Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango azindua sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,886
938
MHE. DR PHILIP MPANGO, MAKAMU WA RAIS WA JMT KATIKA UZINDUZI WA SERA YA TAIFA YA MAZINGIRA YA MWAKA 2021.

Makamu wa Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mhe .Dkt. Philip Mpango Ashiriki katika uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021 iliyozinduliwa leo 12 Februari, 2022 Jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dodoma leo.

✍🏻Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021 imejumuisha masuala ya mazingira yaliyokuwemo katika Sera ya 1997 na masuala mapya.

Masuala mapya katika Sera mpya ya mwaka 2021 ni pamoja na:

✍🏻Udhibiti wa taka za kielektroniki, Usimamizi na matumizi ya kemikali, na Udhibiti wa uchafuzi katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi.

✍🏻 Mabadiliko ya tabianchi; Usimamizi wa matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa; na Udhibiti wa viumbe vamizi.

Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021 imeongeza wigo wa masuala na changamoto za mazingira zinazopaswa kufanyiwa kazi katika kipindi husika ili kuleta maendeleo endelevu na imezingatia changamoto mpya za kimazingira zinazoendelea kujitokeza kutokana na mabadiliko ya mifumo ya kiuchumi, kijamii na kimazingira yanayoendelea duniani” Alisisitiza Bi. Mary Maganga.

Serikali imeamua kuwa na Wiki ya Uzinduzi wa Seraitakayoanza tarehe 07-12/02/2022 ambayo itaambatana na shughuli mbalimbali za hifadhi ya mazingira ikiwa ni sehemu ya masuala ya msingi yanayoelekezwa katika Sera mpya.

#KaziIendelee

IMG-20220212-WA0038.jpg


IMG-20220212-WA0039.jpg


IMG-20220212-WA0043.jpg
 
Safi sana sana sana!!!!

Kuna kitu nakiona kinakuja kwa huyu makamu na mama.....muda si mrefu haters nao watakiona!!
 
Back
Top Bottom