Makamu wa Rais benki ya dunia kutua Tanzania 27/09/2021

Ushindi victory

JF-Expert Member
Dec 11, 2018
960
1,000
HOTUBA YA MWISHO WA MWAKA YA RAIS SAMIA
itakuwa hiv......
...tumefanikiwa kupokea wagen wengii kwa mwaka mzima
....tumefanikiwa kuipromote jinsia ya kike uko dunian
....tumefanikiwa kukamata magaid ya ndani ya nchi
....tumewakomesha wavujishaji wa taharifa za ikulu, mfano bwana yule wa 2014 na mwenye icon ya Jz with kenyan flag
...tumefanikiwa kuunda njia za kukusanya kodi na kuwaziba midomo wa tz wasilalamike
....tumegawa chanjo za bure kwa wingi na weredi mkubwa
.....tumejenga mabarabara mengi(lkn hayajulkan)
.....tumefanikiwa kusafiri nchi mbalmbal ambazo kipind cha bwana yule hatukuwai fanya
....tumedumisha mahusiano na majirani
... .tumepambana na machinga pia wale wanaofanya biashara na uhujumu ktk barabara za magari mijini
.....tumefanikiwa kuunda royal tour
......tumefanikiwa kukomesha ziara za kikazi za rais uko mikoani ili kupunguza gharama zisizo za msingi
.....tumeipromote Zanzibar
Asanteni ndugu wananchi kazi iendelee

Sent from my SM-G935V using JamiiForums mobile app
 
Ushindi victory

JF-Expert Member
Dec 11, 2018
960
1,000
KUMEKUCHAA!!

Rais Samia nilisema na ninasema tena na tena huyu Mama ni habari nyingine,

Kukutana na Rais wa World Bank ni zaidi ya kuhutubia UNGA,

Mliokuwa mnalalamika kaenda mapema sasa muone aibu kwa kuchongoa midomo bila kujua nia ya Rais,

Marekani inaongoza kwa deni kubwa duniani ila kwakuwa inakopa taasisi salama ndio maana iko salama,

HAKIKA HAKUNA KAMA SAMIA
_______________________________
kikwete alikutana na marais wa dunia xhi xhing pin wa china na obama wa marekani wakubwa kulko izo takataka za world bank, je nini kilibadirika????

Sent from my SM-G935V using JamiiForums mobile app
 
Edward Sambai

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
2,824
2,000
Magufuli alikuwa anajua njia sahihi ya kuijenga nchi ila hakuweza kulijenga Taifa.

Mama nae ....................

Ccm tuoneeni huruma
 
Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
4,404
2,000
Mimi ni Chadema ila nampenda sana Rais Samia ,
Hizi ndio sera zetu Chadema ,Mama Samia anamaliza kila hoja ya Upinzani, Magufuli tulimchongea lakini Samia anafika mwenyewe kwa MABEBERU,
Huyu atawale tu mpaka 2050,
mama anfanya vizuri sana.
Agombee tena 2025.
Lakini tukikatae hicho kirusi cha ,,mpaka atakapochoka"
Hakina tija na hakina miisho myema.
 
Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
4,404
2,000
Hongera Rais na kinachofurahisha zaidi unapokopa unasema nimekopa hakuna siri
Ana lengo la kuwa muwazi ,hii ni nzuri sana kwenye utawala. Unaacha watu wanakulaumu kwa mambo madogomadogo na hutengenezi maadui. Na pia huondoa chuki.
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,054
2,000
KUMEKUCHAA!!

Rais Samia nilisema na ninasema tena na tena huyu Mama ni habari nyingine,

Kukutana na Rais wa World Bank ni zaidi ya kuhutubia UNGA,

Mliokuwa mnalalamika kaenda mapema sasa muone aibu kwa kuchongoa midomo bila kujua nia ya Rais,

Marekani inaongoza kwa deni kubwa duniani ila kwakuwa inakopa taasisi salama ndio maana iko salama,

HAKIKA HAKUNA KAMA SAMIA
_______________________________
Tumefika hapa sababu ya awamu ya 5.Pamoja na mambo mengine ila sababu kuu ya ujio wake ni hii hapa 👇

Screenshot_20210927-075145.png

Screenshot_20210927-075717.png

Screenshot_20210927-075507.png

Screenshot_20210927-075301.png

Screenshot_20210927-075426.png

Screenshot_20210927-075539.png
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,054
2,000
Haaaa,

Ivi tulikuwa tunakwenda wapi?

