Makande na Bajeti za Mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makande na Bajeti za Mjini

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Adrian Stepp, Feb 19, 2012.

 1. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #1
  Feb 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  jamani ee!

  HIli swala la kuvamiwa na wageni bila taarifa linakera na kuudhi hasa unapokua na mipangilio ya bajeti zako..Huwezi kuwakufuka.. sometimes umejikalia wewe na familia yako jumamosi weekend mmenua kikilo chenu cha nyama na mboga ya majani na maharage nusu..

  Ghafla wageni wana wavamia mida ya saatano na hawatoki mbaka wale..wakila pale ujue bajeti ya jioni imevurugika lazima mboga ziongezwe..

  Sipendi, kweli mtu anakuvamia na watoto wake kafungasha na mkewe na mtoto wa wifi yake..

  SASA..

  Nika piga plan ya kusimplify mambo hapa mjini nikaamua kwamba! kila weekend especially Jumapili ni mwendo wa kande tu..kwanza na minimize cost

  ntanunua..Maharage nusu
  Njugu Nusu
  Karanga Nusu
  Mahindi Nusu na Nazi mbili na Mchicha fungu 5...
  Msosi simple but very smart..Hutaki Acha!

  Msosi safi kabisa asie kula aache akale kwake..wageni wanakuja hata matunda hambebi af mnakuja kama delegation..

  Mjini hapa kuharibiana budget inahusu?
   
 2. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Aaah! Tbag noma mkuu!
   
 3. s

  shosti JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  huo mkaa sasa wa kuivisha hizo kande..labda kama wapikia maranda au vifuu
   
 4. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Na kweli..

  Bora muwe mmeahidiana kuwa atakuja na familia yake yote,na kuwa watakuja kushinda kwako..

  Hata kama mkiwa mmeahidiana,bado mgeni(kiuungwana/kistaarabu?) anawajibika kubeba chochote(matunda...soda labda) ili kipokelewe na mwenyeji kama mchango wa kufanikisha au kuboresha ziara hiyo..
   
 5. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Au yale makaa ya makaratasi(ndiyo maranda hayo?),very cheap technology..
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  Feb 19, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kumbe wengi mnahusudu bajeti za kipare! Big up sana
   
 7. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Napenda sana kande,kwako wapi?
   
 8. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #8
  Feb 19, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Niliishi na Wapare,siwezi kusahau mapishi yao...
   
 9. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #9
  Feb 19, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  umenikumbusha jana wife kapika kitu cha mahindi mabichi njugu karanga njegere haragwe naz na kachumbar pemben kwa kwel wabena kwa kande kashnda nazo toka jana mpk leo mi nimekimbilia bar ila n bonge la menu protin hapo mech yake.
   
 10. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #10
  Feb 19, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ikitokea wasipokutembelea hao wageni utayapeleka wapi hayo makande?...lol
   
 11. Binti Magufuli

  Binti Magufuli JF-Expert Member

  #11
  Feb 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 7,460
  Likes Received: 766
  Trophy Points: 280
  Uchoyo tu umekuzidi...! wageni wa mara moja kwa mwezi wanakutoa nyongo?? acha hzo hujui Ibrahim alikaribisha malaika bila kujua na ndo chanzo cha kupata mbaraka wa kuzaliwa kwa Isaka? Hata hicho ulichopata ukanunulia nyama hujui ni Mungu alikupa?? Watu wanaacha shuhuli zao kukutembelea coz wanakuthamini alafu unalalamikia chakula........

  shauri yako uchoyo huo utakuzibia mibaraka
   
 12. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #12
  Feb 19, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ila inabidi kuangalia,usiwe na karoho ka uchoyo uchoyo.. Mrembo by N may have a point...
   
 13. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #13
  Feb 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280

  Shosti..mkaa hauna shida bwana wageni 6 sometimes mbaka kumi?? aargh wapi watakula kande mbaka wajut
  e
   
 14. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #14
  Feb 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  sasa ndugu zangu mimi kila siku hawana ..sasa sijui mi naziokotaga wapi..yani nimechoka
   
 15. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #15
  Feb 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Mi mtu wa Iringa..sina habari za kipare..tuna angalia cost reduction na inflation hii ukifanya mchezo 50 inakutoka kwa mchana mmoja tu ukijumlisha na vinywaji vya wageni!!
   
 16. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #16
  Feb 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Sweetie haya makande yanapikwa kwenye sufuria size ya kati sio unayajaza kama uko kwenye hitma..kiasi tu ..simple but smart!!

   
 17. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #17
  Feb 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Hebu Tafakari

  Ni mtoto wa kakako..kakuzidi umri..umemsomesha..umemtafutia kazi kaacha mara afanye vurugu..ameoa ana watoto kila akija anakuja na watu si chini ya 4 mpaka 6 na wanakula kweli..swala si uchoyo swala hapa ni kwamba nimechoka!! wao kila siku hawana..kwani waliskia nafanya kazi benki ya dunia?? ningekua mchoyo angeishi kwangu kaolea nyumbani kwangu..uchoyo wangu uko wap?? kumbuka nimetoka kulipa ada ya mtoto last month sina hela ..nime choka na siku ukija kwangu nakukandamizia kandamizia makande kama sina akili nzuri!!

   
 18. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #18
  Feb 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280

  Gamba,

  Mbaka nafikia kuchukua hatua wame take advantage sana ya roho yangu..ushauri huu nilipewa somewhere na rafiki yangu..inaweza isiwe kande tu..ila kitapikwa chakula kimoja tu cha siku nzima aidha pilau au wali ama makande lakini wali kilo ngap sasa maana kilo 2500..sasa ukinnua kilo 3 ni 7500 bado mboga mafuta na nini wakati hiyo 7500 inatosha kabisa makande na chenji ina baki na bia unakunywa huku unakalangiza..
   
 19. s

  shosti JF-Expert Member

  #19
  Feb 19, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  hahahahahahahhahaha kwa hizo kande ungenichukia maana ningetia timu kila jpili....ila maisha yamebadilika mpaka naogopa aisee nikikumbuka miaka ya nyuma wageni wakija nyumbani hata kama mlishaivisha maharage yenu bimkubwa anafanya utaratibu mwingine mnaingia jikoni haraka haraka kutengeneza mambo fulani kwa ajili ya wageni wenu huku mioyo misafi ajabu
   
 20. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #20
  Feb 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Shostito..Nataka niendeshe hii Fatiki ya kande kwa miezi miwili tu ili kila wakija wapeane taarifa.,zamani mkate ulikua sh 200 lakini sasa ni 1000..mshahara wenyewe chambenjela..sijui wanahisi nafanya kazi benki ya dunia..mpssxxyyy
   
Loading...