Makamu wa Rais Zanzibar, amuunga mkono Membe

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
48,757
102,104
Wakuu machafuko CCM yanaendelea,jana Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar amemuunga Benard Membe katika harakati za urais,amempamba kuwa ndiye kada anayefaa.

=========================

Dar es Salaam. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amesema atakuwa bega kwa bega na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe katika mbio zake za kuwania urais.

Membe, ambaye amekuwa akizungumzia kutangaza nia kuwania urais kama "kusubiri kuoteshwa", ameshasema siku ikifika atachukua fomu lakini anatarajia kutangaza rasmi mpango wake jimboni kwake Mtama, sasa anaungwa mkono na mmoja kati ya viongozi wa juu wa Serikali na CCM kutoka Zanzibar ambayo ina nafasi ya pekee katika kuamua mgombea urais wa chama hicho.

Balozi Iddi ambaye amewahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje tangu mwaka 2006, alitoa msimamo huo wa kwanza kwa kiongozi wa juu wa Serikali jana jijini Dar es Salaam wakati akifunga mkutano wa siku tatu wa mabalozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali, akimwakilisha Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein aliyeshindwa kuhudhuria kutokana na msiba wa dada yake.

"Namtakia Membe safari njema na ninamuahidi kuwa tutakuwa naye bega kwa bega katika safari hii ngumu kwake," alisema Balozi Idi bila ya kutaja neno urais.

Kauli ya makamu huyo wa Rais ilikuja baada ya Membe, ambaye amesema wakati ukifika atachukua fomu za kugombea urais, kuwaaga mabaozi hao kabla ya kumkaribisha mgeni huyo rasmi.

Katika hotuba yake ya mwisho kwa mabalozi hao, Membe aliweka wazi kuwa hatarudi tena bungeni akiwa waziri baada ya kuongoza wizara hiyo kwa takriban miaka minane.

Alirejea kauli yake ambayo amekuwa akiitoa mara kwa mara kuwa ameamua kuondoka wizarani hapo ili kujaribu nafasi kubwa zaidi katika siasa na kuwakaribisha bungeni mjini Dodoma ili wasikilize hotuba ya bajeti yake ya mwisho.

"Njooni msikilize bajeti yangu ya mwisho kama waziri kwani sitarajii tena kuingia bungeni kama waziri labda kwa nafasi nyingine ambayo ni ngumu sana," alisema Membe akiwaaga mabalozi 36.

Waziri huyo pia alitumia nafasi hiyo kuwaomba mabalozi hao kuitangaza Tanzania nje, huku akitahadharisha kuhusu mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea kutokea katika baadhi ya mataifa barani Afrika.

Alisema nchini Madagascar, Bunge limepiga kura ya kutokuwa na imani na rais na kuilazimu Mahakama ya Katiba kufanya uamuzi kuhusu suala hilo.

"Rais (Hery) Rajaonarimampianina amepigiwa kura 121 kati ya 125. Sitarajii kama kama Mahakama itaamua tofauti na matakwa ya Bunge. Hukumu inatarajiwa kutolewa leo (jana) baada ya kura hizo kupigwa jana (juzi)," alisema Waziri Membe.

Pamoja na kumuunga mkono Membe, Balozi Iddi aliwataka mabalozi hao kutumia vyema nafasi walizonazo katika kuitangaza Tanzania ili nchi inufaike na fursa za kiuchumi zilizopo huko walipo.

"Amani na utulivu ni rasilimali muhimu katika kuvutia wawekezaji. Zanzibar ipo tayari kusikiliza maoni yenu juu ya nini cha kufanya ili kuitangaza zaidi kimataifa," alisema.

Kaimu kiongozi wa mabalozi wa Tanzania, John Kijazi, akitoa neno kwa niaba ya wenzake, alisema mkutano huo umekuwa wa mafanikio na wamepata maazimio kadhaa wanayokwenda kuyatekeleza katika nchi wanakofanya kazi.

Aliitaka Serikali kuwawezesha ili kutekeleza majukumu hayo kwa ufanisi na kwa wakati ili kuleta tija. Aliwatakia kila la heri viongozi hao wawili wanaotoka katika jamii ya wanadiplomasia nchini katika harakati zao za kisiasa.

"Tunawatakia kila la heri katika nafasi mbalimbali mnazogombea. Kwa mfano wako, Balozi (Iddi) natarajia kuwa mwaka huu kutakuwa na utitiri wa wanadiplomasia watakaojiunga nawe," alisema Balozi Kijazi.

Chanzo: Mwananchi
 
Mtu wa hovyo ambaye CCM ikimsimamisha watashidwa vibaya ni Membe na Pinda.Tumaini la pekee kwa CCM ya sasa ni Lowasa au Maghufuri japo wanamapungufu yao lakini hakuna kiongozi asiyekuwa na Mapungufu..
 
Wakuu machafuko CCM yanaendelea,jana Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar amemuunga Benard Membe katika harakati za urais,amempamba kuwa ndiye kada anayefaa.Mwananchi rimeripoti zaidi

Watapigwa hasa hadi washangae just matter of time . Membe mtu a visasi anataka tuhame akisha kuwa Rais ? Kwanza Membe hana uwezo wa kuongoza . Mambo ya nje imemsinda hadi JK kawa Rais na waziri wa Nje .
 
Watapigwa hasa hadi washangae just matter of time . Membe mtu a visasi anataka tuhame akisha kuwa Rais ? Kwanza Membe hana uwezo wa kuongoza . Mambo ya nje imemsinda hadi JK kawa Rais na waziri wa Nje .