Mungu Asante kwaajili ya Samia
Sijui mwendazake na genge lake,badala ya kusapoti sekta zilizoathirika uchumi usianguke yeye anahangaika na kusema sijui Mungu sijui malaika mara nyingu mambo ya kijinga.

Nilisoma andiko fulani inaonesha robo ya mwisho ya 2020 na robo ya kwanza uchumi ulikuwa kwa 1% tuu huku Jiwe akidanganya watu eti unakua kwa 7% ,ndio chanzo hasa cha kuanza kupora pesa za watu..

Saizi mama anahangaika kiasi kwamba wanasema import bill inakua kubwa kwa sababu ya bei za mafuta duniani kuwa kubwa na weak export ya uchumi wetu kwamba gold exports haiwezi kufidia gap..

Mbaya zaidi unaambiwa zaidi ya bil.500 zinatumika kuagiza mafuta ya kula nje bado sukari ,bado mbolea nk ..

Tuombe tuu wawekezaji walioanza kuingia wasaidie ,hope by 2022 labda ndio uchumi utaanza kuonesha dalili za improvement.Ila utalii utaendelea kuanguka kama juhudi za chanjo hazitafanikiwa maana nchi imewekwa kwenye red line na chanjo hatutaki kwa sababu za propaganda za Jiwe na wapuuzi wenzie.
 
kipande

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
2,128
2,000
Masaa machache baada ya Rais Samia kuhutubia UN Gen Assembly huko New York Marekani na kurejea nchini || Sasa rasmi Makamu wa Rais benki ya dunia kutua Tanzania 27|28|09|2021.
____________________________________________
Makamu wa Rais wa benki ya dunia anayeshughulikia Ukanda huu wa Mashariki na kusini Mr Hafez Ghanem anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili nchi Tanzania yaani trh 27|28|2021 ikiwa ni matoke ya Rais Samia kusafiri nje ( Mtembea bure si sawa na mkaa bure) ,

Mr Hafez Ghanem ambae ni raia wa Misri|Ufaransa ni mtu mwenye uzoefu sana kuhusu miradi ya maendeleo kwa zaidi ya miaka 30,anasimamia nchi za kusini na Mashariki 26 zenye jumla ya miradi 280 yenye thamani ya $49BL karibu Tshs 112.7trilioni ikiwemo miradi yetu 21 yenye thamani ya $4.8BL sawa na Tshs 11.04trillion,

Ziara ya Hafez Ghanem inafuatia kikao cha Rais wetu Samia Suluhu Hassan na Rais wa benki ya dunia Mr David Malpass trh 21|09|2021,Hapa Wale mliokuwa mnalalamika Mhe Rais kawahi Sana kwenda New York fuatilieni vizuri ziara ya Mr Hafez Ghanem mtaelewa kwanini aliwahi,

Mhe Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais huyo wa Bank ya dunia walijadili juu ya juhudi zinazofanywa na Tanzani katika kukabiliana na madhara yatokanayo na janga la Covid -19 pamoja na kuongeza juhudi ya utoaji chanjo lakini pia kuzijengea uwezo sekta binafsi baada ya huu mdororo wa Uchumi chanzo kikiwa ni Corona,

Chanzo hiki kinaonesha Benki ya dunia imeonesha nia ya kuisaidia Tanzania kwenye ununuzi,usafirishaji na usambazaji wa chanjo ya Covid -19 kupitia Shirika lake tanzu la fedha la International Developed Assistance ( IDA) ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya biashara ili kuzisaidia sekta binafsi katika kujijenga Upya,

