Makamu wa Rais Philip Mpango pole na hongera kwa hisia za Wanamtwara. Umeonesha uongozi bora

Paf

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,703
3,304
Dkt.Mpango wewe nikiongozi uliyeonyesha UONGOZI BORA NA SI UTAWALA WA MABAVU.
Hakika mbele za Mungu nakupongeza sana.

Leo 26/7/2021 umehutubia wananchi wa Mtwara waliokusanyika katika kuweka jiwe la msingi hospitali ya kanda ya kusini.Katika kufuatilia waliopewa nafasi ya kuhutubia miongoni mwao ni wasaidizi wako katika wizara.

Nikiri wazi kuwa shughuli za kiserikali zifuate taratibu za kiserikali bila kuingiza uvyama,Busara zako ulizotumia ni za hali ya juu sana pale ulipokuwa ukihutubia wananchi nao wakaanza kukuzomea kwa kelele nyingi huku askari wanataka kuwakamata nawe ukatoa neno WAACHENI TU.

Mh Makamu hisia hizo hazipo hapo Mtwara tu bali nchi nzima watu hushindwa kutoa ya moyoni kwa viongozi wakubwa wakihofia kukamatwa.

Ukweli ni kwamba wasaidizi wenu wanawapa viongozi bila kushughulikia shida za wananchi wa hali ya chini.

Niweke wazi kwa Leo kwa ushahidi.Dr Mollel sio msaidizi wenu mzuri

1.Leo kaongelea Katiba kwenye hadhira yako bila kupima kauli yake kwa wananchi.
2.Huko nyuma aliwahi toa kauli tata na chonganishi kuhusu tamko la TEC kwa habari ya korona (Mnafiki Dr Mollel)

Mh Makamu wa Rais, si utamaduni wa mtanzania kumuzomea kiongozi mkubwa kama wewe.Matokeo haya ya Leo hayajaleta picha nzuri kabisa.Hekima yako isingetumika hao wananchi wangekuwa mahabusu.

Pia niwapongeze sana wana Mtwara kukufikishia ujumbe wa hisia bila nidhamu Bali kwao ndio ilikuwa njia sahihi japo ulifika mahali ukagadhabika.Mungu amekuongoza sana vinginevyo mkutano huo ungevunjika kwa hisia zao Polisi usingewazuia.

Ombi langu:
Nchi hii ni ya wananchi na niyetu sote. Mnavyombo vyombo vinawapa taarifa daily lakini bado Kumekuwa na kauli tata zinatolewa na wasaidizi wenu za kuudhi.

Mkiweza kaeni faragha na Viongozi wa Dini zote muwape Uhuru waongee hali halisi ya nchi yetu.Maoni ya viongozi wa dini mtajua sura nzima za wasaidizi wenu.

Asante.
 
Hebu ongeza nyama, shida mpka kuzomewa ilikuwa ni nini?maana najua vyombo vyetu vya Habari havitatoa taarifa
 
Unaandika kama una rap,andika Uzi kama msomi hata ambaye hakushiriki huo Mkutano ajue kilichotokea
 
Cant believe kuzomewa kiongozi Tanzania bado ni issue inayowaweka watu jela, na please mwandishi kutokuzomea haihusiani na utamaduni wetu ni nidhamu ya woga tuu ya kupigwa au kufunguliwa mashtaka hewa na hao wakoloni weusi CCM
 
Unaandika kama una rap,andika Uzi kama msomi hata ambaye hakushiriki huo Mkutano ajue kilichotokea
Samahani Mimi sio msomi,ni machinga.nimeweza kuandika nilichoona live TBC wakati nakula kwa mama nitilie.
Unaweza ingia TBC oni laini cjui wanavyotamka.
Pole kama nimekukwaza
 
Back
Top Bottom