Makamu wa Rais, linda ofisi yako. Wadau tunapata taabu kwa uzembe wa watendaji wako

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,238
2,866
Kuna tatizo kubwa ndani ya ofisi ya Makamu wa Rais. Tatizo kubwa ni utendaji hafifu wa ofisi ya Mkurugenzi wa mazingira tanzania bara. Ktk mikutano kadhaa ambayo nimehudhulia ktk kanda hii, Sehemu kubwa ya wafadhili hawana imani na mkurugenzi aliyepo kwa sasa hivi. Mkurugenzi huyu anatambuliwa kama mtu fisadi mbele ya macho ya wahisani wa mazingira. Hali hii imekuwepo kwa muda mrefu lakini kwa sasa yaonekana kuumiza serikali baada ya serikali kumtambua rasmi kama Mkurugenzi wa mazingira. Hapo awali alikuwa mkurugenzi msaidizi na haikujionyesha sana.

Kihistoria kutoaminika kwa mtu huyu kulianza miaka ya 2010. Nikihudhulia mkutano mmoja pale Nairobi, mwenzetu mmoja toka moja ya taaisis mashuhuri zinazofadhili miradi ya mazingira, alionyesha masikitiko makubwa juu ya tabia ya bwana huyu, kwa kueleza kwamba alishadiriki kuomba rushwa ili aruhusu mradi wa mazingira. Hali hii ya malalamiko imeendelea kujionyesha na hivi karibuni pia nimesikia nikiwa ktk mkutano mwingine wa kimataifa.

Chonde Chonde kwa ofisi ya makamu wa rais! Mazingira inaendeshwa kwa pesa ya wafadhili. Tunaomba mtu huyu arekebishwe. Kama imeshindikana, tafuteni mtaalamu mwingine.
 
Nahisi namfahamu unayemlalamikia. Kama ni huyo jamaa, iko taabu kabisa. Nimeanza kusikia vituko vyake siku nyingi enzi za akina Batilda. Kwake yeye wizi na ufisadi ni jambo la kawaida. Alishacha mambo ya ushirikina?
 
Mrekodini audio na video anaomba rushwa. Kisha muanikenu.

Teknolojia yote hii mnalialia bila ushahidi?
 
Kama ni huyo ninayemhisi, nadhani hii alert inatosha. NIna hakika hata serikalini anafahamika na kwa kuwa lengo siyo kumshitaki mahakamani, hii inatosha kutupa nje takataka.
 
Ufisadi na Serikali za CCM ni kama ndugu wa baba mmoja mama mmoja..

Sijui unawatenganisha vipi..

Ni ndani ya Serikali hii watuhumiwa wa Rushwa wamepata kuwa promoted..

Ni ndani ya serikali hii, mazingira na matendo ya rushwa hufanyika waziwazi mfano kwenye Chaguzi za CCM lakini hakuna hatua zozote zile zinachukuliwa na watuhumiwa..

Main problem is this, hakuna DHAMIRA ya DHATI ya kupambana na rushwa..

Rushwa haiwezi kuisha asilani Tanzania.
 
Kama ni huyo ninayemhisi, nadhani hii alert inatosha. NIna hakika hata serikalini anafahamika na kwa kuwa lengo siyo kumshitaki mahakamani, hii inatosha kutupa nje takataka.
Tatizo lenu ndiyo hili.

Mnategemea kudra sana.
 
Tatizo lenu ndiyo hili.

Mnategemea kudra sana.
Nawe unaleta ugomvi usiokuwepo. Sisi akina nani? na wewe ni nani?
Ukisoma msg hiyo mwenye thrd hatafuti njia ya kumshitaki. yeye anatahadhalisha watawala wake, Makamu wa rais wachukuwe hatua za kiutawala. angetaka mashitaka angetahadhalisha PCCB:

Wewe umesema wamrecord, ili iweje? Kama unatafuta mbinu ya kumfikisha mahakamani, ni sawa kabisa kuomba ushahidi. Hilo ni suala la uaminifu. Basi! Hebu soma tena maana uelewa tunatofautiana.
 
Naleta ugomvi uliokuwepo kati ya wanaokumbatia na wasiokumbatia wala rushwa.

Kati ya wazembe wanaolialia na wanaotaka mambo yafuatiliwe.

Unasema hatafuti njia ya kumshitaki wakati hata kupost hapa JF ni aina ya kumshitaki.

Unaji contradict.

Kama hamuwezi kufuatilia mambo kwa njia rasmi za kimahakama na kimashtaka mtaombwa rushwa mpaka kupumua.

Na itakuwa haki muombwe rushwa hivyo.

Maana uzembe wenu wa kutofuatilia mambo utawahukumu muwe chakula cha wala rushwa.
 
Una tatizo la uelewa na una tatizo la kiuandishi. Unatumia muna hiki, muna kile, siye akina nani? Na wewe ni nani? Just say it! Are we the ignorant and you the learned? Say it!
 
Wewe hujui kusoma wala kuandika.

Ndiyo maana hujui kuandika "mna" unaanika "muna" kama MCongo.

Ndiyo maana nimeandika nyie wazembe halafu bado unauliza nyie kina nani.

Hujui kusoma. Hujui kuandika. Mzembe. Mjinga. Ngumbaru.

Guluguja.
 
Sorry for my poor Kiswahili language command. It is a native in me. Let us go english. If that will still give you uncomfortable understanding, I may take you to the absoluteness of Latin language.
Who are you?-- And who are we?
 
Wewe hujui Kiswahili wala Kiingereza.

Tatizo lako si lugha tu.

Tatizo ni uwezo wako wa kufikiri.
 
Mrekodini audio na video anaomba rushwa. Kisha muanikenu.

Teknolojia yote hii mnalialia bila ushahidi?
Hizi ni enzi za immediate reaction na changes zinafanyika mara moja kwa manufaa ya nchi. Hizo habari za kupoteza muda wa kutafuta ushahidi wa mahakama ili mtendaji aondolewe, hazihitajiki tena. Atashitakiwa wakati yuko nje ya ofisi.
 
Sasa change gani zimetokea mpaka sasa kwa hiyo immediate reaction unayosema?

Hizi ni enzi za serikali isiyopangiwa.
 
Sorry for my poor Kiswahili language command. It is a native in me. Let us go english. If that will still give you uncomfortable understanding, I may take you to the absoluteness of Latin language.
Who are you?-- And who are we?
nipo hapa kushuhudia mtanange
 
Back
Top Bottom