Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango atambue utendaji mbovu wa MSD umechangiwa na mambo haya

Kanzastone

JF-Expert Member
Jan 14, 2021
244
355
Jana Jumatatu tarehe 21 June,2021 Makamu wa Rais Mh. Dkt Mpango aliitembelea Bohari ya Dawa MSD ili kujua utendaji wa hiyo Bohari ambayo ni kiungo muhimu sana katika sector ya afya kwasababu MSD inashughulika na mambo makuu 3 kutokana na uanzishwaji wake na sheria ya bunge na. 13 ya mwaka 1993 ambapo ni; kununua dawa, kuhifadhi pamoja na kusambaza dawa kwenye vituo vya afya nchi nzima.

Ujio wa Mh. Rais hapa Bohari ya Dawa MSD umekuwa wa ghafla kutokana na uzorotaji wa utendaji wa hii Bohari ya Dawa ambapo ilianza kuwa mbaya zaidi kuanzia mwaka 2016 na sasa hivi imezidi kuwa mbaya zaidi chini ya afande aliyepo sasa hivi kama Mkurugenzi Mkuu wa taasisi.

Nilimshangaa saana Mh. Makamu wa Rais kuzungumzia issue za; udokozi wa dawa kwamba ndo tatizo lililochangia uhaba wa dawa nchini KITU AMBACHO SIO KWELI, Mh. Rais kalishwa matango pori katika hilo. Eti Mh. Makamu wa Rais anadiliki kusema eti MSD ikae na Idara ya Utumishi ili kuangalia integrity ya wafanyakazi, sawa hilo inawezekana lakini hilo sio core tatizo linalochangia utendaji mbovu wa MSD.

Mh. Makamu wa Rais anatakiwa atambue kuwa utendaji mbovu wa MSD umechangiwa na mambo yafuatayo;

1. Wakurugenzi wakuu ambao wamekuwa wakiletwa MSD tangu mwaka 2016 wamekuwa ni watu wanaoletwa kwa majaribio yauongozi na hivyo kukosa vision

2. Kumekuwa na mgawanyjko mkubwa miongoni mwa Wakurugenzi hivyo kukosa common goals

3. Kumekuwa na uendeshaji wa taasisi kimajungu sana ambayo yanakuwa entertained na uongozi wa juu kiasi cha kwamba wafanyakazi wamekuwa wakikosa confidence ktk utendaji

4. Kila Mkurugenzi Mkuu mgeni akifika focus yake kubwa inakuwa ni kuwaondoe wafanyakazi waliokuwepo ili aweke anaowataka yeye

5. Matokeo yake as per 4. above wageni wapya wanakuwa na learning curve ya muda mrefu sana na kuathiri utendaji wa taasisi

6. Kuwaweka watu kwenye maeneo ambayo sio fani yao. Kwa mfano hivi karibuni kuna mfanyakazi aliwekwa kwenye nafasi ya Mkurugenzi wa Manunuzi wakati huyo hajaisomea hiyo fani mpaka wizara walipotoa instruction ya kumuondoa ndipo akatolewabkwenye hiyo nafasi

7. Pamekuwa hapana utulivu

Kwahiyo Mh. Makamu wa Rais anatakiwa aliangalie kwa jicho la pili kuhusu utendaji wa MSD. Kwa mfano kuna Mkaguzi Mkuu wa Ndani ambae amekuwa hana msaada wowote kwa hii taasisi, hawezi kufanya ukaguzi wa mfumo n.k

Asante.
 
Tatizo lingine ni hiyo taasisi ni kama inaendeshwa Kisiasa zaidi badala ya kitaalam.

Imefikia hatua vituo vya Afya vinaishiwa hadi Panador tunaambiwa tukanunue kwenye maduka ya Dawa ya nje ya Hospitali.
 
Ametembelea Dr Phillip Mpango Makamu wa Rais kuangalia shughuli tu ya kuagiza dawa. Sasa nakubali kweli nafasi ya Makamu haina kazi (Redundant). Yaani unakuwa IDLE mpaka unaamua kwenda Bohari Kuu ya Dawa? Si angemtuma Waziri wa Afya tu?? Too low for VP. Wakati wa JKikwette, Gharib Bilal kazi yake ilikuwa ni kukata utepe kwenye majengo yanayo zinduliwa. Naye alikuwa IDLE.

Katiba ijayo iachane na nafasi ya Makamu wa Rais kwa kuwa iko redundant. Sana Sana kama kuna majukumu kidogo Basi yawe consolidated kwa Prime Minister.
 
Jana Jumatatu tarehe 21 June,2021 Makamu wa Rais Mh. Dkt Mpango aliitembelea Bohari ya Dawa MSD ili kujua utendaji wa hiyo Bohari ambayo ni kiungo muhimu sana katika sector ya afya kwasababu MSD inashughulika na mambo makuu 3 kutokana na uanzishwaji wake na sheria ya bunge na. 13 ya mwaka 1993 ambapo ni; kununua dawa, kuhifadhi pamoja na kusambaza dawa kwenye vituo vya afya nchi nzima.

