kwa pamoja?” Alihoji Mchungaji huyo.

  Lakini pia Mchungaji huyo alisema makanisa mengi yameshindwa kujiunga na PCT kutokana na udhaifu wa Dk. Mwasota katika masuala ya uongozi.

  Alimtuhumu Dk. Mwasota kuwa anajipendekeza kwa Serikali kutokana na makosa yake mengi aliyoyatenda ikiwemo kuwa mlezi wa DECI, taasisi ya upatu ambayo baadaye ilisitishwa shughuli zake na Serikali.

  Pia alimtuhumu kiongozi huyo wa PCT kuwa anatumiwa na baadhi ya watu wenye lengo la kumchafua yeye Mchungaji Lusekelo.

  Katika toleo la jana la gazeti hili, Dk. Mwasota amenukuliwa akisema kuwa msimamo uliotangazwa na Lusekelo sio msimamo wa PCT kwani haujawahi kujadiliwa kwenye Baraza hilo.

  Akizungumzia madai ya Lusekelo, Dk. Mwasota alisema jana kwa simu kuwa si kweli kwamba ana uhusiano wowote na DECI kwani wamiliki wake wanaeleweka kuanzia serikalini hata mahakamani.

  “Unajua Mchungaji huyu (Lusekelo) labda ana matatizo yake, lakini wamiliki na wahusika wa DECI wanafahamika kuanzia serikalini, mahakamani hata kwa wale waliokuwa wanachama wake. Hiyo ni njia tu ya kutokubali kile alichokosea,” alisema Dk. Mwasota.

  Kuhusu kutojiunga kwa Mchungaji Lusekelo PCT, alisema hiyo ni hiari yake ingawa haifahamiki kama ana sifa za kuwa mwanachama wa umoja huu unaotambulika na Serikali katika kuunganisha makanisa ya Kipentekoste na sababu zake anazotoa hazina msingi.
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Wanaogopa kulipa kodi, bila kodi tutaendeleaje? Makanisa na misikiti wanapata mapato
  makubwa sana ya sadaka na miradi sasa wanataka wajinemeshe wao huku wakiipigia kelele serikali
  kujenga barabara na miundo mbinu mingineyo wkt hawachangii kodi, shame on them.

  Serikali ingekuwa makini watu kama rwakatare,mzee wa ATN,Mwingira,kakobe na wengineo
  wanapaswa kulipa kodi kulingana na mapato yao kwa mwezi TRA wangepata pato kubwa
  ingewezesha hata mishahara yetu kuongezeka na pia huduma zingine zingeboreshwa.

  Nasema hivi kukaguliwa lazima wapende wasipende wanaogopa nini au hawataki tujue wana
  hammer, mashamba makubwa na wengine wana mpango wa kununua private jet?

  Tunapaswa kujua hizo hela wanapata wapi? Miradi ipi nk manake wengine tunajua wanauza
  hata madawa ya kulevya kwa kivuli cha dini huku wakijipamba na vito vya dhahabu.

  Unafiki mtupu, Yesu alivaa kanzu moja wao wanajilimbikizia afu watu na akili zao wanawahusudu.:dance:
   
 3. f

  fikiriakwanza Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijawaelewa hawa wanaotaka usajili wa madhehebu uwe tofauti na vikundi vingine vya kijamii,kwani kuna tofauti gani kati ya kikundi hicho cha kijamii na dhehebu???Naomba ufafanuzi na kwa nini watake wasikaguliwe????Hiyo ni hoja nyepesi,Dk.Mwasota ,fanya kazi uliyopewa na Bwana Yesu,Lusekelo hali kadhalika haya mengine ni porojo tu.Kitu cha Mungu watu wenyewe watatafuta namna ya kufanya.Mfano mzuri ni Babu wa Loliondo,hakuwaomba usajili wa dawa ua nini watu wenyewe wamefuata na serikali ikaingilia kuwasaidia watu wake.Kwani serikali haimtaki Mungu??nani mjinga asiyemtaka Mungu??watu wanakwenda pale wanapopata msaada.
   
Loading...