Makamu wa Rais ZNZ na Kifo cha CUF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamu wa Rais ZNZ na Kifo cha CUF

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by chipanga, Jun 1, 2011.

 1. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  Katika pitapita yangu nimekutana na habari hii, ya zamani kidogo;


  Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad aliwahi kusema na kunukuliwa na gazeti la nipashe la terehe 12/10/2007 kwamba atarejea kwenye chama tawala cha CCM kama atapewa nafasi ya kuwa Makamu wa rais.

  Alisema kama CCM itakuwa tayari kumpa nafasi hiyo yuko tayari wakati wowote kuanzia sasa (wakati huo) kurejea kwenye chama hicho kwa vile atatekeleza ahadi aliyoitoa kwa wananchi ya kuwaletea maendeleo.

  Aliyasema hayo wakati akiongea na Nipashe kwenye kumbukumbu ya kifo cha Nyerere mwaka huo wa 2007. Aliendelea kusema kuwa hajui ni lini atajiuzuru siasa maana mpaka sasa hajawatekelezea wananchi aliyohaidi, ambayo ni kuleta mabadiliko kiuchumi na kisiasa.

  Mzee aliongea mengi ikiwemo kugombea nafasi ya urais wa muungano baada ya JK, sitaki kugusia huko sbb naona km alikuwa anota tu.


  Binafsi hii habari ilivyo na nikiunganisha na matukio yaliyofutia hadi kuja kupata serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar Napata hofu kidogo, je huu ndio mwisho wa chama cha CUF katika uringo wa siasa za Zanzibar? na pia serikali ya mseto zanzibar ni kiini macho tu, ukweli ni kwamba Maalim na wenzie walioko serikalini wamerudi CCM kinyemela?

  Naomba mchango wenu wakuu.
   
 2. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mwenye macho haambiwi tazama, na alianza kutulia tangu walivyomtambua rasmi km w/kiongozi mstaafu wa znz na kumpa marupurupu yake yote
   
 3. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Kwani siasa dini ? Hivi siasa munaichukuliaje ? Whatever utakavyokuwa ccm au cuf,muhimu ni kwamba unawaletea maendeleo wananchi,waafrica sisi siasa tunaichukulia vibaya,kiasi ambacho badala ya kiongozi kufuata katiba anafuata chama kinavyosema sera zake. Hizo sera zenu za compain hatuzitaki katika uwongozi,tunahitaji mufuate katiba.

  Hapa tanzania na zanzbar viongozi wote hawafuati katiba zinavyosema na ndio maana tunapelekana kama landcruizer,Pia hata ile Articele of union.
   
 4. isk

  isk JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2016
  Joined: Mar 23, 2015
  Messages: 441
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 60
  Kumbuka hiyo posti yako alafu useme na wewe si mnafiki
   
Loading...