Makanisa holela yanaua watu kila siku, Mwamposa ni robo tu ya visa, Makelele ya makanisa uchwara Serikali imenyamaza watu wanakufa kwa presha

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,276
21,394
Kuna namna nyingi za kuuwa watu?

Kilichotokea kwa Mwamposa ni moja tu kati ya matukio hatarishi yanayofanywa na makanisa!

Kuna matukio mengi sana ya kijinga yanafanyika waziwazi na serikali ipo kimya!

Makanisa holela mengi yamefungwa spika zinazozalisha makerere mtaani Serikali ipo kimya kwa sababu haijaona madhara yake waziwazi kama vifo vya Mwamposa!
Wagonjwa wengi wa presha wanapatwa na mishituko kutokana na makelele hayo lakini serikali ipo kimya.

Wamama wajawazito wanazaa watoto vilema kwa sababu ya makelele!

Watu na watoto wengi wanakumbwa na tatizo la Usikio hafifu (ngoma ya sikio inaharibika) kwa sababu ya makelele
Makazi yamekuwa si salama majumbani watu hawasikilizani kwwasababu jilani kuna kanisa linapiga kelele.
Kuna mitaa ina makelele kiasi hata mtu akipigiwa simu hawawezi kusikilizana

Makanisa haya yamekuwa hayana tofauti na michezo ya kubet, watu wanachaniwa mikeka yao kwa kutarajia miujiza
Watu wanauza kila mali waliyonayo kwa agizo la wachungaji ili kujenga kanisa wabarikiwe

Kiufupi makanisa yanauwa watu kisaikolojia, kifikra na kimwili

Kilichotokea kwa mwamposa ni mauaji ya kimwili

Sababu kubwa ya yote kutokea ni uzembe wa serikali kusimamia sheria!

Makelele ya makanisa ni tishio kama la nzige; serikali inakwama wapi?
 
Bahati mbaya sana hata makanisa uchwara ni mengi na yanaota kila siku. Kuna kero kubwa ya kelele nadhani sisi wenyewe tukomae nao waache kelele
 
Bahati mbaya sana hata makanisa uchwara ni mengi na yanaota kila siku.Kuna kero kubwa ya kelele nadhani sisi wenyewe tukomae nao waache kelele
Tufanye nini! Kama njia ya maridhiano imeshindikana unatushauri tuyachome au?
 
Hili la mikelele ni suala mtambuka. Kuna nyumba za Ibada nyingi sana nazo zinapigia kelele watu kuanzia saa kumi alfajiri. Serikali sio kwamba haioni bali imeamua kutumia busara na kuwaacha wote waendelee. Ni kuvumiliana tu.
 
Hawa ni matapeli na wezi wakubwa hapa Tanzania, ni bahati mbaya serikali hailioni hili.
Bahati nzuri hawamforce mtu kutoa mpunga wake. As long as wanakuconvince kwa maneno na wewe unatoa pesa, Serikali haiwezi kupoteza muda kudeal na watu wanaotenda hayo kwa ridhaa zao wenyewe. Na ikumbukwe kwamba mtu aliyetapeliwa ana haki ya kwenda kushitaki police
 
Niliposoma mstari unasema "Watu wanauza kila mali waliyonayo kwa agizo la wachungaji ili kujenga kanisa wabarikiwe" ninegundua una agenda binafsi nje ya hoja husika ya kelele zinazoletwa na makanisa hayo na madhara kwa watu wanaokaa jirani!
 
Kanisa ni moja tu takatifu katoliki la mitume hayo mengine yote unayoyasikia ni makanisa uchwara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwakuwa wewe ni mkatoriki? USIITE MAKANISA MENGINE UCHWARA. Mimi si mkristo ila siwezi tukana au kudharau watu wa imani nyingine. Tukio limekwisha tokea muhimu ni kujifunza kutokana na makosa.

Mbona hata Catholic wanamatukio mengi ya uasi ya siri na dhahiri? Muhimu fuata Biblia inasemaje.
Kwamujibu wa biblia yenu imani ndio itakayo kupeleka mbinguni.
 
Kama Mchungaji anasimama na kuongea upuuzi eti Mbunge wa Wananchj auwawe unategemea nini Kanisani kwake.
Watawatoa sana Kafara waumini wasiojielewa.
 
Mnahangaika na Mwamposa alieua 20 tena bila kutumia mkono wake, tunasema tu kaua, kaua, hivi tunafahamu Bashite yeye kaua wangapi kwa kutumia mikono yake halisi kama ambavyo wamarekani wamesema wana ushahidi, tuhangaike na muuaji wa kweli, active killer, the man Bashite himself, achaneni na huyo passive killer, Mwamposa.

Tutaangamia sana kwa kukosa maarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili la mikelele ni suala mtambuka. Kuna nyumba za Ibada nyingi sana nazo zinapigia kelele watu kuanzia saa kumi alfajiri. Serikali sio kwamba haioni bali imeamua kutumia busara na kuwaacha wote waendelee. Ni kuvumiliana tu.
Hiyo siyo busara! Hata mwamposa alimwaga mafuta kwa busara kila mtu ajikanyagie
 
Mnahangaika na Mwamposa alieua 20 tena bila kutumia mkono wake, tunasema tu kaua, kaua, hivi tunafahamu Bashite yeye kaua wangapi kwa kutumia mikono yake halisi kama ambavyo wamarekani wamesema wana ushahidi, tuhangaike na muuaji wa kweli, active killer, the man Bashite himself, achaneni na huyo passive killer, Mwamposa.

Tutaangamia sana kwa kukosa maarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bashite kanisa lake linaitwaje
 
Kama wasimamizi wa hizo sheria ndiyo hao wazee wa hayo makanisa (vibanda miujiza) na wadhamini wenyewe, unatarajia nini zaidi, hayo unayolalamikia?
 
Kama wasimamizi wa hizo sheria ndiyo hao wazee wa hayo makanisa (vibanda miujiza) na wadhamini wenyewe, unatarajia nini zaidi, hayo unayolalamikia?
Basi kama ni hivyo mwamposa asilaumiwe kwa yaliyotokea
 
Back
Top Bottom