BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 328
- 414
Na Bwanku Bwanku.
Wakati huu, Makamu wa Rais wa Marekani Bi. Kamala Harris akitarajia kuanza ziara yake nchini Tanzania siku ya kesho Jumatano Machi 29, 2023, historia ya mahusiano ya Nchi hizi mbili ni ya kusisimua sana ikianza mwaka 1961, miaka 62 iliyopita.
Ni ziara ya kimkakati ya kuendeleza mashirikiano na Taifa ikijikita kuendeleza mahusiano katika maendeleo ya kiuchumi, mabadiliko ya tabianchi, usalama wa chakula, ongezeko la idadi ya Vijana, kukutana na Wasanii wa Afrika na Tanzania ili kuongea nao na kujua namna bora ya kufikisha mziki wao kwenye masoko makubwa ya muziki Marekani.
Ni ziara inayoendelea kuweka alama ya kazi kubwa anayoendelea kuifanya Rais Samia Suluhu Hassan katika kufungua Nchi kiuchumi na kuimarisha mahusiano ya kimataifa yanayoshusha Viongozi wakubwa kama hawa wa kidunia kuja kufungua zaidi uchumi wetu.
Kwa mujibu wa kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Marekani imewekeza zaidi ya Trilioni 11 kwenye miradi mbalimbali hapa Tanzania ambayo imetoa ajira zaidi ya 50,000 kwa Watanzania ambapo kwa ziara hii ya Makamu wa Rais, itazidi kuimarisha uhusiano huu wenye faida kubwa na kufungua zaidi fursa za uwekezaji na biashara kati ya Nchii hizi mbili.
Tukumbuke, Kiongozi mkubwa kama huyu wa Marekani anapokuja nchini, anakuja na ujumbe mkubwa (delegation) iliyo na Wawekezaji wakubwa wa Marekani, Wafanyabiashara na makundi mengine makubwa yanayoangalia maeneo ya uwekezaji na biashara na mwisho Taifa kupata uwekezaji mkubwa unaofungua ajira zaidi, uchumi na maendeleo.