Makamu wa Rais ukimaliza likizo ya Sikukuu tembelea vibanda vya chips Dar na Dodoma ujionee maajabu!

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,227
26,047
Ofisi ya Makamu wa Rais ndo inashughulikia Mazingira.

Baada ya Mifuko ya Plastik kuweza kuondolewa pale Mama Samia alipokuwa Makamu wa Rais Naona sasa Waziri wako Jaffo anataka kuichafua Ofisi yako

Nimetembelea Dar na Dodoma Naona kwenye vipanda vya chips wameanza kufungia mifuko ya plastiki.

Kabla halijafika kwa Mama Samia naomba ufanye ziara ukimaliza likizo yako Kwa Dodoma au Dar tu alafu fanya maamuzi ya kumshauri Rais juu ya huyu Suleiman Jaffo. Naona kazi imemshinda.

Niwatakie heri ya sikukuu ya Noeli.
 
Ile mifuko ni dili la wenye nchi na wenye nchi wamerudi kazini kwaio sahau kuondolewa iyo mifuko.
Tupe ushahidi! Acha kubwabwaja

Mwenye nchi sasa ndo aliyesimamia kuondolewa kwa iyo mifuko sasa mantiki ya hoja yako iko wapi?
 
Alafu huyu Jaffo anaenda kununua PhD Udom badala afanye kazi zenye kuleta impact
Hivi nani alisikiliza presentation ya Jafo ya miaka 60 ya Uhuru performance ya wizara .yaani unaona kabisa hapa hakuna kitu . Anaulizwa swali majibu ya jumla jumla .hawa watu wanakula pesa zetu za bure hawana lolote
 
Daah..inasikitisha sana wapiga dili wameanza kurudisha viwanda vyao vya mifuko ya nylon taratibu..huku mamlaka zikibariki kuanzia rais..makamu wa rais..waziri mwenye dhamana hadi nemc...serikali ya ccm ni laana kwa nchi hii.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ofisi ya Makamu wa Rais ndo inashughulikia Mazingira.

Baada ya Mifuko ya Plastik kuweza kuondolewa pale Mama Samia alipokuwa Makamu wa Rais Naona sasa Waziri wako Jaffo anataka kuichafua Ofisi yako

Nimetembelea Dar na Dodoma Naona kwenye vipanda vya chips wameanza kufungia mifuko ya plastiki.

Kabla halijafika kwa Mama Samia naomba ufanye ziara ukimaliza likizo yako Kwa Dodoma au Dar tu alafu fanya maamuzi ya kumshauri Rais juu ya huyu Suleiman Jaffo. Naona kazi imemshinda.

Niwatakie heri ya sikukuu ya Noeli.
Je huyo Jafo ndio amewatangazia rasmi yatumie hiyo mifuko ya plastic au yeye aliichukua na kwenda kuwapa hiyo mifuko?
 
Back
Top Bottom