Ujio wa Mh. Rais hapa Bohari ya Dawa MSD umekuwa wa ghafla kutokana na uzorotaji wa utendaji wa hii Bohari ya Dawa ambapo ilianza kuwa mbaya
Shida haijaanza hiyo 2016
Wala si kwa sababu ya uongozi mpya
Shida ni watawala
Watawala kwao muhimu ni siasa posho/wabunge teuzi na ubinafsi
Hospitali za serikali zina madeni kuliko
Wizi rushwa ndio mwake

Mfumo mzima ni mbovu
Umemzungumza afande huyu aliyekwa juzi kati au?
Bohari inaagiza cheap medicines from India na China tangu enzi za mstaafu so afande unamuonea au kuna lingine
 
Kuna mtu kapiga simu anashangaa sana kuona kwamba ni kwanini Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Bohari ya Dawa MSD bado yupo wakati hajawai kuonyesha impact yoyote ya utendaji katika taasisi hii.

Mkaguzi Mkuu wa Ndani kazi yake imekuwa kufanya kazi zake kwa majungu tu, hafanyi kazi ki-profession kama wafanyavyo wakaguzi wengine kwenye maeneo mengine. Mbali ya ku-base kwenye majungu katika utendaji wake ambao unachangia kutokuwa na output yoyote, Mkaguzi Mkuu wa Ndani pia amekuwa ni mtu aliyefanikiwa sana kuwagawa wafanyakazi wa kwenye Idara yake.

Dawa zinaharibika yeye yupo tu, mtandao wa kompyuta unashindwa kufanya kazi accurately yeye yupo tu, mtu anawekwa kwenye nafasi ya Ukurugenzi wa Manunuzi wakati hana sifa yeye yupo tu!!

Huyu mtu hajakuwa na msaada wowote kwa Mkurugenzi Mkuu mbali ya kufanya kazi kimajungu and unethical kabisaa.
 
Tatizo la MSD ni mfumo na sio kiongizi. Hata akiletwa kardinali pengo kuwa dg hapo bado kutakuwa na changamoto. Kuna network kubwa sana ya wizi wa madawa ndio maana akiletwa mkurugenzi halafu aanze kuziba mianya lazima ahujumiwe au apigwe zengwe. Akijaribu kuwatoa watumishi wanaoonekana ndio masterminder wa wizi wa dawa basi atapigwa zengwe tu.

Huenda hata wewe mleta mada ukawa ni mmojawapo wa watumishi wapigaji.
 
Kwa hiyo yule BWANAKUNU alipigwa zengwe kwa sababu ya kuziba wizi? Kama ameonekana hana makosa na DPP basi arudi ofsini na major General aende Jeshini alikotoka
 
Tatizo la MSD ni mfumo na sio kiongizi. Hata akiletwa kardinali pengo kuwa dg hapo bado kutakuwa na changamoto. Kuna network kubwa sana ya wizi wa madawa ndio maana akiletwa mkurugenzi halafu aanze kuziba mianya lazima ahujumiwe au apigwe zengwe. Akijaribu kuwatoa watumishi wanaoonekana ndio masterminder wa wizi wa dawa basi atapigwa zengwe tu.

Huenda hata wewe mleta mada ukawa ni mmojawapo wa watumishi wapigaji.
Kwani askofu pengo ndio nani!

Kinachotakiwa hapo ni kiongozi mwenye; team work na sio kuwagawa wafanyakazi, mwenye high level of integrity, mwenye vision iliyo clear kuhusu taasisi husika na sio kufanya kazi kwa kurukiarukia tu vitu ambavyo continuity yake ni questionable.

Kupigwa zengwe ni kitu gani. Huwezi ukawa na kiongozi ambae focus yake kubwa ni kuwatoa watumishi aliowakuta na kutaka kuwaweka watu wake kwa kisingizio cha eti kuziba uizi wa dawa. Kama uizi upo basi ni udokozi tu na sio kwamba eti mtu anaweza ku-justify uhaba wa dawa nchini na udokozi uliofanyika la sivyo mtu afanye quantification ya uhaba wa dawa na dawa zilizoibwa bohari ya dawa msd kitu ambacho sidhani kama kutakuwa na uhalisia wowote.

Wakiletwa wakurugenzi wenye clear vision, wasiofocus kuwatoa watumishi waliowakuta, wasioendekeza majungu, mfumo wa tehama uliotengemaa, mkaguzi mkuu wa ndani akifanya kazi kiutaalamu bila majungu na kumshauli vizuri dg nafikili utendaji wa bohari ya dawa itakuwa nzuri.

After all, kwa kiongozi change management ni pamoja na kubadirisha mtazamo na fikra za watumishi uliowakuta na sio kufukuzafukuza tu, huo ndo uongozi!
 
Back
Top Bottom