Kinuju
JF-Expert Member
- Mar 20, 2021
- 2,390
- 5,310
Wakandarasi wazawa wa Tanzania wamekuwa mfano mbaya sana kwenye ujenzi wa barabara nchini.
Waziri Mbarawa amelalamikia barabara ya Kidatu - Ifakara inayojengwa kwa lami na wazawa, ni mwaka wa 4 sasa hiyo barabara ya kilomita 64 haijakamilika.
Kuna barabara nyingine kule Musoma ya km 59 inajengwa na wazawa ni mwaka wa 5 sasa huu haijakamilika!
Wanachokifanya wakisikia kuna ziara ya waziri au kiongozi yoyote wa kitaifa anakuja wanakusanya magreda na vifusi, baada ya ziara kuisha wanatokomea kusikojulikana mpaka watakaposikia kuna ziara tena!
Hali hii inasikitisha sana hasa kwa kuwa wazawa wamekuwa wakilalamika kuwa wageni wanapewa kazi, je kwa hali hii ni kiongozi gani ataendelea kuwapa wazawa miradi ya ujenzi?