Makamu wa Rais mteule, Dkt. Philip Mpango kuapishwa, Machi 31 saa 9 alasiri - Dodoma

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
1617099652729.png
 
Itakuwa vyema kama Mama Samia na serikali yake watabaki Dodoma kuliko kuhamia tena Dar.

Hongera zake makamu wa Rais.

Ni uchaguzi mzuri.

Umagufuli bila Magufuli nauona huoooo
 
Daaahh, mambo mengi muda mchache.

Jiwe alituchelewesha sana, au nasema uongo ndugu zangu?
 
Hongera kwake. Rais na Makamu wake nawaona wote wanamuonekano wa upole na usikivu, yale matamko ya hovyo ya Mpango wakati ule nadhani yalikuwa influenced zaidi na aina ya kiongozi aliyekuwepo, sitashangaa nikimuona tofauti wakati huu, ok sura ni ile ile, lakini maneno na matendo yake yanaweza badilika.
 
Kwa hiyo kutakuwepo na kagwaride kadogo ka jeshi la wananchi wa Tanzania au ataapishwa tu kama Waziri wa Nishati.
 
Ni matumaini yetu kwa Rais na Makamu wake kurejesha Tanzania ya Haki, uhuru na utengamano baina ya Watanzania.
 
Hongera kwake. Rais na Makamu wake nawaona wote wanamuonekano wa upole na usikivu, yale matamko ya hovyo ya Mpango wakati ule nadhani yalikuwa influenced zaidi na aina ya kiongozi aliyekuwepo, sitashangaa nikimuona tofauti wakati huu, ok sura ni ile ile, lakini maneno na matendo yake yanaweza badilika.
kwa hiyo tuwasamehe kina Harry James! Maana matamko yao ya kudunga watu sindano za sumu yalikuwa influenced na aina ya uongozi?
 
Itakuwa vyema kama Mama Samia na serikali yake watabaki Dodoma kuliko kuhamia tena Dar.

Hongera zake makamu wa Rais.

Ni uchaguzi mzuri.

Umagufuli bila Magufuli nauona huoooo
Mpango atulie sasa. Aache propaganda na makeke ya kigufuli gufuli. Akae kiserikali na siyo kichama. Akae mkao na mwenendo wa Samia Suluhu Hassan.
 
Ukiangalia kwa umakini utagundua kuwa nchi yetu ina uhaba wa viongozi licha ya kuwa na utitiri wa watu kwenye vyama na makundi mbalimbali ya kijamii.
 
Back
Top Bottom