Makamu wa Rais Dkt. Mpango kaeleza ukweli aliposema kupata hofu baada ya kauchiwa kuongoza nchi

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,862
5,680
Makamu wa Rais Bwana Philip Mapango wakati akimpokea SSH alisema kuwa alipata hofu alipo achiwa nchi kwa siku hizo chache lakini anashukuru SSH amerudi ameutua mzigo.

Wengi wanamlaumu Makamu wa Rais kwa kudai kuwa eti ameonesha udhaifu Sana ktk uongozi kwa kusema kuwa aligopa na alitakiwa kuwa mkakamavu na kujiamini.

Wanao mlaumu hawajui tuu kuwa jamaa kasema ukweriiii na msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Huwezi ingia madarakani kwa wizi wa kura na hadaa halafu usibakie na hofu kwa wananchi unao walazimisha kutawala.

SSH alisikika akiwa Mbeya akisema hata mkipigia kura Chama kingine CCM ndio itakayo unda serikali. Alikuwa anajua hawakubaliki na wananchi ila wataunda serikari ya mwanasesere.

Mpango ataachaje kuwa na hofu ikiwa Chama Chao kimeshinda kwa kishindo uchafuzi halafu kinaogopa kongamano la KATIBA la Chama kisicho na Mbunge hata mmoja bungeni?

Ktk serikali iliyo undwa ya Mseto ya Jeshi la polisi na CCM unaachaje kuwa na hofu? Hofu lazima iwepo maana hujui polisi wanawaza nini juu ya kutwaa Madaraka na wananchi pia hujui wanawaza nini.

Mpango sio mtu wa Kwanza kueleza ukwerii kuwa CCM haikubaliki. Hata Kikwete aliwaambia ukwerii kuwa CCM kwa sasa inategea polisi kufanya siasa na wakiendelea itakula kwao.

Ni ktk mazingira hayo utaona lazima kubinya haki za watu ili mkoloni mweusi CCM aendelee kutawala. Mtabambikia watu kesi zisizo na mashiko kwa hofu ya kupoteza Madaraka lakini haita saidia kitu. KATIBA mpya ni lazima tuipate iwe jua iwe mvua.

Kwa taarifa yenu ni kuwa Madaraka mmesha yapoteza hayo mliyo nayo ni Madaraka ya Mwanasesere tuu Bibi wewee.
CC Mataga
CC Chifu Hangaya.
 
Nilitegemea hoja kuhusu hofu ya Mpango, Makamu wa Rais, kumbe ni kuanika hisia zako za kuibiwa kura!! Hakuna hata mgombea mmoja ambaye amefikisha tuhuma za kuibiwa kura kwenye vyombo vya Haki, kikatiba.
 
Mh.Dr Mpango ni lazima awe na hofu....yeye si mkuu wa nchi....yeye si amiri Jeshi wa majeshi ya Ulinzi na usalama.....

#SiempreJMT
 
Mtama Mghabho Ametuangusha Na Vidono Vyetu Sisi Waha
Wabhonye Chambu
Hajawaangusha....

Anajitambua....

Huyo msomi na muumini wa adabu na heshima kwa BOSS wake.....

Naye mh.SSH alikuwa hivyohivyo chini ya hayati JPM(Rip)....

#SiempreJMT
 
Nilitegemea hoja kuhusu hofu ya Mpango, Makamu wa Rais, kumbe ni kuanika hisia zako za kuibiwa kura!! Hakuna hata mgombea mmoja ambaye amefikisha tuhuma za kuibiwa kura kwenye vyombo vya Haki, kikatiba.
Utakuwa una matatizo kichwani dogo, toka lini kesi ya ngedere akapewa nyani kuwa hakimu? Ndio maana watu wenye Akili wameona KATIBA mpya ndio jibu la hayo matume huru ya CCM ambayo matokeo yake hayapingwi Mahakamani.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Kwanza mimi siyo dogo, hivyo huna hoja ila yaelekea ni mwenyeji wa kijiweni.

Kusingizia kukwama kwa masuala mbalimbali (kwa mfano uliotoa) kuwa ni "KATIBA" kana kwamba ni "mtu" ni ishara ya uvivu, ufinyu na ufukara wa mawazo kiuhalisia wa mambo kimaisha.
 
