Makamu wa rais muungano ni changa la macho ?

sijuikitu

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
286
12
bilal1.jpg
Hapo zamani za kale kwa mujibu wa mkataba wa muungano, Zanzibar ilikuwa na mdau muhimu ndani ya muungano ambae pia alikuwa ni makamu wa rais ndani ya serekali ya muungano.

Tumeondoshewa hilo la uwakilishi wa Zanzibar katika nafasi hio.Sio tuu kwenda kinyume na makubaliano yaliopo ya muungano, bali pia ni kutuondoshea nafasi muhimu kwa Zanzibar katika mawasiliano na nchi za nje.

Hii sijuwi tuite kero ? Nadhani kuita kero itakuwa ni kupumbazana.Sasa hivi nadhani nikiwa kama mzanzibari sifahamu nini haswa kazi za makamu wa rais.Kutembelea mbuga za wanyama au kujadili migodi ya mkaa!

Kwa ufupi Zanzibar na watu wake tusipokuwa makini, basi taifa letu linaelekea kubaya (hatarini kupotea kwa maneno mengine).Hii ni ndoto mbaya kuchombezea mwana, M.Mungu atuepushie.Hapo kwa kukubushana kuomba dua pekee hakutoshi, jitihada za wazi zinahitajika kutoka kwa wazanzibari wenyewe.
 
Back
Top Bottom