Kwamsiojua, Banki ya dunia inafadhili miradi kama Usafirishaji, Makazi, Elimu, Nishati, Maji,Uhifadhi wa kijinsia, mazingira, mali asili, maendeleo ya teknolojia pamoja na Utawala,

Kwa msiofahamu banki ya dunia iligoma kutupa misaada na mikopo kwa kipindi flani kiasi ambacho ilitulazimu tuanze kukopa mikopo yenye masharti ya kibiashara ambayo ni hatari zaidi kwa Ustawi wa Uchumi wa nchi yetu hasa mikopo toka China,Wote mnajua,Leo hii Wachina wako mbioni kuichukua bandari ya Mombasa ya Kenya kisa marejesho ya Mikopo yenye masharti ya kibiashara,

Riba na muda wa marejesho kwa mkopo wa World Bank ni nafuu sana, Mfano IDA shirika tanzu la World Bank wao riba yao ni 1.56% tu na muda wa marejesho ni hadi miaka 38,hii ni sawa na kusema World Bank wakikupa mkopo leo wa Tshs 100,000 utalazimika kuwalipa|kurejesha jumla ya Tshs 102,000 sawa na riba ya Tshs 2,000 tu kwa miaka 38,Kwa lugha rahisi World Bank ni sawa na kusema hawana riba ila wanakupa pesa ujenge miradi then uirudishe pesa yao, seriously am speechless vile Rais Samia anaupiga mwingi kwa Usahihi mkubwa huu,

Tukubaliane tu,kwa mwendo huu wa connections za Rais Samia kidunia mpaka kufikia 2030 Uchumi wa nchi hii utakuwa ni wakupigiwa mfano duniani,Tumuunge mkono Rais wetu kwa kufanya kazi kwa bidii.

.........Kazi iendelee .........

VIVA TANZANIA VIVA || VIVA SAMIA VIVA [/B]

View attachment 1953360
Ndugu unatumia nguvu nyingi sana kutuaminisha propaganda zako. Kuna Mkaa bure alitekeleza miradi lukuki kwa kipindi kifupi sana bila kuwafuata hao mabwanyenye huko nje na kufuata masharti yao ya Covid 19. Tena wengine walikua wanakuja wenyewe hapa nchini.
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
15,359

Ni ziara ya kawaida ya kikazi na biashara kwa Benki hii ya dunia kutoa mikopo na kukusanya riba ya kibiashara kadri fursa inapotokea. Hayati mwendazake Rais John PombeJoseph Magufuli alifanya kazi na Benki hii bila kufika makao makuu yao Washington DC wala kukutana naye katika vibaraza vya nje ya kumbi za Umoja wa Mataifa ambapo pia wafanyabishara wa mabenki au kampuni kubwa kama za Johnson & Johnson, Google, Microsoft, General Electric, Boeing n.k wanapigana vikumbo katika "Gulio - Kuu " kukutana na viongozi wa nchi mbalimbali kutafuta fursa za kibiashara. Wasipopata nafasi hiyo watakufuata kwenu kama walivyomfuata rais John Magufuli Ikulu Tanzania :

TOKA MAKTABA : 16 November 2018​

DKT HAFEZ GHANEM AMESEMA BENKI YA DUNIA IMERIDHIA KUTOA DOLA MILIONI 300 KWA TANZANIA
Video : Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Dr. Hafez M.H Ghanem aliyekutana na Mhe. Rais Magufuli tarehe 16 Novemba, 2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Dr. Hafez M.H Ghanem amesema pamoja na kuridhia kutoa fedha US$300 million za mradi huo, Benki hiyo inaendelea kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 5.2 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 13 na kwamba miradi hiyo inatekelezwa kutokana na uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati yake na Tanzania. Dkt. Hafez Ghanem amesema katika mazungumzo hayo wamejadili juu ya maendeleo ya miradi hiyo na kazi nzuri ambayo inafanywa na Tanzania kuimarisha uchumi, na pia amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa matokeo mazuri ya mapambano dhidi ya rushwa na kuimarisha huduma za kijamii.

Source : Ikulu Tanzania 16 Nov 2018
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
12,954
2,000
Masaa machache baada ya Rais Samia kuhutubia UN Gen Assembly huko New York Marekani na kurejea nchini || Sasa rasmi Makamu wa Rais benki ya dunia kutua Tanzania 27|28|09|2021.
____________________________________________
Makamu wa Rais wa benki ya dunia anayeshughulikia Ukanda huu wa Mashariki na kusini Mr Hafez Ghanem anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili nchi Tanzania yaani trh 27|28|2021 ikiwa ni matoke ya Rais Samia kusafiri nje ( Mtembea bure si sawa na mkaa bure) ,

Mr Hafez Ghanem ambae ni raia wa Misri|Ufaransa ni mtu mwenye uzoefu sana kuhusu miradi ya maendeleo kwa zaidi ya miaka 30,anasimamia nchi za kusini na Mashariki 26 zenye jumla ya miradi 280 yenye thamani ya $49BL karibu Tshs 112.7trilioni ikiwemo miradi yetu 21 yenye thamani ya $4.8BL sawa na Tshs 11.04trillion,

Ziara ya Hafez Ghanem inafuatia kikao cha Rais wetu Samia Suluhu Hassan na Rais wa benki ya dunia Mr David Malpass trh 21|09|2021,Hapa Wale mliokuwa mnalalamika Mhe Rais kawahi Sana kwenda New York fuatilieni vizuri ziara ya Mr Hafez Ghanem mtaelewa kwanini aliwahi,

Mhe Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais huyo wa Bank ya dunia walijadili juu ya juhudi zinazofanywa na Tanzani katika kukabiliana na madhara yatokanayo na janga la Covid -19 pamoja na kuongeza juhudi ya utoaji chanjo lakini pia kuzijengea uwezo sekta binafsi baada ya huu mdororo wa Uchumi chanzo kikiwa ni Corona,

Chanzo hiki kinaonesha Benki ya dunia imeonesha nia ya kuisaidia Tanzania kwenye ununuzi,usafirishaji na usambazaji wa chanjo ya Covid -19 kupitia Shirika lake tanzu la fedha la International Developed Assistance ( IDA) ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya biashara ili kuzisaidia sekta binafsi katika kujijenga Upya,

Kwamsiojua, Banki ya dunia inafadhili miradi kama Usafirishaji, Makazi, Elimu, Nishati, Maji,Uhifadhi wa kijinsia, mazingira, mali asili, maendeleo ya teknolojia pamoja na Utawala,

Kwa msiofahamu banki ya dunia iligoma kutupa misaada na mikopo kwa kipindi flani kiasi ambacho ilitulazimu tuanze kukopa mikopo yenye masharti ya kibiashara ambayo ni hatari zaidi kwa Ustawi wa Uchumi wa nchi yetu hasa mikopo toka China,Wote mnajua,Leo hii Wachina wako mbioni kuichukua bandari ya Mombasa ya Kenya kisa marejesho ya Mikopo yenye masharti ya kibiashara,

Riba na muda wa marejesho kwa mkopo wa World Bank ni nafuu sana, Mfano IDA shirika tanzu la World Bank wao riba yao ni 1.56% tu na muda wa marejesho ni hadi miaka 38,hii ni sawa na kusema World Bank wakikupa mkopo leo wa Tshs 100,000 utalazimika kuwalipa|kurejesha jumla ya Tshs 102,000 sawa na riba ya Tshs 2,000 tu kwa miaka 38,Kwa lugha rahisi World Bank ni sawa na kusema hawana riba ila wanakupa pesa ujenge miradi then uirudishe pesa yao, seriously am speechless vile Rais Samia anaupiga mwingi kwa Usahihi mkubwa huu,

Tukubaliane tu,kwa mwendo huu wa connections za Rais Samia kidunia mpaka kufikia 2030 Uchumi wa nchi hii utakuwa ni wakupigiwa mfano duniani,Tumuunge mkono Rais wetu kwa kufanya kazi kwa bidii.

.........Kazi iendelee .........

VIVA TANZANIA VIVA || VIVA SAMIA VIVA [/B]

View attachment 1953360
Kumbe hujui kuwa rais (siyo makamu) wa benki ya dunia aliwahi kumtembelea Magufuli pia? Soma hapa kwenye rekodi za world bank.

Kwa wao kutembelea wateja wao siyo jambo la ajabu, na wala hawafuati siasa za nchi bali wanafuata maslahi yao.
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
15,359
2,000
Baada ya mazungumzo haya ya New York, sasa Benki ya Dunia yafuatilia agenda zilizokubaliwa

September 22, 2021​

Mhe. Rais Samia akutana na kuzungumza na Viongozi mbalimbali UN​
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais wa Benki ya Dunia Bw. David Malpass, walipokutana katika ufunguzi wa mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UN Jijini New York Nchini Marekani leo Sept 21,2021. Source : Picha na Habari kwa hisani kubwa ya IKULU.
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
15,359
2,000
STATEMENT SEPTEMBER 21, 2021

Readout from World Bank Group President David Malpass’s Meeting with President Samia Suluhu Hassan of Tanzania​

NEW YORK CITY, September 21, 2021—This afternoon, World Bank Group President David Malpass met with President Samia Suluhu Hassan of Tanzania.

President Malpass and President Hassan discussed the World Bank’s support to Tanzania in its efforts to mitigate the impacts of the COVID-19 pandemic and accelerate vaccinations.

President Malpass affirmed the World Bank’s willingness to support vaccine procurement, uptake, and deployment through IDA.

President Malpass encouraged Tanzania’s efforts to improve the business environment and facilitate private sector-led growth through regulatory reforms.

President Malpass raised the importance of electricity access, affordable housing, and digital infrastructure, including through regional solutions to improve efficiency and create more competitive markets.

President Malpass also emphasized the importance of debt transparency and encouraged careful selection of investment programs and their financing sources.

Source : Readout from World Bank Group President David Malpass’s Meeting with President Samia Suluhu Hassan of Tanzania

Source :
David R. Malpass was selected as 13th President of the World Bank Group by its Board of Executive Directors on April 5, 2019. His five-year term began on April 9.
David Malpass
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
15,359
2,000
Kumbe hujui kuwa rais (siyo makamu) wa benki ya dunia aliwahi kumtembelea Magufuli pia? Soma hapa kwenye rekodi za world bank.

Kwa wao kutembelea wateja wao siyo jambo la ajabu, na wala hawafuati siasa za nchi bali wanafuata maslahi yao.

Umefafanu vizuri mahusiano ya haya mabenki ya kimataifa na shughuli zao. Pia huja na masharti magumu kwa serikali ya Tanzania kama uwazi wa takwimu, mimba za wasichana wanafunzi, kuondoa ubaguzi na masuala mengine magumu ambayo hata hayati mwendazake rais John Pombe Joseph Magufuli aliyakubali kwa shingo upande. Sasa mwaka huu 2021 mwezi September sijui hawa jamaa ndiyo wanafuatilia utekelezwaji wa masharti yao.. magumu ya 'kibeberu'...

TOKA MAKTABA:

MAGUFULI AKUBALI MKOPO KWA SHINGO UPANDE WA US$ 300m

16 November 2018
Ikulu Dar es Salaam

Magufuli's concessions to the World Bank over $300m loan​

Vice president of the World Bank for Africa Dr. Hafez M. H Ghanem appreciate efforts made by president of Tanzania Dr. John Pombe Magufuli in fighting corruption

The World Bank’s vice president for Africa Hafez Ghanem has revealed the details of his discussions with Tanzania’s president John Magufuli, that will lead to the disbursement of a $300m loan towards education projects.

On Wednesday last week, the World Bank said it had not presented the education programme to its board for financing approval last month after the country reaffirmed its policy of banning pregnant girls from school and made it a crime to question official statistics.

