Makamu wa rais wa TLS akamatwa na Polisi Shinyanga akituhumiwa Ujambazi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,481
Makamu wa Rais a chama cha wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Godwin Ngwilimi amekamatwa na polisi huko mkoani Shinyanga na anashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi mkoani humo.
eb6287f1e6c408266ca15e448564a84d.jpg

Taarifa iliyotolewa na Rais wa TLS Mhe.Tundu Lissu ni kwamba Ngwilimi akiwa katika gari yake alisimamishwa na askari aliyekua kavaa kiraia, akitaka kukagua gari yake.

Ngwilimi alimtaka Askari huyo ajitambulishe kwanza kwa kutoa kitambulisho cha kazi kabla ya upekuzi. Lakini badala ya kujitambulisha alimzuia Ngwilimi na kumuelekeza kituo kikuu cha polisi Shinyanga ambapo anashikiliwa hadi sasa.

Chanzo cha habari ni Rais wa TLS Tundu Lissu
8fcf62e72160aec8118dbae976ac58ba.jpg

Wakili alikuwa natokea Mwanza kuelekea Dar es Salaam. Alipofika nje ya Shinyanga Mjini mida ya saa kumi na moja jioni, akasimamishwa na Askari wa Usalama barabarani, baada ya Kusimama ikaja gari ndogo iliyokuwa na watu watatu wanaodaiwa ni Makachero wakiwa na Siraha, wakamblock kwa mbele kisha wakashuka na kumwambia tunahisi wewe ni Jambazi hivyo shuka tukukague.

Akawambia hamuwezi kunikagua hadi mnioneshe Search warrant ya aliyewatuma. Wakaanza kumtisha ndipo akashuka kwenye gari na kusimama nje kisha akafunga gari akisimamia haki yake ya kupewa Search warrant ya aliyewatuma.

Katika kuvutanavutana ikabidi wapelekane kituo cha Polisi Shinyanga. Alipofika Wakataka Kusearch bado akakataa akawataka aje OCD, OCCID, RPC au RPO ndipo wamkague. Mwisho wake akapatikana mmoja ya hao aliowataka baada ya kusubiri muda mrefu, alivyokuja akaandika Search warrant na kuanza kumkagua.

Hawajapata chochote, hata gari lake halikuwa na Kosa lolote. Kwakuwa habari zilikuwa zimeshaaenea kwenye Mitandao ya Kijamii, Pia huyu Wakili ni Mwalimu wa sheria na amewafundisha baadhi ya Polisi waliokuwa Pale, Baadhi yao wakamtambua, wakaja kugundua kumbe waliyemkamata ni Makamu wa Rais a chama cha wanasheria Tanganyika (TLS).

Wakamuomba msamaha na kumwambia hawakujua. Wakamuomba radhi kwa kumchelewesha Safari yake. Ndipo wakamuachilia bila mashariti yoyote akaondoka zake mida ya saa nne usiku kuelekea Saa tano za usiku.
 
Hamna polisi wapuuzi wanaoweza mkamata MTU bila sababu.....Inawezekana huyu so called makamu wa rais TLS alitaka jificha kwenye mwamvuli wa makamo wa RAIS....maana na hii so called TLS ishakuwa chama cha siasa sasa.......wanafanya makosa intentionally wakikamatwa ionekane wanawindwa wao na haka katabia anako TUNDU LISSU ni hivi JESHI LA POLISI msicheke na hawa wapuuzi wachache zama za kuchekeana zishapitwa na WAKATI....
Mimi ndio ningekuwa ni RPC shinyanga kama kweli huyu jamaa kafanya kosa kwa kukusudia kisa eti ni kiongozi TLS dawa ni kumlaza KWENYE CHOO CHA MAABUSU usiku mzima AKILI ZIKAE SAWA......maana hawa wapuuzi wachache wana sababisha wengi kuumia badala jeshi la polisi kulinda raia huku mitaani linaanza kuhaingaika na hawa WAPUUZI wanaofanya maigizo
 
Unajua kazi ya jeshi la polisi ?

Ni kulinda RAIA wasidhuriwe na Mali zao.
Acha alindwe
 
Back
Top Bottom