Hakuna atufaaye ccm kwa urais Tanzania
 
Kama ameshindwa siasa za Zanzibar za bara ataweza? Mwezi wa pili mwaka huu alikuwa anampigia chapuo pinda leo kamkimbia yuko kwa Membe
 
MAKAMU WA RAISI AMEPASUA JIBU ; KWA KUWEKA MSIMAMO WAKE WAZI KUMUUNGA MKONO WAZIRI KAMILIUS MEMBE KATIKA KINYANGANYIRO CHA URAIS

Source mwananchi
 
Wakuu machafuko CCM yanaendelea,jana Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar amemuunga Benard Membe katika harakati za urais,amempamba kuwa ndiye kada anayefaa.Mwananchi rimeripoti zaidi
Wewe jamaa uwa una matatizo sana ya uelewa, machafuko yapo wapi sasa hiyo ndiyo demokrasia unadhani Chadema hiyo ukipingana na Mbowe au Slaa unaitwa msaliti.
 
Wewe jamaa uwa una matatizo sana ya uelewa, machafuko yapo wapi sasa hiyo ndiyo demokrasia unadhani Chadema hiyo ukipingana na Mbowe au Slaa unaitwa msaliti.
demokrasia bila nidhamu ni furugu.hayo makundi yamejaa fitna,uchafu na rushwa ndio demokrasia?
 
Wewe jamaa uwa una matatizo sana ya uelewa, machafuko yapo wapi sasa hiyo ndiyo demokrasia unadhani Chadema hiyo ukipingana na Mbowe au Slaa unaitwa msaliti.

Mkuu mbona CDM kama umeivaa kama nguo? Hebu jaribu kuwa innovative katika mawazo, unaweza kutunga hoja bila kuisema CDM na hii itaonyesha kuwa innovative ki mawazo. Hiyo sheria uliyosomea uliipataje? Au ndo wale wa copy and paste?
 
Seif Idd, sio kiongozi, like Membe...hafai...!!! "Birds of same feathers fly together"..!!! Seif Idd jimbo lake huko Pemba hawezi pata tena, haya jimboni hakubaliki... sio kiongozi kabisa, just like Membe...!!!

Kiongozi pasipo na shaka CCM, kwa sasa ni Lowassa tu, huyu ndio tumaini jipya...!!! Bahati nzuri Wananchi wote wameonyesha moyo wa ajabu kumuunga mkono...!!! Mafuriko ya ajabu yataanza rasmi Arusha 30 May 2015...

Tunataka kiongozi mkweli, mtendaji, mwenye maamuzi magumu na asie na undugu na urafiki rafiki ktk kazi za serikali...!!! Ni Lowassa kwa sasa ndie mwenye hizo qualities and quantities za uongozi...!!!

CCM ndio kuna demokrasia ya UKWELI....unatangaza nia hata kama HUTAKIWI, UKO HURU, unaita vyombo vya habari na kusema mm nataka urais kupitia CCM, na hata ukiwa sio mbunge wa CCM, as long ni mwana CCM unaruhusiwa kugombea nafasi yoyote hadi ya urais ili mradi ufuate kanuni na taratibu za CCM, hakuna wa kumshika mtu mkono, NI WANA CCM ndio watakupa ridhaa kwa wingi wa KURA YAO KUKIONGOZA CHAMA CHETU CCM, of which i believe EL this time atapewa...

Ila huko CDM, ni UNDUMI LA KUWILI, Umangi meza, chama cha UKOO fulani tu, ukitaka kujua CDM ni ya MTEI family, of which Mbowe ni mkwe wa Mtei, jaribu kugombea UENYEKITI WA CDM uone... utafukuzwa kama mbwa, na kutwa msaliti, unfaithful to CDM, etc etc...hakuna uhuru na demokrasia ya KWELI CDM..., ww kama ni wa Mbeya, Tanga, Mtwara, Singida, Morogoro, mikoa mingine EXCEPT ARUSHA NA MOSHI....kuwa mwenyekiti wa CDM sahau kabisa... najua mtaongea sana hapa, ila jua Mbowe hana term limit ya UENYEKITI CDM, yaani atakuwa mwenyekiti forever... huo ndio ukweli, hakuna Demokrasia kabisa huko, which is exactly a MODERN DAY DICTATORSHIP rulers in CDM... and not leaders...!!! these cdm are soft tongue modern day dictators, hiding under umbrella of WORD DEMOCRACY... to fool the FOOLS....!!!

CCM 2015...the true Democracy and Leadership...!!!
 
Wewe jamaa uwa una matatizo sana ya uelewa, machafuko yapo wapi sasa hiyo ndiyo demokrasia unadhani Chadema hiyo ukipingana na Mbowe au Slaa unaitwa msaliti.
Changamoto waliyonayo wana-CCM ni kuwa watia nia wote hawana uwezo wa kujipima na kijitathmini ni nafasi gani ya uongozi wanaimudu!!!
 
Wakuu machafuko CCM yanaendelea,jana Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar amemuunga Benard Membe katika harakati za urais,amempamba kuwa ndiye kada anayefaa.Mwananchi rimeripoti zaidi

Analake jambo anamsapot huyu akijuwa fika ndie ambaye anamuelekeo kama wa kwakwe kuiuza Zanzibar Tanzania Bara
 
Huyu balozi seif idd mwenyewe ni goi-goi fulani ivi. Sasa sijui nani anaweza kuwa convinced na hilo chaguo lake.
 
anajipendekeza angalau apate ugombea mwenza, kaishiwa huyu mzee anaona hata akigombea uenyekiti wa mtaa hatopata
 
Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ally Iddi amesema atamuunga mkono Mh.Benard Membe katika mbio za kuwania urais kupitia tiketi ya CCM.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom