Makamu wa Rais Dkt. Mpango amemuwakilisha Rais Samia katika mkutano wa (Africa – CARRICOM Summit) uliofanyika kwa mtandao

Sabreena juma

New Member
Sep 5, 2020
3
6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hii leo Septemba 7, 2021 amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kwanza wa Afrika na Umoja wa Nchi za “Carribbean”(Africa – CARRICOM Summit) uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Akizungumza katika mkutano huo, Makamu wa Rais amesema nchi za Afrika na za “ Carribean” zinafanana katika katika masuala mbalimbali hasa katika nia ya kuhitaji maendeleo ya haraka hivyo kuwepo na ushirikiano baina nchi hizo kutaongeza kasi ya maendeleo pamoja na kuwa na sauti ya pamoja kwa manufaa ya mataifa yote ndani ya umoja huo.

Makamu wa Rais amesema Tanzania inaunga mkono mapendekezo ya kuwepo kwa siku maalum ya umoja huo pamoja kuziasa nchi washiriki wa mkutano huo kuendelea kutoa msukumo wa kupatikana kwa chanjo kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona katika nchi zinazoendelea zenye uhitaji mkubwa wa chanjo hiyo.

Mkutano huo umejadili ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo Uchumi wa Bluu, Afya, Teknolojia Mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kudhibiti Ugonjwa wa Corona.

Mkutano huo umehudhuriwa na wakuu wa nchi na serikali kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na Carribean.

1.jpg
2.jpg
3.jpg

#TwendePamoja #KwaMatokeoYaHaraka
 
Tunashukuru Mpango amejua nafasi yake siku hizi amekuwa kimya kama inavyotakiwa.
 
Uwakilishahji huu umewezekana kwa vile tu ni kwa njia ya mtandao. Kama ungekuwa ni wa nje ya nchi mama angepanda Airbus mwenyewe aende.
 
MAKAMU WA RAIS WA JMT DKT. PHILIP ISDOR MPANGO ASHIRIKI MKUTANO WA AFRICA - CARRICOM SUMMIT KWA NJIA YA MTANDAO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hii leo Septemba 7, 2021 amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kwanza wa Afrika na Umoja wa Nchi za “Carribbean”(Africa – CARRICOM Summit) uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Akizungumza katika mkutano huo, Makamu wa Rais amesema nchi za Afrika na za “ Carribean” zinafanana katika katika masuala mbalimbali hasa katika nia ya kuhitaji maendeleo ya haraka hivyo kuwepo na ushirikiano baina nchi hizo kutaongeza kasi ya maendeleo pamoja na kuwa na sauti ya pamoja kwa manufaa ya mataifa yote ndani ya umoja huo.

Makamu wa Rais amesema Tanzania inaunga mkono mapendekezo ya kuwepo kwa siku maalum ya umoja huo pamoja kuziasa nchi washiriki wa mkutano huo kuendelea kutoa msukumo wa kupatikana kwa chanjo kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona katika nchi zinazoendelea zenye uhitaji mkubwa wa chanjo hiyo.

Mkutano huo umejadili ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo Uchumi wa Bluu, Afya, Teknolojia Mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kudhibiti Ugonjwa wa Corona.

Mkutano huo umehudhuriwa na wakuu wa nchi na serikali kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na Carribean.

#TwendePamoja
#KwaMatokeoYaHaraka

IMG-20210907-WA0063.jpg

IMG-20210907-WA0065.jpg

IMG-20210907-WA0064.jpg
 
Back
Top Bottom