Mimi ni muimini wa utawala bora wa sheria na haki ila napingana na wewe kusema katiba ndio suluhisho sio kweli suluhisho hapa ni sisi wenye nchi yao yaani wananchi wa Tanzania kuilinda na kuitetea na kuisimamia katiba isivunjwe nakuhakikishia hata hii iliyopo sio mbaya sana ubaya tume uleta sisi wenyewe nchi sio wanasiasa wala viongozi

Hawa wanaotutawala au kutuongoza wanapo ivunja katiba kwa kwenda minyume chake mfamo spika wa bunge kavunja katiba kwa kuwa pokea na kuwa ruhusu wabunge hewa ambao hawajakidhi matakwa ya katiba kuwa wabunge wale 19 wa wanajiita niwa chadema wakati chadema walisha wafukuza sasa kwa kosa hili na mengine mengi ambayo viongozi wanaya fanya ikiwemo kuzuia kufanya mikutano ya siasa, sisi wanyenchi tungeilinda katiba kwa kuandamana nchi nzima kwa mda usio koma ili kushinikiza viongozi wetu kutoendelea kuvunja katiba..

Sasa unapo sema tunahitaji kaiba mpya kama hatuwezi kuilinda na kuitetea sisi wenye nchi wala haina maana yoyote itakuwepo ndio lakini wataivunja na hamna kitu watafanywa walioivunja mbona sisi raia au wanachi tukikosea sheria hukuchua mkondo wake mfano, ukiua, kuiba, kubaka, nk mbona mahakama na police zipo kwa ajili ya kutushufhulikia kwann na. Wao tusiwashughulikie wanapo tukosea kwa kukiuka katiba yetu waliyoapa kuitetea na kuilinda??

Najua jibu unalo huwezi kujibana wewe mwenyewe unapofanya kosa, utabanwa na wengine ulio wakosea sasa leo hii mahakama, majeshi ikiwemo wa police wote ni mali ya viongozi walio madarakani walio shika dora watashughulikiwa na akina nani kama sio mimi na wewe!?? Fikiria mkuu wa majeshi yote na mkuu wa police na Jwtz, majaji, wote wanateuliwa na mtu mmoja alie kweny chama kinachoongoza dora je kiongoz huyo alie kuteua akifanya kosa la kuvunja katiba anaweza kuwajibishwa na watu alio wateua??!! Jibu unalo ndo maana ya hayo yote wanayo endelea nchini kwetu, ukiwa mpinzani nchi hii na mkosoaji, msemaji ukweli kama, Mbowe kila siku makesi ya uongo au utauliwa kama Lissu , ben saanane, mawazo, au kuteswa kama Mdude, msaani Roma mkatoliki na wengine wengi

Wananchi wa Tanzania tuamke usingizini tutaburuzwa mpaka tumbe poo tutakuwa watumwa kweny nchi yetu kwa kuwa hatujui wajibu wetu wala haki zetu au ni wigan wetu je babu zetu leo yaani nyerere angejihurumia na kuogopa mazungu na wakoloni leo hii tunge kuwa wapi je kungekuwa na neno wala nchi Tanzania tuache ushamba, mabeberu na WAKOLONI wa leo hii ni CCM ambao miaka 60 yote wanatufanya wajinga.
 
Raid alisafiri tu. Hakumkabidhi mtu yoyote madaraka yake. Lingetokea tatizo angerudi bila hata kuihutubia UN
 
Nilitegemea hoja kuhusu hofu ya Mpango, Makamu wa Rais, kumbe ni kuanika hisia zako za kuibiwa kura!! Hakuna hata mgombea mmoja ambaye amefikisha tuhuma za kuibiwa kura kwenye vyombo vya Haki, kikatiba.
Hivyo unavyoviita vyombo vya haki ndivyo vilivyoanza kusema kabla ya uchaguzi "hata mfanye nini hamuwezi kushinda"!
 
Mbaba anaogopa kuongoza anashkuru mmama karudi I'll try asking msaidizi.... Eliminate yetu inashida haitupi ujasiri Labda wanafunzi wavuta bangi
 
Kwanza mimi siyo dogo, hivyo huna hoja ila yaelekea ni mwenyeji wa kijiweni.

Kusingizia kukwama kwa masuala mbalimbali (kwa mfano uliotoa) kuwa ni "KATIBA" kana kwamba ni "mtu" ni ishara ya uvivu, ufinyu na ufukara wa mawazo kiuhalisia wa mambo kimaisha.
Dogo siyo umri.Ulichoandika ni ujinga ndiyo maana umeitwa dogo.Tena ulipaswa kuitwa ndogo.😝😝😝😝
 
Next time Rais akisafiri asimuachie nchi huyo Makamu wake...!! Inawezekana Maza anamjua ndiyo maana hata zile safari alikuwa anamtuma Mwinyi badaya yake. Maza atakuwa kaamua kumchagua huyu bwana ili kujisafishia njia take ya 2025.
 
Back
Top Bottom