Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Harakati ya William Ruto Makamu wa Rais wa Kenya ya kutaka kuwa Rais wa nchi hiyo baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutarajiwa kumaliza muda wake 2022 wa awamu ya 2 endapo Rais Uhuru Kenyatta atatawala mihula miwili, kutasababisha kwa Rais Uhuru Kenyatta kushindwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga katika uchaguzi utakaofanyika mwezi wa nane mwaka huu.
Willam Ruto ameonyesha chuki za wazi dhidi ya Gideon Moi mtoto wa Rais mstaafu Arap Moi ni hii inaweza kupunguza kura za Jubilee katika eneo analotoka Gideon Moi la Baringo, Gideon Moi mwenyewe ana dhamira ya kugombea urais mwaka 2022.
William Ruto amesababisha Gavana wa Bomet Isack Ruto kutoka chama cha Jubilee na kuanzisha chama cha mashinani ambacho kipo kwenye Muungano wa vyama vya NASA, Isack Ruto anatoka kabila la wa Kipsigisi ambao ni sehemu kubwa ya wapiga kura wa Bonde la Ufa. Viongozi wengi wameamua kuacha kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta baada ya Makamu wa Rais William kuendesha kampeni chafu dhidi yao akimutumia mpambe wake Adan Duale.
Aliyekuwa mgombea ugavana wa Nairobi Peter Keneth na aliyekuwa mgombea ugavana Kiambu Kabogo wote wamejiondoa kwenye chama cha Jubilee na kuamua kuwa wagombea binafsi baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mchujo wa Jubilee na wote wamelaumu kwa William Ruto kuhusika kwake binafsi katika wao kushindwa. Ikumbukwe Gavana wa Kiambu Kabogo alishawahi kutamka kuwa William Ruto hawezi kuwa Rais wa Kenya 2022.
Kama Rais Uhuru Kenyatta atashindwa uchaguzi wa mwaka huu Makamu wake William Ruto atachangia kiasi kikubwa.