Makamu wa Rais wa Iran kuwasili kesho atalakiwa na mwenyeji wake, Dk. Gharib Bilal | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamu wa Rais wa Iran kuwasili kesho atalakiwa na mwenyeji wake, Dk. Gharib Bilal

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 28, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]


  na Mwandishi wetu

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dk. Mohamad Reza Rahimi, atawasili jijini Dar es Salaam kesho tayari kwa ziara ya siku tatu ya kikazi hapa nchini, ambapo atalakiwa na mwenyeji wake, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Gharib Bilal.


  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa Irani nchini, Mohsen Movahedi, alisema wakati wa ziara yake, Dk. Rahimi ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa hospitali mbili za kisasa huko Kigamboni na Mkoa wa Magharibi Unguja.

  “Jumatano ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa hospitali ya Kigamboni itakayogharimu sh. bilioni 1.5 na Alhamisi atakuwa Zanzibar kwa jukumu kama hilo katika ujenzi wa hospitali itakayogharimu sh. bilioni mbili,” alifafanua Balozi Movahedi na kuongeza kuwa, keshokutwa pia atazindua zahanati mpya ya Msasani ambayo imejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Iran.


  Akitoa ratiba ya ziara hiyo, Balozi Movahedi alisema mapema Jumatano, Dk. Rahimi ataonana na kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete Ikulu Dar es Salaam, kabla kuzumgumza na mwenyeji wake, Dk. Bilal na kisha kukutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.


  “Lengo kubwa la ziara ya Dk. Rahimi hapa Tanzania ni kukuza mahusiano ya kidiplomasia na kihistoria kati ya Tanzaania na Iran. Ni katika msingi huo Iran imetoa msaada wa ujenzi wa hospitali hizo mbili, pia itaweka vifaa na kuanza kuendesha chuo cha mafunzo stadi cha Zanzibar,” alisema balozi huyo wa Iran nchini.


  Kwa upande wa Zanzibar, Dk. Rahimi atakutana na kufanya mazungumzo ya kina na Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharrif Hamadi na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Iddi Seif.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  VP wa IRAN anazuru Tanzania Mwenyeji wake Dr. Bilal, atasema nini kuhusu Machafuko Zanzibar?

  IRAN huwa wanatoa pesa kusaidia zinazotaka kujitenga
   
 3. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Anakuja kuangalia kama jumiki na uamsho yao wanatumia vizuri misaada yao ya kuifanya Zanzibar kama Moghadishu. Matatizo yote haya yamesababishwa na CCM kuifanya nchi isijitegemee licha ya rasilimali lukuki. Matokeo yake Iran inahamasisha vurugu
   
 4. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,730
  Trophy Points: 280
  Anakuja kuwapongeza wana uamsho kwa kazi nzuri ya kulipua makanisa.
   
 5. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,986
  Likes Received: 1,557
  Trophy Points: 280
  ndivyo ulivyoambiwa kanisani kwako hivyo ????
   
 6. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2012
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,986
  Likes Received: 1,557
  Trophy Points: 280
  mchungaji wako ndio alikuambia hayo maneno kanisani??
   
 7. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2012
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,986
  Likes Received: 1,557
  Trophy Points: 280
  hayo umeyapata kanisani kwa mchungaji wako muhogolo??
   
 8. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,075
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Gavana walitaka aje obama atoe misaada ya masharti ya kukubali ushoga iingzwe kwenye katiba mpya labda ...
   
 9. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #9
  May 29, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,730
  Trophy Points: 280
  Nimeyapata kwa Mufti
   
Loading...