READ MORE: EU, Denmark, World Bank review relations with Tanzania

On Friday, Magufuli met with Ghanem and announced thereafter that the World Bank was not scrapping the $300m loan.
He insisted it had actually not been withdrawn, blaming the confusion on ‘persons who did not wish the country well’.

READ MORE: Tanzania govt says World Bank not scrapping $300m loan

Before leaving for the World Bank headquarters in Washington on Saturday, Ghanem revealed details of the meeting with Magufuli to the local Citizen newspaper.

Pregnant girls in school
Ghanem said the World Bank had agreed with Magufuli that the education project is redesigned to find a way for pregnant girls to return to school.

‘’...girls’ education is central to development, we are a development institution. We cannot accept that some girls are denied education,’‘ explained Ghanem.

Tanzania has banned pregnant girls from attending state primary and secondary schools since 1961. Magufuli affirmed his commitment to this policy last year, saying school girls who become pregnant must be expelled and not allowed to return.

Ghanem added that the project would still be subject to board approval before the funds could be disbursed.

Statistics law
The World Bank had also expressed concerns over the Statistics Law passed by the Tanzanian parliament in September.

At the time it was passed, the global lending institution said the law that would punish anyone who questions official statistics, could ‘undermine the production of useful and high quality data’.

READ MORE: World Bank could suspend funding to Tanzania over new statistics law

Ghanem said the government in Friday’s meeting, gave the World Bank assurances that it was open to discussion on implementation of the law.

‘‘We need statistics that are reliable and credible because all our decisions and analyses are based on statistics,’‘ argued the World Bank official.
‘’...our technical team and statisticians are working with the government on the details.’‘

Discrimination against gay community
Asked about the World Bank’s stance on the issue of human rights and discrimination against the gay community in Tanzania, Ghanem said Tanzania had committed to non-discrimination based on race, ethnicity, gender and sex orientation.

According to the World Bank, Tanzania was one of the countries that approved the World Bank’s Environment and Social Framework last month. One of the principles provided for in this framework is non-discrimination.

‘‘On the case of human rights, and LGBTI, the government reassured that there would be no more discrimination against people of any ethnicity, religion or sex orientation.’‘

The World Bank official declined to comment on the state of democracy and press freedom, saying the institution does not discuss political issues. Source : Magufuli's concessions to the World Bank over $300m loan | Africanews

Source:
Dr. Hafez M.H Ghanem began his career at the World Bank in 1983 as a Young Professional. Over the span of 24 years (1983-2007),
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
15,359
2,000

28.09.2021​

Dkt. Mpango akutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia​

Dr john Masawe
Dr john Masawe
2 hours ago

Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hii leo Septamba 28, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt Hafez Ghanem Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais Dkt. Mpango amemuhakikishia Dkt. Ghanem kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana na Benki hiyo katika masuala mbalimbali ya kuinua uchumi hapa nchini.

Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema kwamba serikali ya awamu ya sita imeweka kipaumbele katika kuinua sekta binafsi pamoja na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji hapa nchini. Amesema mpango wa maendeleo wa miaka mitano umelenga kuinua sekta ya viwanda hapa nchini hivyo serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kufanikisha hilo.

Aidha Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema ili kukidhi mahitaji ya sekta binafsi hapa nchini serikali imeweka mkazo katika sekta ya elimu hasa elimu ya ufundi ili kupata wahitimu wenye ujuzi watakaoweza kusaidia kuinua sekta hiyo.

Makamu wa Rais amesema serikali ya awamu ya sita imeendelea kuimarisha utawala bora pamoja na kudhibiti rushwa hapa nchini hivyo kuweka mazingira rafiki ya kutekeleza miradi mbalimbali.

Kwa upande wake makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Hafez Ghanem ametaja maeneo ambayo benki hiyo itashirikiana na Tanzania ambayo ni pamoja na uboreshaji miundombinu, , mapambano dhidi ya uviko19 pamoja na kuinua uchumi baada ya janga la Uviko 19.
Source : Dkt. Mpango akutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom