Makamu wa Rais Shein is the Best in Leadership: (Picha) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamu wa Rais Shein is the Best in Leadership: (Picha)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 19, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  What can I say.. you lead by example!

  [​IMG]

  Kwa mujibu wa Michuzi Makamu wa Rais akiwa kijijini cha Misenyi huko Kagera ambako yuko katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo. Alipewa zawadi ya ngoma na balakashia aliyovaa.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Duuuh jamani, huo u best in leadership ni kutokana na kupewa zawadi ya ngoma na kuipiga au hapa mimi sijaelewa hii title?
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kheee heeee heeee!
  Umeshaanza kuchokonoa na kusiko chonokoreka.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,238
  Trophy Points: 280
  Asante MMKJ. The man is simple, humble and down to earth. Hana majigambo, hajisikii, yaani yopo yupo tuu. Mungu ambariki sana!.
  Nakumbuka mwaka 2002 alikuja Rome kuhudhuria Mkutano wa World Food Day, Ten Years After. Baada ya Mkutano, on his way home, Alitakiwa apande Alitalia mpaka Bern, aunganishe na Swiss Air back home. Kufika airport Taarifa zikaja Alitalia imefilisika hivyo hakuna ndege. swissair wakamwambia asubiri hapo atatumiwa ndege nyingine any moment. Alisubiri tangu saa 2 asubuhi mpaka saa 10 Jioni. Balozi wakati huo Mahalu akashauri arudi hotelini lakini Muungwana akasema atasubiri tuu hapo hapo kama watu wengine.
  Alipata fursa ya kuongea na waTanzania tuliokuwa hapo, kusema kweli ni mtu wa ajabu, hakuonyesha kukerwa kokote, yaani ana uvumilivu wa ajabu. Wangekuwa viongozi wengine mbona pangekuwa hapatoshi.
  Binafsi japo tuliteseka sana haswa akina sisi wa senti zero on your way home, lakini
  Tulifarijika sana kuteseka na Mkuu wetu miongoni mwetu.
  He is really A Man of The People!. Tena bora JK asimalizie his second term bali ampishe huyu jamaa. Ni mtu wa Swala 5 kiukweli sio za kuzugia ama kuonyeshea watu waone. Nchi itatulia neema na ustawi vitaonekana.
   
 5. A

  Aluta Member

  #5
  Mar 19, 2009
  Joined: Aug 16, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hapo ni baada ya kukata UTEPE kwa MKASI wake; ambao haukosekani mfukoni mwake! Teh! teh!

  By the way; ni vizuri kuona Makamu wetu wa rais yupo serious na wananchi hana makuu na
  safari zisizo kuwa na mpango kama Rais. I think if Kikwete could be busy like this with Wananchi then we could have gone one step forward. Kuna viongozi hawajui hata mtanzania wa kawaida anaishije!
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Mar 19, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Nafikiri Dr. Shein anaweza kuwa rais mwenye maadili sana; hana makuu. Nasikitika sana kuwa Dr. Omar hatunaye tena, that man was probably the best of the best in CCM's top echelon.
   
 7. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Tatizo Shein na hata dr Omar, hawawezi kuchaguliwa kwa sababu wabongo tunapenda wababe na mapedejee na mabishoo.
  When we start rewarding people on merit, ndipo tutakapoanza kupata maendeleo ya kweli.
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Mar 19, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  I kinda like Shein.....yaani hata nikimwangalia sipati vi feeling vya yeye kuwa fisadi fisadi (I know I could be wrong but that's the vibe I get)
   
 9. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Kwani umefungiwa fisadi- detector mwilini?
  kwiwkwiiiii!
   
 10. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mzee kweli hana makuu.Pamoja na usomi wake uliotukuka lakini yuko simple tu.Urais haumfai huyu mzee kwa sababu anaonekana ni mpole sana na mwenye huruma huruma.
  Nasikia Kikwete alitaka amwage 2005,sasa sijui atarudi nae 2010?
   
 11. A

  Audax JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Shein mimi namuombea maisha marefu,katawala na mkapa alikuwa anamu isolate kama vile hayupo, mkapa na sumaye kuwa ndo wenye mamlaka. Lakini alikuwa mpole akalivumia na mkapa akaondoka,.angalieni na awamu hii,Mheshimiwa katulia, yeye na shughuli zakeo a kutembelea wananchi,wakishaharibu huko ndo wanamfuata,mheshimiwa kasoma na ameelimika.Ni mpole na anaheshima kwa wananchi woote bila kuchagua rangi wala kabila.
   
 12. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  sawa ni mpole nakubali, lakini is he effective as a leader? Mimi mpaka sasa hivi sijaona anachofanya au alichofanya kikubwa hata akiondoka tutamkumbuka/ I mean utendaji wenye impact kama vile wa akina Sokoine, Mrema, Magufuli na hata Lowassa (unfortunately)! TZ ni kweli tunahitaji kiongozi asiye na makuu kama Shein, but frankly we still need more than that!
   
