Makamu wa Rais Samia Suluhu amuwakilisha Dkt Magufuli Swaziland Mkutano wa SADC

Makamu wa Rais SAMIA SULUHU amuwakilisha Dkt MAGUFULI Swaziland Mkutano wa SADC

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ardhi ya mji wa Mbabane nchini Swaziland tayari kuhudhuria mkutano wa 36 wa SADC wa Wakuu wa nchi na Serikali ambao utafanyika tarehe 29 Agosti mjini hapo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Phiwayinkhosi Mabuza wa Swaziland ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha mara baada ya kuwasili kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Mfalme Mswati III.
........................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN amewasili mjini Mbabane - Swaziland leo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 36 wa Wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika- SADC-.

Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dakta JOHN MAGUFULI katika mkutano huo ambao utafanyika tarehe 29 Agosti 2016 ambapo Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo.

Mkutano huo wa 36 wa SADC ni maalum kwa wakuu wa nchi na serikali wanaounda Kamati ya siasa,ulinzi na usalama ambao watajadili kwa kina hali ya siasa na usalama, demokrasia na maombi ya Burundi na Comoro kwa ajili ya kujiunga na SADC.

Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN katika msafara wake amefuatana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amina Salum Ali.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Mbabane – SWAZILAND.
Naona Burindi wameamua kuingia SADC.Nice move kwenye suala la kibiashara na usalama.EAC maadui wengi.Hopefully watakubaliwa maombi yao.Mh Mahiga ni kiboko!
 
Sasa bila ya mkuu kutia mguu tutapewahuo u chairman wa Saddc ?
 
Yes, watu wanadumisha mila bwana ile wengine kwisa sindwa!!
 
Hehehe. Utajua utumwa wa muafrika hauwezi kuisha pale mweusi anaejua kingereza na kubeba ma box ulaya anamkebehi mweusi mwingine kwa kutokujua kingereza ila ni kiongozi wa watu million 50!!
Yani mweusi anaetumikia wazungu ulaya na kuwataza wazee huko ulaya leo hii anajiona ni bora kuliko kiongozi wa mamilioni ya watu kisa kujua lugha ya kingereza. Hahaha. Dah!

Sasa nini faida ya hicho kingereza? Inanishangazs sana.
Leo karne ya 21, miaka zaidi ya 50 baada ya "uhuru" wa mwafrika ila bado ubora wake unapimika kwa kiwango chake cha kufanana na mkoloni wake!! Na sio kwa ubora wa matendo na tabia yake!

Aisee, kweli kusoma sio kuelemika na wala kuelimika sio kuwa na akili wala busara.
 
Jiandae na makombora kutoka vichaka vya huko america na ulaya wanapoishi watumwa kutoka Tanzania.... Nakuomba uwe mvumilivu mkuu
 
Kwa hiyo ulitaka huo uenyekiti tupewe kwa fax?
Ili tu viongozi wasisafiri?
[HASHTAG]#Think[/HASHTAG] Big.
Ukumbuke Tanzania inakabidhiwa uenyekiti wa SADC. Hapo atakabidhiwa Samia kama nani? Naye akirudi nchini atafanya nini? Lumumba mnashida......
 
Ukumbuke Tanzania inakabidhiwa uenyekiti wa SADC. Hapo atakabidhiwa Samia kama nani? Naye akirudi nchini atafanya nini? Lumumba mnashida......
Umeelewa lakin nilichomjibu au umekurupuka tu kujibu???
Umejua tulianzia wapi au ndio umekurupuka best.
 
Back
Top Bottom