 13. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimechungulia kwenye katiba nikakuta kazi za makamo wa rais wa tanzania kama ifuatavyo

  a)assist the president in making a follow up on the day to day implementation of union matter.
  b)perform all duties assigned to him by the president
  c)perform all duties and functions of office of president when the president is out of office or out of the country.

  back to you mkuu:utendaji wa makamo wa rais unaoutaka ufanane na wa sokoine,magufuli,mrema nk uko katika kipengele gani katika hiyo orodha ya kazi zake?Kila wakati tunamuona anakata utepe kuzindua miradi labda ndiyo kazi alizopangiwa na rais,huoni kwamba huyu mtu labda hatumiki vizuri hivyo kufanya ashindwe kuonyesha uwezo wake?
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Mar 20, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Oyaa Mkarateka salama lakini? Umejifunza kidogo kuhusu MMA?
   
 15. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Anatakiwa kuwa mbunifu. Yeye ni zaidi ya mawaziri na ni zaidi hata ya waziri mkuu! Kama unaweza kufikia cheo cha juu hivyo halafu unasubiri kuambiwa cha kufanya na mkuu wako wa kazi then kuna tatizo ndani ya "bongo za miafrika" au kwenye mfumo mzima wa uongozi wa nchi zetu.

  Katinba haimzuii kulivalia njuga suala moja kubwa kama ufisadi, mauaji ya albino, elimu, matumizi ya serikali, etc.
   
 16. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Ninadhani the guy is not effective as a leader!! Ni jambo gani anajiweza kujivunia baada ya kuwa madarakani miaka yote hiyo? Anaweza kutuambia ameifanyia nini nchi? He is part of failed leaderships, an associate of both regimes (the former corrupt and the present dying leadership). What has he done?
   
 17. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makamo wa Rais kwa katiba ya tanzania huwezi kumfananisha na waziri mkuu ambaye ndiye msimamizi wa shughuli zote za serikali.Ndiyo maana utaona hapo wamemtupa kwenye mambo ya muungano na kusubiri kutumwa na rais.Sasa ubunifu gani mkuu,aingilie majukumu ya watu?Utaona hata kama kuna shughuli inayomuhitaji rais ndani au nje ya nchi na akashindwa kufika basi atamtuma waziri mkuu amuwakilishe.kwanini asipelekwe shein?
   
 18. Yombayomba

  Yombayomba JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2009
  Joined: Aug 23, 2006
  Messages: 818
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Jamani,
  Hivi mlikuwa mnamjua Dr Omar au mnasema tu? JK is much better kuliko wote hawa.
  1) Nitaanza na Dr. Omar, kama kweli yeye alikuwa mtu wa watu kama mnavyotuambia mnajua ni gharama kiasi gani alizokuwa analiletea taifa? yaani kila weekenda lazima akalale Pemba kumbuka ni gharama gani za yeye na wapambe wake wote kwenda nao huko kila weekend? Huyu jamaa alikuwa ni mbabe kuliko hata Mkapa, kumbukeni hata hotuba zake akiwa waziri kiongozi.
  2) shein, ni dhaifu na wala hana ushauri wala msaada wowote ndo maana hata JK hana muda naye hilo wengi naona hamlihui, akipewa nchi tutarudi nyuma kuliko hata nchi ilvyochuchumaa wakati wa Myinyi. tuombe Mungu asituiletee hii balaa jamaa hamna kitu kichwani ndo maana mnaona huu upole, ambao ni sababu ya pumba kujaa kichwani
   
 19. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  yombayomba mkuu,
  Mi naona kama ulichokiongea hakiko-substantiated, kwa sababu:
  1. Dr omar sikumbuki ubabe wake labda kama unaweza ukatukumbusha specifically
  2. Dr Shein unasema ni dhaifu, kwa nini? kwa sababu siyo wheeler dealer na mtu wa ma-dili kama Jk? Ndo maana JK alimweka pembeni? Basi kwa taarifa yako hatutaki watu wa ma-dili kutuongoza, tunahitaji watu ambao wametulia (siyo kusaifiri kila siku kuuza sura kama JK) na wana uwezo wa kutafakari. Sidhani kama unaweza kulinganisha intelligence ya JK na Shein kwa sababu Dr Shein ambaye ni scientist anampita kwa mbali sana huyo beloved JK wenu! Rais wenu ndo kajaa pumba kichwani maana mpaka sasa hajafanya lolote - unasema Shein akiongoza nchi itachuchumaa, labda mwenzangu we maisha yako bado mazuri kutokana na kuwa uko karibu na moto, lakini maisha ya watanzania wengine hivi sasa ni dhaifu na nchi imeshakaa chini si kuchuchumaa tu!
   
 20. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huyo jamaa ni mpemba japo hajaenda kwao toka aukwae Umakamo sidhani kama anaweza kukabidhiwa zaidi ya hapo ,ila nuingependa kuona Karume anatimiza ahadi yake ya kuwa Raisi wa Muungano ,angalau walabu watafarijika.
   
Loading...